• LOGIN
  • No products in the cart.

LSC: MADA KUU 1.3 HESABU

Number chart - Definitions, Types, Charts

Utangulizi

Hesabu ni nzuri sana, ujuzi wa hesabu ni muhimu sana kwa sababu hutumika katika nyanja mbalimbali. Kwa mfano, pesa ambazo hutumika kila siku hutumia tarakimu mbalimbali. Watu mbalimbali pia wanafaa kujua hesabu ili waweze kuhesabu mali yao.

Funzo a: Kuhesabu tarakimu

Shughuli 1.3: Kusikiliza na kuzungumza

Katika makundi,

1. Shirikiana kusoma na kuhesabu tarakimu zifuatazo.

0 Sufuri
1 Moja
2 Mbili
3 Tatu
4 Nne
5 Tano
6 Sita
7 Saba
8 Nane
9 Tisa
Taz; Kati ya nambari hizi kuna nambari shufwa na nambari wit

Taz; Kati ya nambari hizi kuna nambari shufwa na nambari witiri.

Nambari shufwa ni nambari ambazo huweza kugawiwa mbili bila kuacha baki kama vile; 2,4,6,8.

Nambari witiri ni nambari ambazo haziwezi kugawiwa mbili kama vile 1 au baada ya kuzigawa na mbili zinaacha baki la 1 kama vile; 3,5,7,9.

Nambari shufwa ni; 2,4,6,8 na kadhalika.

Nambari witiri ni; 1,3,5,7,9 na kadhalika.

Halafu kuna nambari hasi (-) mfano -1(hasi moja) na nambari chanya (+) mfano +2 (chanya mbili).

shirikiana na wenzako kusoma tarakimu zifuatazo

10 Kumi
11 Kumi na moja
12 Kumi na mbili
13 Kumi na tatu
14 Kumi na nne
15 Kum na tano
16 Kumi na sita
17 Kumi na saba
18 Kumi na nane
19 Kumi na tisa
Shirikiana kujaza mapengo baadhi ya
nambari zilizo kati ya 20-29
20 Ishirini
21 Ishirini na moja
22
23
24
25
26
27
28
29 Ishirini na tisa
Jaza mapengo kwa kuandika tarakimu
kwa maneno
30 Thelathini
31 Thelathini na moja
32
33
34
35
36
37
38
39 Thelathini na tisa
Nambari 40-49
40 Arubaini
41 Arubaini na moja
42 Arubaini na mbili
43 Arubaini na tatu
44 Arubaini na nne
45 Arubaini na tano
46 Arubaini na sita
47 Arubaini na saba
48 Arubaini na nane
49 Arubaini na tisa
Funzo b: Kulinganisha tarakimu na
maneno
Shughili 2. 3 Kusoma na kuandika
Jaza mapengo kwa kuandika tarakimu
kwa maneno
50 Hamsini
51 Hamsini na moja
52 hamsini na mbili
53 Hamsini na tatu
54 Hamsini na nne
55 Hamsini na tano
56 Hamsini na sita
57 Hamsini na saba

58 Hamsini na nane
59 Hamsini na tisa

Nambari 60-69
60 Sitini
61 Sitini na moja
62 Sitini na mbili
63 Sitini na tatu
64 Sitini na nne
65 Sitini na tano
66 Sitini na sita
67 Sitini na saba
68 Sitini na nane
69 Sitini na tisa

70 Sabini
71
72
73
74
75
76 Sabini na sita
77 Sabini na saba
78 Sabini na nane
79 Sabini na tisa
Shirikiana kujaza mapengo baadhi ya
nambari zilizo kati ya 80-89
80 Themanini
81
82
83
84
85
86
87
88
89 Themanini na tisa
Shirikiana kujaza mapengo baadhi ya
nambari zilizo kati ya 90-99
90 Tisini
91 Tisini na moja
92
93
94
95
96
97
98
99 Tisini na tisa
Nambari 100-900
100 Mia moja
200 Mia mbili
300 Mia tatu
400 Mia nne
500 Mia tano
600 Mia sita
700 Mia saba
800 Mia nane

Funzo c: Kutofautisha alama za hesabu

Shughuli 3.3 Kusikiliza na kuzungumza

Katika makundi,

1. Tambua alama za hesabu zifuatazo

• Alama ya kuondoa       –
• Alama ya kujumlisha   +
• Alama ya kuzidisha     ×
• Alama ya kugawanya  ÷
• Alama ya mlinganyo   =

2. Tumia alama hizo kupata matokeo mbalimbali

Funzo d: Kutambua siku za wiki

Shughuli 4.3 Kuoma

1. Someni na kujadiliana kuhusu siku za wiki zifuatazo

Leo –      siku hiyo iliopo.
Jana –    Siku kabla ya leo.
Juzi-      Siku kabla ya jana.
Kesho – Siku baada ya leo.
Kesho kutwa – Siku baada ya kesho.
Mtondo      –       Siku baada ya kesho kutwa
Mtondogoo – Siku baada ya mtondo
Siku ya Sabato  kwa Wakristo ni Jumamosi au Jumapili.
Waislamu huenda msikitini siku ya Ijumaa.

2. Katika makundi, shirikiana kujibu maswali yafuatayo;

(a) Leo ni siku gani? jumamosi
(b) Jana ilikuwa siku gani? ijumaa
(c) Kesho itakuwa siku gani? jumapili

(d) Juzi ilikuwa siku gani? alhamisi
(e) Kesho kutwa itakuwa siku gani? jumatatu

Funzo e: Kueleza shughuli za siku

Shughuli: 5.3 Kusikiliza na kuzungumza

Katika vikundi,

i. Jadiliana kuhusu shughuli mbalimbali unazofanya nyumbani kabla ya kuja shuleni na baada ya kurudi nyumbani.  ii. Jadiliana kuhusu shughuli mbalimbali unazofanya nyumbani hasa wakati wa wikiendi.
iii. Wasilishieni matokeo ya majadiliano yenu mbele ya darasa

Funzo f: Kutamka miezi ya mwaka

Shughuli 6.3 Kusoma na kuandika

1. Shirikiana na wenzako kusoma na kujadili miezi ya mwaka
i. Mwezi wa kwanza wa mwaka ni Januari.
ii. Mwezi wa pili wa mwaka ni Februari.
iii. Mwezi wa tatu wa mwaka ni Machi.
iv. Mwezi wa nne wa mwaka ni Aprili.
v. Mwezi wa tano wa mwaka ni Mei.
vi. Mwezi wa sita wa mwaka ni Juni.
vii. Mwezi wa saba wa mwaka ni Julai.
viii. Mwezi wa nane wa mwaka ni Agosti.
ix. Mwezi wa tisa wa mwaka ni Septemba.
x. Mwezi wa kumi wa mwaka ni Oktoba.
xi. Mwezi wa kumi na moja wa mwaka ni Novemba.
xii. Mwezi wa kumi na mbili wa mwaka ni Desemba.

Msamiati unaohusiana na miezi ya mwaka

• Mwezi huu
• Mwezi ujao/ mwezi kesho- Baada ya mwezi huu
• Mwezi uliopita/ mwezi jana- Kabla ya mwezi huu
• Mwanzoni mwa mwezi
• Katikati mwa mwezi
• Mwishoni mwa mwezi

3. Katika makundi, shirikiana kujibu maswali yafuatayo;

(a) Mwezi huu ni mwezi wa……………………………………
(b) Mwezi wa kwanza una siku………………………………..
(c) Mwezi wa mwisho wa mwaka ni…………………………..
(d) Mwezi wa Oktoba una siku ……………………………….
(e) Mwezi ujao utakuwa mwezi wa…………………………….

Funzo g. Kueleza Saa

Shughuli 7.3 Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Soma na kujadiliana kuhusu msamiati unaohusiana na saa ufuatao

Saa ni chombo ambacho huonyesha wakati.

Siku nzima ina saa ishirini na nne.

Msamiati unaotumiwa kwenye saa

Dakika        – Saa moja ina dakika sitini.

Sekunde    – Dakika moja ina sekunde sitini.

Nusu         – Dakika thelathini.

Robo        – Dakika kumi na tano.

Kasorobo – Dakika kumi tano kuingia saa nyingine.

Kamili – Hakuna dakika ambayo imepita kwenye saa.

Alfajiri – kati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi.

Adhuhuri – Saa sita.

Mchana – Ni kipindi kinachoanzia kuchomoza kwa jua hadi kutua kwake/ Kipindi kilicho kati ya Saa sita hadi saa tisa.

Jioni – Ni wakati baina ya alasiri na magharibi.

Usiku – Saa moja hadi saa tano.

Usiku wa manane – Saa saba hadi saa tisa usiku.

2. Katika makundi, shirikiana na wenzako kutambua na kutaja saa mbalimbali zifuatazo;

Sasa ni saa ngapi?

3. Someni, chora na kutaja saa zifuatazo

(a) Saa kumi na mbili kamili asubuhi.

(b) Saa kumi na moja na robo jioni.

(c) Saa nne na nusu usiku.

(d) Saa mbili na dakika ishirini asubuhi.

(e) Saa nane kasoro dakika kumi mchana.

Funzo h: Kusoma kalenda

Shughuli 8.3: Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Someni, tamka na kuandika tarehe zifuatazo kwa maneno

Jumamosi 10/3/1992 – Jumamosi tarehe kumi mwezi wa Machi mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na mbili.

Alhamisi 6/10/2000 – Alhamisi tarehe sita mwezi wa Oktoba mwaka elfu mbili.

Jumanne 25/4/2017 – Jumanne tarehe ishirini na tano mwezi wa Aprili mwaka wa elfu mbili kumi na saba.

2. Someni, tamka na kuandika tarehe zifuatazo katika tarakimu

i. Ijumaa tarehe thelathini mwezi wa Julai mwaka wa elfu moja mia nane themanini na nane.
ii. Jumatatu tarehe tatu mwezi wa Januari mwaka wa elfu mbili kumi na nane.
iii. Jumapili tarehe ishirini na nne mwezi wa Novemba mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na tisa.
iv. Jumatano tarehe kumi na saba mwaka wa Desemba mwaka wa elfu mbili na moja.
v. Alhamisi tarehe tisa mwezi w a Mei mwaka wa elfu moja mia sita sabini na nne.

3. Katika kikundi, Someni na kujadiliana kuhusu taarifa katika makala hii.

SIKU ZA WIKI

Wiki/Juma ni muda wa siku saba. Katika lugha ya Kiswahili, wiki ina siku saba kwa ujumla. Siku ya kwanza katika kalenda ya Kiswahili ni Jumamosi. Jumamosi ni siku ambayo Wakristo wa dhehebu la Kiadventi huenda kanisani kuomba Mungu.

Siku ya pili katika lugha ya Kiswahili huitwa Jumapili. Hii ni siku ambayo Wakristo wengine kama vile Wakatoliki na Waprotestanti huenda kanisani kwa ajili ya kumwomba Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa mema ambayo amewajalia.

Siku ya tatu huitwa Jumatatu. Hii ni siku ya kufanya kazi. Wafanyakazi wote huenda kazini na wanafunzi huenda shuleni kusoma.

Siku ya nne katika lugha ya Kiswahili inaitwa Jumanne. Siku hii pia ni ya kufanya kazi. Vile vile, wanafunzi huenda shuleni kuhudhuria vipindi.

Siku ya tano katika lugha ya Kiswahili ni Jumatano. Hii ni siku ya kufanya kazi pia.

Siku ya Alhamisi ni siku ya sita katika wiki. Katika siku hii pia watu huenda kufanya kazi.

Siku ya Ijumaa ni siku ya saba ambayo ni ya mwisho katika wiki. Siku hii Waislamu huenda msikitini kuswali/ kufanya ibada ya swala ambayo ni ya lazima kwa kila mwislamu.

4. Katika kikundi, Someni na kujadiliana kuhusu taarifa katika makala hii.
i. Wiki ina siku ngapi?

    wiki ina siku saba
ii. Taja siku ya kwanza ya wiki katika lugha ya Kiswahili.

jumamosi ni siku ya kwanza katika lugha ya kiswahili.

iii. Waadventi huenda kanisani siku gani?

waadventi huenda kainsani siku ya jumamosi.

iv. Je, Wakristo huenda kanisani kufanya nini? Taja hoja mbili.

Sarufi

Funzo i; Kutambua vivumishi vya idadi na sifa

Shughuli 9.3 Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Someni na kujadiliana kuhusu matumizi ya vivumishi vya Idadi

Hutueleza zaidi kuhusu kiasi, au idadi ya nomino. Kuna aina mbili za vivumishi vya idadi.

a) Idadi Kamili

Hii hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino. Kwa mfano: tatu, mbili, kumi.

msichana ameuua nyoka wawili.

Nyoka mmoja.                                                Nyoka wawili

       

• Siku kumi zimepita tangu Bi Safina alipojifungua watoto watatu.

mtoto mmoja.                                           watoto wawili.

     

b) Idadi Isiyodhihirika

Kivumishi hiki cha idadi huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili. Kwa mfano: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.

• Watu wachache waliohudhuria mazishi ya Kajuta walikula chakula kingi sana.

• Baba yao alikuwa mateka kwa miaka kadhaa.

2. Someni na kujadiliana kuhusu matumizi ya vivumishi vya sifa

Hivi ni vivumishi ambavyo hutoa sifa ya kitu, mtu, mahali, na kadahalika kwa mfano: kizuri, kali, safi, mrembo. Ni neno/maneno ambayo hutaja maana ya sifa ya nomino au kiwakilishi cha nomino jinsi kilivyo.

Mifano:

• Paka mwizi amelala jikoni
• Ugonjwa hatari umeukumba dunia
• Gari zuri limegongwa
• Nyumba kubwa imejengwa bondeni
• Kijana mpole kasusa kula

3. Someni na kujadiliana kuhusu matumizi ya viulizi vifuatavyo;

Viulizi ni maneno yanayotumika katika kuulizia kwa mfano: je, gani, lipi, nani, nini, wapi nk

Mifano katika sentensi;

1. Je?
i) Je, ulimwona mwalimu wa Kiswahili?
ii) Mlifanyaje mtihani?

2. Nani?
i) Nani anafundisha Kiswahili?
ii) Nani ananiita?
iii) Unaitwa nani?

3. Nini?
i) Umenunua nini?
ii) Tutakula nini?
iii) Unataka nini?

4. Lini?
i) Utarudi lini?
ii) Mwalimu atafika lini?
iii) Mtanitembelea lini?

5. Gani?
i) Huyu ni mtu gani?
ii) Unakula chakula gani?
iii) Nikupe kitu gani?

6. Namna gani?
i) Tutapita namna gani?
ii) Unakula namna gani?
iii) Umeketi namna gani?

7. Kwa nini?
i) Kwa nini ulitoroka?
ii) Kwa nini mnapiga kelele?
ii) Kwa nini ulikataa kunisaidia?

8. Tangu lini?
i) Tangu lini umekuwa hapa?
ii) Wamelala tangu lini?
iii) Amekuwa mgonjwa tangu lini?

9. Mara ngapi?
i) Unakula mara ngapi?
ii) Mwanafunzi yule alitoroka mara
ngapi?
iii) Mariam amelia mara ngapi?

10. -ngapi?
i) Mmesoma vitabu vingapi?
ii) Unacheza michezo mingapi?
iii) Mna walimu wangapi shuleni?

11. -pi?
i) Unataka mwalimu yupi?
ii) Ameandika vitabu vipi?
iii) Wamenunua gari lipi?

4. Shirikiana na wenzako kutunga angalau sentensi tatu kwa kila kiulizi ulichosoma hapo juu.

Funzo j: Kutunnga sentensi kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.

Shughuli 10.3 Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Shirikiana kusoma na kujadiliana kuhusu matumizi ya vipatanishi vya kisarufi vya li-ya.

Ngeli hii hujumuisha nomino za baadhi ya vitu visivyo hai pamoja na nomino za ukubwa za ngeli mbalimbali. Kuna baadhi ya nomino za ngeli hii ambazo huanza kwa kiambishi Ji katika umoja na nyingine nyingi hazina kiambishi hiki. Hata hivyo, wingi wa nomino zote katika ngeli hii, huchukua kiambishi awali Ma au Me katika wingi.

mifano;

UMOJA                                       WINGI

Somo                                         masomo

jina                                             majina

kosa

jibu                                             majibu

ua                                               maua

godoro

gunia

wazo

soko

jani

zoezi

tofali

bati

sanduku

bega

swali

jino                                            meno

jua                                            majua

kofi                                           makofi

neno                                        maneno

2. Shirikiana na wanafunzi wenzako kutafuta majina mengine ya li-ya kutokana na kamusi

3. Soma na kujadili sentensi zifuatazo kutokana na majedwali kisha uunganishe vipengele mbalimbali hivyo kutunga sentensi zenye maana.

UMOJA

majina                  vionyeshi           kuwa            vivumishi

kosa                     hili                     ni                   baya

godoro                 lile                    si                   dogo

jibu                                                                      zuri

WINGI

majina                 vionyeshi            kuwa           vivumishi

makosa                haya                   ni                   mabaya

magodoro          yale                     si                    madogo

majibu                                                                  mazuri

UMOJA                                               WINGI

majina               vimilikishi              majina        vimilikishi

Kosa                  langu                    makosa          yangu

godoro             lako                       magodoro      yako

jibu                   lake

gunia                letu

jani                   lenu

yai                    lao

4. Tunga sentensi angalau kumi kutokana na kila jedwali mlilosoma hapo juu.

Funzo k: Kuandika Insha

Shughuli 11.3 Kuandika

Katika makundi, shirikiana kuandika insha ya mwongozo kuhusu ratiba yako ya kila siku kuanzia wakati unapoamka asubuhi hadi wakati unapoelekea kulala usiku.

Shughuli ya jumla
Siku ya likizo kuisha ni kesho. Leo umeomba pesa kwa mzazi wako ili uende sokoni kununua
baadhi ya vitu utakavyotaka kutumia shuleni.

d) Elezea na kisha undike kwa ukionyesha siku yenyewe pamoja na tarehe utakaporudi shuleni. Ungependa utoke nyumbani saa ngapi na mwendo unaweza kukuchukua saa ngapi kufika shuleni?
e) Tunga angalau sentensi tano kwa kila kipengele ukitumia vivumishi vya idadi, sifa na viulizi ili kubainisha tofauti ya kila kipengele.

Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu,

a. Kuhesabu tarakimu kutoka 1-1000.
b. Kulinganisha tarakimu na vitu vilivyoandikwa nambari au tarakimu hizo.
c. Kutofautisha alama za hesabu mbalimbali.
d. Kutambua siku za wiki kupitia mfumo wa kiarabu.
e. Kueleza saa kwa kutumia mfumo wa kiswahili.
f. Kusoma makala yanayohusu hesabu na kujibu maswali.
g. Kutambua vivumishi vya idadi, sifa, na viulizi na kuvitumia katika sentensi.
h. Kutambua upatanishi wa kisarufi wa ngeli ya li–ya katika sentensi.
i. Kuandika insha ya mwongozo ya ratiba yake ya kila siku

 

Courses

Featured Downloads