Kuandika Insha
Stadi: Kuandika
Shughuli 5.12: Kuandika insha fupi kuhusu umuhimu wa hesabu.
Katika makundi,
Shirikiana katika kuandika insha ya maelezo kuhusu umuhimu
wa kujua kuhesabu.
Mfano wa Shughuli jumlishi:
Ujuzi wa kutambua, kutamka na kusoma tarakimu mbalimbali ni muhimu sana katika maisha ya binadamu.Ukipewa pesa kiasi cha milioni moja, andika insha yenye maelezo ya bajeti kuhusu vile utazitumia zote kwa kununua vitu angalau ishirini ambavyo unahisi ni muhimu katika maisha yako.
Muhtasari wa mafunzo ya mada
Katika mada hii, umejifunza,
Kuhesabu tarakimu.
Kutambua tarakimu katika vitu mbalimbali.
Kutumia alama za hesabu mbalimbali kupata matokeo mapya
ya tarakimu.
Kueleza tarehe.
Kubainisha akisami mbalimbali na kuzitumia katika sentensi.
Kutambua maumbo mbalimbali na kuyalinganisha na vitu vya
kawaida.
Kukariri shairi.
Kutunga sentensi katika ngeli ya Li-Ya.
Kutambua vivumishi vya idadi na vya sifa na kuvitumia katika
sentensi.
Kufumba na kufumbua mafumbo.
Kuandika insha.
4(a) what are your roles as citizen of Uganda? (b) Each and every individual in…
3(a) why do we political Eduction in the New Uganda curriculum? (b) Explain the roles…
2(a) Describe the creation story in relation to the origin of man. (b) Explain why…
Leave a Comment