• No products in the cart.

20

Hiki ni kitabu cha Mwanafunzi wa kidato Cha tatu kwa shule za upili nchini Uganda. Kitabu hiki kinaendeleza udhibiti wa …

FREE

Hiki ni kitabu cha Mwanafunzi wa kidato Cha tatu kwa shule za upili nchini Uganda. Kitabu hiki kinaendeleza udhibiti wa umilisi na mawasiliano kwa matumizi ya Kiswahili sanifu.
Kitabu hiki kinakuza na kuendeleza ujifunzaji na upataji wa umilisi kutoka kidato Cha kwanza na pili. Kinazidi kuweka msingi madhubiti wa kuimarisha umilisi unaomwezesha mwanafunzi kutumia Kiswahili fasaha kutokana na upanuzi wa misamiati na tajiriba za kumwezesha mwanafunzi kuwasiliana
katika miktadha mbalimbali kwa mahitaji yake ya kila siku. Kitabu hiki cha mwanafunzi kwa kidato cha tatu ni nguzo imara katika ujifunzaji wa Kiswahili sanifu. Mada za kitabu hiki zimeandaliwa kuakisi na kutosheleza mahitaji na malengo ya mtaala kwa Shule za upili nchini Uganda-Mahitaji ya mwanafunzi katika harakati na mchakato wa ujifunzaji umetiliwa maanani. Mwanafunzi amepewa uhuru wa kufikiri, kuhakiki, na kutatua matatizoya masuala ibuka ya kiuzalendo, kimazingira na kimaisha yanayomkumba
shuleni, nyumbani na katika jamii yake.Kitabu hiki ni ngao ya kujifunzia Kiswahili kwa vile kinavyoakisi na kutoshelezamalengo ya mtaala kwa Shule za upili nchini Uganda. Mahitaji ya mwanafunzikatika harakati zake za kujifunza Kiswahili yanatiliwa maanani. Mwanafunzimwenyewe atapata uwezo wa kufikiri, kuhakiki na kutatua matatizo yanayomkumba shuleni, nyumbani na katika jamii yake. Vilevile, kitabu hiki kitamsaidia mwanafunzi kupata uwezo wa ubunifu na uvumbuzi anapojifunza Kiswahili darasani. Kadhalika, mwanafunzi atapata umilisi wa mawasiliano kwa Kiswahili. Mwanafunzi atajifunza zaidi teknolojia yakisasa kwa mazoezi ya matumizi ya tarakilishi na ukokotaji. Pamoja na hayo,
mwanafunzi atazidi kujiendeleza kimaadili kwa kushirikiana na kufanya kazi pamoja na wenzake. Kwa hivyo, ni jambo muhimu kila mwanafunzi kushirikiana na wenzake darasani katika jozi au vikundi ili kuendeleza ushirikiano, uvumbuzi, usikilizaji, uongeaji na mawasiliano ili kufanikisha mkakati wa ujifunzaji Kiswahili sanifu.

Course Currilcum