To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Utangulizi
Je! unaishi na kina nani nyumbani? Unaweza kutamka majina yao kwa ufasaha? Kwa mfano, kuna silabi ngapi katika jina la kila mmoja wao? Mawasiliano yatakuwa kamilifu iwapo sauti, silabi na maneno ya lugha yoyote ile hutamkwa kwa namna inayostahili. Pia ni muhimu kuthamini na kushirikiana na watu wa nyumbani kimazungumzo na katika shughuli mbalimbali.
Kwa hivyo, mada hii itakupa uwezo wa kutambua matamshi bora ya sauti za Kiswahili. Mada hii pia itakuwezesha kutambua watu wa nyumbani na jinsi ya kuwasiliana na kuishi nao kwa namna inayostahili.
Funzo a: Kutamka sauti za Kiswahili
Shughuli 1.1 Kusikiliza na Kuzungumza
Katika vikundi,
1. Tamka, kariri, na kusoma kwa sauti maneno yafuatayo kwa kuzingatia matamshi bora ya vokali za Kiswahili.
a– anza, baba, kaka, dada
e– endesha, endelea,
i-inuka, ingia, bibi, mimi, sisi
o– omba, ona, ondoa, oga, wote
u– uhuru, umoja, kuku, nguvu
2. Tamka maneno yafuatayo yenye matumizi ya vokali mbili
aa– kaa, jaa, baada, saa,
ee– mzee, pekee
ii– tii, bidii
oo– choo, njoo
uu– juu, mguu
3. Tamka maneno yafuatayo yenye matumizi ya vokali mbili zisizofanana
ondoa, lia, ongea, fagia, pokea, chuo, kimbia, somea
4. Shirikiana na wenzako kutambua, kutamka na kuandika baadhi ya maneno yenye vokali mbalimbali.
Shughuli 2.1 Kusikiliza na Kuzungumza
Katika vikundi,
1. Tamka sauti zifuatazo.
i. /b/, /p/, /m/ /w/
ii. /f/, /v/
iii. /dh/, /th/
iv. /d/, /l/, /n/, /r/, /s/, /t/, /z/
v. /ch/, /j/, /ny/, /sh/, /y/
vi. /k/, /g/, /ng’/, /gh/, /kh/
vii. /h/.
2. Tamka tena sauti zilizo juu. Tambua mahali sauti hizo zinakotamkiwa.
3. Unganisha konsonanti na vokali ulizotamka hapo juu kuunda silabi na maneno.
fa, fe, fi, fo, fu
ba, be, bi, bo, bu
cha,che,chi,cho,chu
dha, dhe,dhi,dho,dhu
4. Shirikiana na wenzako katika kikundi kuandika alfabeti ya Kiswahili kutoka A hadi Z.
Funzo b. Kutambua msamiati wa watu wa nyumbani
Shughuli 3.1 Kusikiliza na kuzungumza.
Katika vikundi,
WATU WA NYUMBANI.
Majina ya ukoo;
Neno ukoo linafasiliwa kama kundi la watu wa nasaba moja. Nasaba ni uhusiano wa watuwenye uzao mmoja.
majina ya wa watu wenye uhusiano unaotokana na ukoo mmoja ni kama yafuatayo;
Baba: Ni mzazi wa kiume au mume wa mamako.
Mama: Ni mzazi wa kike.
Kaka: Ni mtoto wa kiume mliyezaliwa naye.
Dada: Ni ndugu wa kike wa kuzaliwa na nawe.
Bin : Ni mtoto wa kiume wa mtu fulani.
Binti: Ni mzaliwa wa kike wa wazazi.
Babu: Ni mzazi wa kiume wa baba au mama.
Bibi/nyanya: Ni mama aliyemzaa baba au mama.
shangazi: Ni ndugu wa kike wa baba .
Ami/baba mdogo: Ni mwamume aliyezaliwa katika tumbo moja na baba.
mjomba: Mwanaume aliye ndugu wa mama au kaka wa mama.
mama mdogo: Ni mwanamke aliyezaliwa katikatumbo moja na mama.
binamu: Ni mtoto wa shangazi ami au mjomba.
Ndugu: Ni mtu wa kike au kiume aliyezaliwa naye kutoka kwa baba,kwa mama au wazazi wote wawili.
wifi: Jina la heshima la kifamilia waitanaklo mke na ndugu wa kike wa mume.
shemeji : Ni ndugu au rafiki wa mke au mume.
mkwe: Ni baba au mama wa mume au mke wako .aidha ni mume au mke wa mwana wako au binti yako.
mama mkwe: Ni mama wa mkeo au mumeo.
baba mkwe/bamkwe: Ni mzazi wa kiume wa mke au mume wa mtu fulani.
2. Jadiliana na wenzako kutafuta maana ya maneno uliyopewa katika boksi
3. Elezea kuhusu watu wa familia yako kwa kutaja majina yao.
4. Shirikiana na wenzako kusoma na kujadili maana ya sentensi zifuatazo
i. Baba yangu ni dereva wa basi.
ii. Mama yangu ni mwalimu wa Kiswahili.
iii. Dada yake Peter anafundisha katika Chuo Kikuu cha Kyambogo.
iv. Bin yangu anaitwa Haba.
v. Kaka yangu anasomea katika Chuo cha walimu cha Nakaseke.
vi. Binti yake Yusuph ni mrembo sana.
vii. Tafadhali niitie yule kaka yangu.
viii. Eve ni binti yake mzee Lutaaya.
ix. Dada yako anaitwa nani?
x. Mama ananyonyesha mtoto.
Kazi mradi
Katika kikundi, fanya utafiti kuhusu msamiati mwingine wa watu wa ukoo. Unaweza kutumia kamusi, maktaba au mtandao. Kisha, wasilisha matokeo ya utafiti wako darasani.
5. Ambatanisha majina ya watu wa ukoo kutoka sehemu A na B.
A B
Baba ndugu wa kike wa baba.
Mama mzazi wa kiume.
Shangazi ndugu wa kike wa kuzaliwa na kaka.
Kaka mzazi wa kike.
Dada ndugu wa kiume wa kuzaliwa na dada.
Nyanya mzazi wa kike wa baba au mama.
Funzo c: Kuigiza majukumu ya watu wa Nyumbani
Shughuli 4.1 Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Baba anakama ng’ombe. Mama anapika chakula.
Dada anaosha vyombo. Kaka anafyeka nyasi.
3. Shirikiana katika vikundi kuelezea na kuigiza majukumu mbalimbali ya watu wa nyumbani.
Funzo d. Kueleza kazi zinazofanyika nyumbani
Shughuli 5.1 Kusikiliza, kuzungumza na kuandika
Katika vikundi,
1. Jadiliana kuhusu kazi mbalimbali zinazofanyika nyumbani kwenu.
2. Kwa zamu, elezea kazi unazofanya nyumbani kwenu wakati wa likizo.
3. Jaza mapengo kwa kutumia vitenzi vifuatavyo vinavyohusu kazi za nyumbani.
(paka, ezeka, jenga, safisha, fyeka)
(a) Dada yangu ana ………………… vyombo.
(b) Ami ali ………………… nyasi katika boma lake.
(c) Baba yetu anafanya kazi ya ku ………… rangi.
(d) Nili ………… mabati juu ya nyumba yetu.
(e) Babu yetu ali …………. nyumba kubwa sana kijijini.
Funzo e. Kusimulia hadithi fupi kuhusu familia
Shughuli 6.1 Kusikiliza, kuzungumza na Kuandika
Chora watu unaoishi nao nyumbani kwenye karatasi, kisha usimulie hadithi inayohusu watu wa familia yako.
Funzo f. Kutambua matumizi ya Salamu na maneno ya adabu
Shughuli 7.1 Kusikiliza na kuzungumza.
Taz: Salamu ni maamkizi ya kujuliana hali miongoni mwa watu. Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nyingi za salamu kulingana na umri/cheo, wakati, hali, idadi ya watu unaosalimia na uhusiano wa watu husika.
Salamu kulingana umri/cheo: Shikamoo ni salamu ya heshima kwa mtu anayekuzidi umri au cheo.
watoto wanamsalamia mke.
salamu kulingana na wakati.
salamu jibu
sabalkheri sabalkheri/alkheri
masalkheri masalkheri/alkheri
TANBIHI:Sabalkheri ni salamu inayotumiwa wakati wa asubuhi ilihali masalkheri inatumiwa wakati wa jioni kuanzia alasiri
Salamu kulingana na hali mbalimbali
Salamu Hali Jibu
habari ya /za masomo/shuleni? nzuri/njema.
habari ya/za nyumbani? nzuri/njema
habari ya/za safari? nzuri/njema
habari ya/za kupotea? nzuri/njema
habari ya/za kazi? nzuri/njema
iii. Salamu za kujuliana hali kulingana na idadi ya wanaoitikia.
Shughuli 8.1 Kusikiliza na kuzungumza
Kakika vikundi,
1. Igizeni salamu na majibu yake kama ifuatavyo;
Salamu Jibu
hujambo? Sijambo.
hamjambo? Hatujambo.
umeamkaje/umelalaje? Salama.
mmeamkaje/mmelalaje? Salama.
umeshindaje?/mmeshindaje? Vizuri/vyema.
u mzima? m wamzima? Ni mzima/ tu wazima.
u hali gani?/mhali gani? Njema/nzuri.
Funzo g. Kutambua na kuigiza maneno ya adabu
Shughuli 9.1 Kusikiliza, kuzungumza na kusoma
Katika vikundi,
Funzo h. Kusoma na kuigiza mazungumzo
Shughuli 10.1 Kusoma na kuandika
1. Katika jozi, someni na kuigiza mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali
Tom : Habari ya siku nyingi rafiki?
Rehema : Ni nzuri, labda zako?
Tom : Mimi ni mzima. Umepotea sana siku hizi!
Rehema : Ndiyo, mama yangu amekuwa mgonjwa.
Tom : Eee! Pole sana, sasa yuko vipi?
Rehema : Tumempa dawa, atapata nafuu.
Tom : Hebu tuombe Mungu apone haraka
Rehema : Amina. Hebu niende nyumbani, Alamsiki!
i. Kwa kutumia kamusi, tafuteni maana ya maneno mapya kutokana na mazungumzo.
ii. Tambua na kuandika salamu na maneno ya adabu yaliyotumika katika mazungumzo.
Sarufi
Funzo i. Kutumia vipatanishi sahihi vya nomino za ngeli ya A-WA katika sentensi
Shughuli 11.1 Kusoma na kuandika
Katika vikundi,
1. Tazameni na kujadiliana kuhusu kinachotendeka katika michoro.
Ngeli ya A-WA inajumuisha viumbe wote wenyeuhai na damu kama vile watu,wanyama,wadudu, ndege nakadhalika.
Shirikiana kusoma kwa sauti na kutafuta maana ya nomino zifuatazo;
Umoja Wingi
mtu watu
mtoto watoto
mhubiri wahubiri
mke wake
mume waume
mkulima wakulima
mzazi wazazi
mwalimu walimu
mfalme wafalme
mwanafunzi wanafunzi
mlevi walevi
mlinzi walinzi
mwislamu waisilamu
msichana wasichana
mvulana wavulana
UPATANISHO WA KISARUFI
A(UMOJA)
majina vionyeshi kuwa vivumishi
mtu huyu ni mrefu
mgeni yule si mfupi
mdudu mbaya
mnyama mdogo
1, mtu huyu ni mrefu.
2,mtoto yule si mbaya.
3, mdudu yule ni mbaya.
B ,(WINGI)
majina vionyeshi kuwa vivumishi
watu hawa ni warefu
wageni wale si wafupi
wadudu wabaya
wanyama wadogo
1,watu hawa ni warefu.
2,watoto wale si wabaya.
3,wadudu wale ni wabaya.
majina (umoja) vimilikishi
mzazi wangu(my /mine)
mpishi wako(your/s)
mgeni wake(his /her)
mgonjwa wetu(our/s)
wenu(their)
wao(your /p)
1,Mzazi wangu ni mzuri. Wazazi wangu ni wazuri.
2,Mtoto wangu ni mbaya. Watoto wangu ni wabaya.
3,Mpishi wako ni msafi. Wapishi wako ni wasafi.
4,Baba yangu ni mrefu. Baba zangu ni warefu.
5,Binti yake ni mkubwa. Binti zake ni wakubwa.
majina kiwakilishi(a-) kiwakilishi(wa-)
msichana anasoma wanasoma
mwalimu analala wanalala
mnyama anakula wanakula
mganga anakimbia wanakimbia
1, Msichana anasoma. Wasichana wanasoma.
2,Mwalimu analala. Walimu wanalala.
3,Mnyama anakula. Wanyama wanakula.
Shirikiana na wenzako kuandika sentensi zifuatazo katika wingi.
i. Mama analima shambani.
ii. Kaka na dada wanaosha vyombo.
iii. Mfalme amekaa.
iv. Mganga anatibu mgonjwa.
v. Mvulana anapasua kuni.
vi. Mzee anapeana mawaidha.
vii. Mwanafunzi alienda shuleni asubuhi.
Funzo j. Kuakifisha kwa usahihi
Shughuli 12. 1 Kusoma na kuandika
Katika vikundi,
1. Someni na kujadili ujumbe katika kifungu.
Nalubega na Onyango ni marafiki sana. Siku moja, Nilimsikia Onyango akisema, “Mimi na rafiki yangu Nalubega tumetembelea mataifa mengi ulimwenguni.” Kwa mfano, Mataifa ya Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania, Sudani Kusini, Rwanda na Burundi), Ujerumani, Uhispania, Brazil, Marekani na Uchina. “Umetembelea nchi gani wewe?” Aliniuliza. “Mimi sijawahi hata kuvuka mpaka wa Uganda!” Nilimjibu. Alaa! Alishangaa. Bahati yako itakuja usijali. Alinitia moyo.
2. Tambua na kuandika alama za uakifishaji katika kifungu ulichosoma.
3. Fanyeni utafiti kuhusu alama nyingine zozote za uakifishaji ambazo hazijatajwa katika kifungu.
Funzo K. Kuandika Insha
Shughuli 13.1 Kuandika
Katika makundi,
1. Andikeni insha kuhusu watu wa ukoo wako.
Zingatieni yafuayo;
Jina lako? Unasoma kidato gani? Unaishi wapi? Unaishi na nani nyumbani? Watu wa nyumbani kwenu wanafanya kazi gani? Wewe, unasaidiaje wazazi wako katika kazi za nyumbani.
Shughuli ya jumla
Umeandaliwa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwako nyumbani kwenu. Umeita baadhi ya
marafiki zako kutoka darasani mwako kuhudhuria. Baada ya chakula na kukata keki,
umeombwa kutambulisha kila mtu aliyehudhuria. Umemaliza kuwatambulisha marafiki
zako.
a. Watambulishe watu wa ukoo wako waliohudhuria.
b. Kila mtu wa nyumbani alisema kuwa marafiki zako ni watoto wenye adabu. Ni mambo gani waliyofanya ili kuonyesha kuwa ni wenye adabu.
c. Andika maneno uliyozungumza wakati wa hotuba yako.
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu,
• Sauti za Kiswahili kwa usahihi
• Msamiati wa watu wa nyumbani.
• Usimulizi w hadithi fupi kuhusu familia yako.
• Salamu kwa namna inayostahili.
• Maneno ya adabu
• Uigizaji wa mazungumzo.
• Matumizi ya aina mbalimbali ya majina ya watu wa nyumbani katika sentensi.
• Vipatanishi vya nomino vya ngeli ya A–WA katika sentensi.
• Uakifishaji.
• Uandishi wa insha