kuandika insha: sherehe katika familia

Funzo j: Insha
Stadi: Kuandika
Shughuli 3.10: Kuandika insha
Katika makundi,
Kwa kurejelea masimulizi yenu katika shughuli 3.9, ongozana katika kuandika insha kuhusu sherehe mlizowahi kuhudhuria nyumbani kwenu au katika jamii zenu.

(i)Ilikuwa ni sherehe gani?
(ii)Ilitokea lini? Matayarisho yalianzaje?
(iii)Watu wengine waliohudhuria ni kina nani?
(iv)Zungumzia chakula na vinywaji.
(v)Ni shughuli gani nyingine zilizotendeka?
(vi)Ni kitu gani ambacho kilikupendeza sana au kukukasirisha?
(vii)Sherehe iliishaje?
Unaweza kuongeza mambo yako mengine yanayohusiana
na sherehe hiyo.

Mfano wa Shughuli jumlishi:
Katika jamii yenu, kunatokea sherehe mbalimbali. Baadhi ya sherehe hizi huwa ni za furaha, na nyingine huwa ni za huzuni. Katika sherehe hizi zote, wanajamii hujumuika pamoja kufurahia au kuhuzunika na wanajamii wenzao. Andika insha ukielezea sherehe mbalimbali ambazo zimewahi kutokea katika jamii yenu pamoja na maana au umuhimu wa sherehe hizo.

Muhtasari wa mafunzo ya mada
Katika mada hii, umejifunza,

Kutambua sherehe mbalimbali katika jamii.
Kueleza umuhimu wa sherehe katika jamii.
Kuigiza jinsi ndoa hutendeka katika utamaduni wako.
Kujadili madhara ya kushiriki mapenzi kabla ya ndoa.
Kusoma na kujibu maswali kutokana na insha.
Kutunga sentensi kwa kutumia upatanisho wa kisarufi wa ngeli
ya PA-KU-MI-J.
Kueleza mnyambuliko wa vitenzi katika kauli ya kutendeka,
kutendesha na kutendua.
Kubainisha vitate mbalimbali na kuvitumia katika sentensi.
Kusimulia hadithi ya sherehe ya familia.
Kuandika insha juu ya sherehe uliyowahi kuhudhuria.

tumugonze Timothy

Leave a Comment
Share
Published by
tumugonze Timothy

Recent Posts

QUESTION 4

4(a) what are your roles as citizen of Uganda?   (b) Each and every  individual in…

1 year ago

QUESTION 3

3(a) why do we political Eduction in the New Uganda curriculum?    (b) Explain the roles…

1 year ago

QUESTION 2

2(a) Describe the creation story in relation to the origin of man.    (b) Explain why…

1 year ago