To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Majanga
Utangulizi
Majanga ni hatari sana katika maisha ya watu. Majanga haya hutokea bila Sisi kutambua. Hali huenda ikawa shwari na ya kawaida asubuhi na ikapindukia kuwa hatari jioni na kuwaangamiza watu wengi katika eneo kubwa. Je, umewahi kushuhudia janga lolote katika nchi yako? Je, unaweza kutaja mifano yoyote ya majanga? Unafikiri majanga yana manufaa yoyote kwa jamii au yana hasara pekee? Mada hii itakuwezesha kukuza msamiati unaohusiana na majanga na pia kukuwezesha kujihadhari na majanga kwa
kutumia njia zinazoweza kuzuia majanga kutokea.
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua msamiati muhimu wa majanga
Utangulizi
Katika utangulizi wa mada hii, umetambua kuwa majanga ni hatari katika jamii na hutokea na kuathiri eneo kubwa na kuathiri watu wengi. Ni jambo gani ambalo limewahi kutokea katika eneo unakotoka na kila mtu akaanza kulalamika kuhusu jambo hilo? Je, umewahi kutambua majanga ambayo yaliwahi kuathiri jamii yako? Je, Umewahi kusikia au kuona majanga yaliyoangamiza maisha ya watu, kuharibu mazao, wanyama, nyumba au hata afya za watu? Mada ndogo hii itakuwezesha kujibu maswali haya na mengine yanayohusiana na mada hii.
) Shughuli 2.1
Kutambua msamiati wa majanga
Katika vikundi, tazameni picha hizi na kutambua kwa neno moja hali ya kitendo
Baadaya kutambua msamiati, tunga sentensi moja kwa kila picha kueleza hali.
Taz: Umetambua msamiati wa majanga ambayo yamekuwa yakiathiri watu katika jamii zetu. Utaweza kutambua dalili za utokeaji wa hali kama hizi na kujihadhari nayo.
Stadi za lugha: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
Funzo b: Kutaja sehemu zilizowahi kukumbwa na
majanga nchini
Kuna majanga mengi sana ambayo hutokea katika mazingira yetu. Hata hivyo baadhi ya majanga huweza kutokea katika sehemu fulani fulani lakini sio kila mahali. Je, umewahi kushuhudia kutokea kwa janga lolote nchini kwako? Unaweza kueleza kilichosababisha kutokea kwa janga hilo? Mada hii itakuwezesha kutambua na kueleza juu ya majanga ambayo yamewahi kutokea nchini Uganda.
Shughuli 2.2 Kutaja Sehemu zilizoshuhudia majanga nchini
Katika vikundi, tambueni na kutaja mahali ambapo majanga yanayoonyshwa katika picha zifuatazo yalitokea.
2.Elezeni mahali ambako majanga haya hutokea kila mara
a) Mafuriko b) Maporomoko ya ardhi c) Ukame
3.Kuna majanga ambayo hayajawahi kutokea Uganda na Afrika bali
hutokea sana katika nchi za mbali. Tambueni aina za majanga na
mahali ambako mmewahi kusikia zikitokea.
4.Majanga mengine hutokea sana katika mazingira yetu. Hata mengi yanaweza kutokea mahali tuliko. Je, mnaweza kuyatambua na pia kutambua mahali ambako ni rahisi majanga haya kutokea?
5.Katika vikundi jadiliana majanga ambayo yaliwahi kutokea katika mazingira yenu aidha unakoishi, kijijini ama mjini.
Taz: Katika funzo hili umeweza kutambua majanga mbalimbali na kutambua mahali ambako yamewahi kutokea. Aidha umeweza kutambua kuwa baadhi ya majanga hutokea katika eneo la kijiografia maalumu na mengine ni majanga ambayo yanaweza kutokea popote. Kwa kutumia maarifa haya unaweza
kujikinga na kukinga jamii yako kutokumbwa na majanga haya.
3.Elezeni mahali ambako majanga haya hutokea kila mara
a) Mafuriko b) Maporomoko ya ardhi c) Uka
3.Kuna majanga ambayo hayajawahi kutokea Uganda na Afrika bali hutokea sana katika nchi za mbali. Tambueni aina za majanga na mahali ambako mmewahi kusikia zikitokea.
4.Majanga mengine hutokea sana katika mazingira yetu. Hata mengi yanaweza kutokea mahali tuliko. Je, mnaweza kuyatambua na pia kutambua mahali ambako ni rahisi majanga haya kutokea?
5.Katika vikundi jadiliana majanga ambayo yaliwahi kutokea katika mazingira yenu aidha unakoishi, kijijini ama mjini.
Taz: Katika funzo hili umeweza kutambua majanga mbalimbali na kutambua mahali ambako yamewahi kutokea. Aidha umeweza kutambua kuwa baadhi ya majanga hutokea katika eneo la kijiografia maalumu na mengine ni majanga ambayo yanaweza kutokea popote. Kwa kutumia maarifa haya unaweza
kujikinga na kukinga jamii yako kutokumbwa na majanga haya.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo c: Kujadili chanzo na sababu za kutokea kwa majanga
Utangulizi
Majanga yanayotokea huwa yanasababishwa na mambo mengi; mengine hutokana na shughuli za binadamu na mengine ni kwa sababu za asili. Je, unaweza kueleza chanzo cha majanga mbalimbali? Katika mada ndogo hii, utajifunzi vianzo vya majanga yanayotokea ili upate kuhadhari kabla ya hatari.
Kujadili sababu zinazoleta majanga
Taz: Mjadala huu umekuwezesha kujifunza vyanzo na sababu za kutokea kwa majanga. Unafaa kukumbuka kuwa, baadhi ya majanga yanayotokea katika mazingira yetu hutokana na mazingira yenyewe, yaani, ni majanga ya asili ambayo binadamu hana uwezo wa kuyazuia na mengi ni majanga
yanayosababishwa na binadamu.
Baada ya somo hili, jishughulisheni na kutafiti juu ya mikakati ya kuzuia majanga kwa jamii yenu. Mnaweza kutumia mtandao wa intaneti na hata maktaba.
Funzo d: Kujadili njia mbalimbali za kuepukana na
majanga hayo
Utangulizi
Majanga mengi husababisha madhara makuu katika jamii zetu. Hata hivyo, baadhi ya majanga haya yanaweza kuepukika. Je, ni kweli kuwa tunaweza kujiepusha na majanga haya na madhara yake? Majanga hutokea mahali ambako yanaweza kutokea. Hata hivyo, baadhi ya majanga yanaweza
kuepukika. Je, umewahi kuzuia janga lolote kutokea katika jamii yako? Je, unaweza kuelezea njia ambazo ulitumia kuzuia janga husika? Katika mada ndogo hii, utajifunza jinsi ya kuweza kukomesha majanga kutokea.
Shughuli 2.4
1.Kueleza Matokeo ya majanga katika taifa Mkiwa katika vikundi, tazameni picha zifuatazo kwa makini. Jadiliana kuhusu kinachotendeka katika kila picha.
Taz: Katika kueleza matokeo ya majanga, umeweza kutambua kuwa majanga ni hatari sana katika maisha yetu. Vilevile, unafaa utambue kuwa majanga yanavyotokea, huathiri mazingira yetu, wanyama, mimea, binadamu hata na uchumi wa serikali yetu. Kwa hivyo, ni muhimu kulinda mazingira yetu na
kujilinda kwa ajili ya kuepukana na athari za majanga katika mazingira yetu.
Shughuli 2. Kujadili njia za kukomesha majanga
Katika vikundi, shirikiana na kutaja matokeo ya majanga ambayo
yamewahi kutokea katika jamii zetu.
Elezeni jinsi matokeo hayo yanavyotokea.
Katika vikundi, jadiliana njia za kuweza kuzuia majanga yafuatayo:
a) Moto
b) Mafuriko
2.Mbali na majanga haya mawili katika 1 hapo juu, tambueni majanga mengine na kujadiliana kuhusu jinsi tunaweza kukomesha majanga
hayo kutotokea katika jamii.
3.Wasilisheni njia ambazo zinaweza kukomesha majanga.
Taz: Katika funzo hili, umejifunza kuwa kuna majanga ya asili ambayo binadamu hana uwezo wa kuzuia ila anastahili tu kuepukana nayo kwa kutokaribia mazingiraya majanga husika. Aidha umetambua kuwa majanga yanayoweza kukomeshwa haraka ni majanga ambayo husababishwa na binadamu.
Stadi za lugha: kusoma
Funzo e: Kusoma makala na kujibu maswali juu ya majanga
Utangulizi
Maporomoko ya ardhi yamekuwa yakitokea sana katika maeneo ya Bududa, Kigezi na sehemu nyinginezo nyingi. Je, unajua katika dira ya Uganda mahali ambako maeneo haya yanapatikana? Je, unaweza kutambua ni mara ngapi majanga haya yametokea katika sehemu hizi? Mada ndogo hii itakuwezesha kutambua Wilaya ambazo zimeathirika sana na majanga.
Shughuli 2.6
Soma makala haya kuhusu maporomoko ya ardhi katika Wilaya ya Bududa, Kigezi na sehemu zinginezo.
Maparomoko ya ardhi ni hali ya ardhi kumegeka na kuangukia watu,mimea na wanyama. Maporomoko ya ardhi husababisha madhara makubwa kwa jamii na kusababisha utegemezi wa hali ya juu pamoja
na kurudisha maendeleo ya nchi nyuma. Maparomoko ya ardhi ni hatari sana katika maisha ya watu hasa wanaoishi katika maeneo ya milimani. Maporomoko ya ardhi nchini Uganda hutokea zaidi katika
maeneo ya Mashariki hasa, Kapchorwa, Kwen, Bukwo, Bulambuli, Budadi/i, Manafwa, Namisindwa na Bududa. Hata hivyo, Bududa imeathirika mara nyingi zaidi kuliko maeneo mengine.
Aidha, katika maeneo ya Kigezi, maporomoko ya ardhi hutokea sana Kisoro na Rwenzori. Maeneo haya hujikuta katika hali moja na ya Mashariki. Mlimani Rwenzori, kumeripotiwa janga la maporomoko ya ardhi hasa katika kijiji cha Bukumbya, tarafa ya Mahango, wilayani Kasese. Maporomoko
ya ardhi yanapotokea katika maeneo haya, husababisha mito kufurika na kubeba mawe na udongo na kusababisha maafa zaidi. Kwa mfano, katika Wilaya ya Kasese, Mito ya Nyamwamba, Rwimi, Mubuku, na Nyamugasani hufurika na kuja yakiwa na maporomoko ya mawe mazito ambayo hugonga
nyumba na mwisho kuwauwa wakaazi wa maeneo haya. Septemba mwaka wa elfu mbili na kumi na tisa, watu zaidi ya watano katika Wilaya ya Kisoro walisukumwa na kupelekwa na maporomoko ya
ardhi. Miili ya watu hawa watatu ilipatikana katika Mto Rwafi. Manusura walipelekwa hospitalini. Maeneo ambayo ni hatari kwa maporomoko ya ardhi katika sehemu hii ya Kigezi ni Wilaya ya Rukiga, kijiji Cha Mugambira, Bikokora, Mugombwa, mtaa wa Nteko, tarafa ya Nyabwishenya na
sehemu nyinginezo za Kigezi kukiwemo Rubanda na Kisoro. Maporomoko ya ardhi ya/iyotokea zaidi na kuvunja rekodi ya yale yaliyitokea Mashariki mwa Uganda. Maporomoko haya kwanza
yaliangamiza kijiji kizima na baadaye kuwaua watu zaidi ya hamsini. Tukio hili lilitokea mchana saa nane katika Wilaya ya Bududa, kijiji Cha Buka/asi, maeneo ya Mlima wa Elgon. Maji, udongo pamoja na miti, yaliyo poromoka kutoka mlimani hadi chini mtoni, kufunika makao ya watu hadi sehemu tambarare,na kusababisha maafa makubwa mkiwemo mimea na mifugo kuzikwa.
wakiwa hai. Duru za habariziliripoti kuwa watu zaidi ya 500 wamelazimika kuyahama makaazi yao kwa hofu ya kuzikwa na udogo kwani hata nyumba zao hazionekani. Sababu za maafa haya yalitokana na mvua i/iyonyesha kwa masaa manne na kusababisha mto Suume kufurika na kuvunja kingo zake na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi. Kwa jum/a, kuanzia mwaka 1997, 2010, 2012 hadi 2019, zaidi ya watu 400 wamefariki na kugharimu nchi zaidi ya bilioni 35 kwa ajili ya kuokoa
maisha ya watu katika eneo hi/i la maporomoko ya ardhi. Maeneo ya/iyoathirika na majanga haya sehemu ya Mashariki ni Bu/ucheke, Busi/iwa, Bumasifa, Buluganya, Bududa, Bushika, Bukalasi,
Bumwa/ukani, Busika, Kato, Nametsi katika Wilaya ya Bududa, Manafwa na Namisndiwa. Katika Wilaya ya Kapchorwa, Kwen, Bu/ambu/i na Sironko, maeneo ya/iyoathirika zaidi na maporomoko ya
ardhi ni Zesui, Buginyanya, Bumasifwa, Buluganya, Masila, Bulago, Buyobo, Buwa/asi, Butandiga, Busika, Busulani, Namusuni, Lusya na Sisiyi katika Wilaya za Bulambuli na Sironko.
Kwe/ijanga la maporomoko ya ardhi ni hatari sana. Hata hivyo wananchi wanafaa kue/imishwa na kutambua masua/a ya kupanga uzazi. Hii ni kwa sababu maeneo haya ni maeneo yenye idadi kubwa ya watu. Pili wanafaa kue/imishwa kupata ripoti juu ya hali ya hewa kutoka katika Wanaanga na kuchukua tahadhari ya kuepuka sehemu hizo wakati wa mvua. Aidha, serika/i inastahili kuweka mikakati ya kuwaondoa wahasiriwa na wale waliokata/ia katika maeneo haya kwa madai kuwa ni asi/i yao. Ni vyema kutahadhari kabla ya hatari kuliko kujidai kama Juliasi Kaiziri aliyedai kuwa yeye ni hatari ku/iko hatari yenyewe.
1.kujibu maswali kuhusiana na habari
Shughuli 2.7
1.Katika vikundi, jadiliana juu ya maeneo ya Bududa na Kigezi ambako maporomoko ya ardhi hutokea sana.
2.Elezeni kwa nini maeneo haya huathirika zaidi na maporomoko ya ardhi. Ni madhara gani ambayo yamesababishwa na utokeaji wa maporomoko ya ardhi katika maeno haya?
4.Mnafikiri, mbali na maporomoko ya ardhi, ni majanga gani mengine ambayo huathiri jamii?
5.Maporomoko ya ardhi yanaweza kutokea kutokana na mazingira au shughuli za binadamu. Elezeni.
6.Kwa maoni yako unafikiri, ni njia gani mwafaka ambazo zinaweza kutumika kuzuia janga la maporomoko ya ardhi kutokea katika maeneo yaliyotajwa katika hadithi?
Taz: Mmesoma juu ya maporomoko ya ardhi katika Wilaya ya Bududa, Kigezi na maeneo mengineyo. Katika usomaji wenu mmeweza kujadiliana na kueleza kuhusu maeneo haya na yanakopatikana kwenye dira ya Uganda. Ni vizuri kujua kuwa majanga haya yanaweza kutokea kokotenchini Uganda, sio Bududa au Kigezi pekee. Hata kwenu yanaweza kutokea. Kwa hivyo, ni vizuri kujihadhari kabla ya hatari.
Stadi za lugha: kusoma na kuandika
Funzo f: Sarufi – Kutunga sentensi kutumia hali ya
Mazoea na Ukanushaji Wake
Utangulizi
Je, unajua hali ya mazoea ni hali gani? Kila siku wewe hula chakula, huoga, hupiga mswaki na kadhalika. Je, unaweza kueleza hali hiyo katika hali ya mazoea? Ikiwa dada yako au rafiki yako anapenda kuimba kila asubuhi
akiamka na kuimba UnaWeZa kutunga kueleza kitendo chake cha kila siku? Mada ndogo hii itakuwezesha kutunga sentensi katika hali ya mazoea katika mtindo wa kukubali na kukanusha.
I.Kutumia hali ya mazoea na kukanusha
Katika vikundi tambueni matumizi ya hali ya mazoea katika sentensi zifuatazo:
a) Mpishi hutupikia chakula shuleni.
b) Majanga ya moto hutokea sana jikoni, viwandani na shuleni.
c) Ardhi huporomoka sana mahali pa milimani.
d) Kolera hutokea wakati wa mvua na mafuriko.
2.Kanusheni sentensi zifuatazo:
a) Maporomoko ya ardhi hutokea sana maeneo ya Kigezi na Bududa.
b) Wahasiriwa wa majanga huteseka sana nchini.
c) Waziri mkuu huwatembelea wahasiri wa majanga kila ikitokea.
d) Daktari huwatibu wagonjwa hospitalini.
3.Ni mabadiliko yapi ambayo mmegundua baada ya kukanusha sentensi hizo?
4.Katikajozi, andikianeni sentensi mbili katika hali ya mazoea na kuzikanusha.
5.Katika jozi, mmoja ataje sentensi akitumia hali ya mazoea namwingine aikanushe.
6.Kanusha sentensi hizi katika hali ya mazoea, mtindo wa kukubali.
a) Muuguzi hauguzi wagonjwa waliolazwa.
b) Wazazi wangu hawaendi kazini kila siku.
Taz: Katika funzo hili, umejifunza kuwa kukanusha ni kukataa jambo. Kile ambacho unastahili kutambua ni kuwa ukanushaji huzingatia ngeli, njeo na hali. Katika ukanushaji wa hali ya mazoea, umetambua kuwa
hali hii huwakilishwa na kiambishi h- ambacho hutokea mwanzoni mwa kitenzi. Aidha ni muhimu kutambua kuwa ukanushaji wa hali ya mazoea, hufuata ukanushaji wa wakati uliopo.
Stadi za lugha: kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika Funzo g: Kutumia Viwakilishi vya nafsi katika sentensi
Utangulizi
Katika mazingira ya utendaji wa matendo, kuna watu watatu. Mtu wa kwanzakatika utendaji ni mimi (kwa umoja) na Sisi (kwa wingi) katika utendaji. Mtu wa pili katika utendaji wa mambo ni wewe (kwa umoja) na nyinyi (kwa wingi) na mtu wa tatu katika utendaji ni yeye (kwa umoja) na wao (kwa wingi). Je, ikiwa
ni wewe unayecheza mpira utamwelezaje mwenzako anayekuuliza kitendounachofanya? Je, ikiwa mwenzako ndiye anayecheza, wewe utanielezajekuwa mwenzako ndiye anafanya kitendo cha kucheza mpira? Na ikiwa wewena mimi hatuchezi mpira lakini mtu wa tatu ndiye anayecheza, utasemaje?
Mada ndogo hii itakuwezesha kujifunza mengi kuhusu viwakilishi vya nafsi nanamna ya kuvitumia katika mawasiliano ya kila siku.Kutambua viwakilishi vya sifa na kuvitumia katika sentensi
1.Katika jozi, tambueni viwakilishi vya nafsi ya kwanza, ya pili na ya tatukwa umoja na wingi.
2.Tungeni sentensi tatu kwa umoja na wingi kwa kutumia viwakilishi nafsi.
3.Kwa kutumia viwakilishi vya nafsi, tungeni sentensi kutokana na picha hizi.
Taz: Katika funzo hili, umetambua kuwa viwakilishi vya nafsi ni maneno yanayotumika kuwakilisha mtendaji au nomino. Aidha, umetambua kuwa viwakilishi hivi ni vitatu kwa umoja na vitatu kwa wingi.
Fasili simulizi
Stadi za lugha: kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
Funzo h: Kukamilisha na kueleza maana za methali mbalimbali kuhusiana na majanga
Utangulizi
Katika enzi za mababu zetu, wahenga walikuwa wanatumia maneno yabusara kutolea vijana ujumbe wa kuwajenga kitabia na kuwapa motisha yakufanya kazi. Moja wapo ya maneno waliyotumia ni methali. Kila jamii inamethali ambazo inatumia kutolea wanajamii hasa vijana, mafunzo. Je, unajuamethali maana ya methali? Kuna methali ambazo unajua katika lugha yako ya
mama? Umewahi’ kutumia methali katika mazungumzo yako? Ikiwa umewahi kuzitumia, una uwezo wa kukamilisha methali ukipewa sehemu moja ya methali hiyo? Je, unajua kuwa methali hutumika kulingana na ujumbe au mazingira? Ikiwa unatambua hilo, unaweza kutambua baadhi ya methali zinazohusiana na
majanga? Mada ndogo hii itakuwezesha kutambua methali zinazohusiana na majanga na jinsi ya kuzitumia katika mawasiliano yako ya kila siku.
Shughuli 2.11
Kueleza maana ya methali
I. Katika vikundi, elezeni maana za methali mlizokamilisha hapo juu.
Taz: Umejifunza jinsi ya kukamilisha methali na kueleza maana zake. Vilevile, unastahili kutambua kuwa methali ni pambo la lugha. Mbali na kutoa ujumbe, hutumika kupamba lugha na kuifanya ya kuvutia katika mawasiliano.
Stadi za lugha: kuandika
Funzo i: Kuandika insha ya ripoti juu ya majanga na madhara yake
Utangulizi
Ripoti ni maelezo juu ya jambo fulani lililotokea. Sijui kama umewahi kusoma ripotiyoyote. Je, unaweza kutambua muundo wa kuandika ripoti? Mwisho, unaweza kuandika ripoti? Mada ndogo hii itakuwezesha kuandika ripoti kwa usahihi.
1hughuli 2.12
Kuandika ripoti kuhusu janga lolote lililotokea nchini mwako
1.Katika vikundi, jadiliana kuhusu muundo wa ripoti na kuwasilisha matokeo yenu mbele ya wanafunzi.
2.Kila kikundi kiandike insha ya ripoti kuhusu janga lililotokea nchini.
Wasilisheni ripoti yenu mbele ya wanafunzi.
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza juu ya:
Msamiati muhimu wa majanga
Sehemu mbalimbali zilizowahi kukumbwa na majanga
Sababu zinazochangia majanga kutokea
Njia mbalimbali za kuepukana na majanga
Kusoma makala yanayohusu maporomoko ya ardhi
Kujibu maswali yanayotokana na makala kuhusu majanga
Matumizi ya sentensi katika hali ya mazoea na ukanushaji wake
Viwakilishi vya sifa katika sentensi
Methali zinazohusiana na majanga.
Insha ya ripoti juu ya majanga na madhara yake.
Assignment
ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli Jumlishi JUU Majanga MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days