To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
LSC: MADA KUU 1.5 MIMEA NA MATUNDA
Utangulizi
Mungu aliumba wanyama mbalimbali. Kuna wanyama wanaoishi msituni na wengine wanaoishi nyumbani. Wanyama hawa wote wana umuhimu mbalimbali. Wawe wa msituni au wa nyumbani wote wana umuhimu kwa binadamu na kwa taifa nzima. Kwa hivyo, mada hii, itakuwezesha kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na mimea, vyakula na matunda pamoja na vipengele vya lugha vilivyoteuliwa katika mawasiliano.
Funzo a. Kutambua mimea mbalimbali na mazao yake
Shughuli 1.5 Kusoma na kuandika
Katika makundi madogo,
1. Shirikiana na wenzako kusoma na kujadiliana kuhusu taarifa katika makala hii.
Mimea na matunda.
Ni wazi kuwa maisha katika uso wa dunia hutegemea ubora wa huduma zitolewazo na mimea pamoja na matunda.Mimea ni uti wa mgongo wa maisha humu duniani kwa sababu huboresha maisha ya mwanadamu na mazingira.
kwanza kabisa ,kila kitu tunachokila huja moja kwa moja na huku vingine vikiwa si vya moja kwa moja kutoka katika mimea.Tukitazama historia ya mwanadamu,takribani mimea elfu saba,mimea ya aina tofauti tofauti imetumiwa na watu kama chakula. kando na haya, mimea pia imethibiti mzunguko wa maji.Mimea husaidia katika usambazaji na usafishaji wa maji yaliyomo katika sayari hii.Mimea huvuta hewa ya kaboni dayoksaidi wakati wa mchana ili kutegeneza chakula na kutuachia sisi binadamu na wanyama hewa safi ya oksijeni.Bila hewa safi,sisi hatungeweza kuishi.Pia inasaidia katika usafirishaji wa maji kutoka katika udongo hadi kwenye anga.vile vile,inapaswa tuelewe kuwa robo moja madawa yote ambayo sisi hutumia tukiwa wagonjwa hutoka katika mimea.mbali na haya , watu zaidi ya asilimia sabini hii leo wantegemea mimea kama msingi wa tiba yao.bila mimea ,viumbe wengi kama vile samaki na wanyama wa porini wangekosa makaazi iwapo mimea inge kuwepo.pia tusisahau kuwa mimea huwa ni kma vifaa vya ujenzi ya nyumba zetu.
Kwa upande mwingine ,taifa la uganda limebarikiwa na aina mbalimbali ya matunda kama vile maembe, mapapai,zeituni,balungi,tikitikimaji,nanasi,zambarau,ndimu,zabibu,maparachichi,bibo,tope,ubuyu,ukwaju,tunda nyaya,fenesi,ndizi mbivu, chenza mapera,machungwa mengine mengi.
Si ajabu leo kuwa watu wanaothamini sana matunda wanaishi maisha marefu kuwazidi wale wasiotumia matunda .Matunda huzuia maradhi mwilini na kumfanya mtu awe na afya bora.Hurutubisha mwili na kuupatia kinga. Pia ,matunda humpa mwanadamu madini na vitamini mbali mbali zinazosaidia kujenga, kukarabati na hata kuzuia bakteria.
1. Shirikiana na wenzako katika makundi kutambua na kueleza maana ya maneno mapya kutokana na makala. Mnaweza kutumia kamusi.
2. Shirikiana pia kujibu maswali yafuatayo;
i. Taja hoja nne za umuhimu wa mimea katika jamii yako.
ii. Watu wanaothamini sana matunda hufikwa na bahati gani?
iii. Je, matunda yana manufaa yoyote katika maisha ya binadamu kulingana na makala uliyosoma hapo juu?
iv. Nenda katika soko lililokaribu na kwenu kisha uandike majina ya matunda unayoyaona.
Shughuli 2.5 Kusoma na kuandika
Katika makundi,
1. Someni na kujadiliana kuhusu mimea na mazao yake kama ifuatavyo.
MIMEA NA MAZAO YAKE
2. Shirikiana na wenzako kutaja mimea sita inayopatikana nyumbani kwenu pamoja na mazao yake.
3. Someni na kujadili umuhimu wa mazao mbalimbali ya mimea
– Huwa ni kama chakula cha binadamu na wanyama.
– Ni mbolea hasa baada ya mazao haya kuozea shambani.
– Ni njia ya ajira ya watu wengine wanaopata kipato chao kwa kuyauza mazao ya mimea.
– Mazao ya mimea huweka kutuletea pesa za kigeni kupitia utalii hasa wakati watalii wanataka kutazama mimea ya kipekee isiyopatikana katika sehemu zingine za ulimwengu.
Funzo b: Msamiati wa matunda na vyakula mbalimbali.
Shughuli 3.5 Kusikiliza na kuzungumza
Katika makundi madogo,
1. Tazameni na kujadiliana kuhusu majina ya matunda yafuatayo katika Kiswahili.
Nanasi Maembe Parachichi chungwa
paipai kakara Mapera fenesi
2. Tazameni na kujadiliana kuhusu vyakula vya kawaida kutokana na maeneo unakotoka.
3. Jadiliana kuhusu vyakula vifuatavyo.
(a) Maharagwe
(b) Mahindi
(c) Wali
(d) Ngano
(e) Mtama
(f) Mawele
Funzo c. Kuigiza mazungumzo ya kuagiza chakula hotelini.
Shughuli 4.5 Kusikiliza na kuzungumza.
Katika makundi,
1. Shirikiana kusoma na kuigiza mazungumzo yafuatayo;
Muhindo: U hali gani Chepkorir?
Chepkorir: Nimepata afueni sasa ingawa bado nahisi maumivu kiasi.
Muhindo: Daktari amekuambia nini kuhusu maradhi yanayokusumbua?
Chepkorir: Mwenzangu, yangu ni mazito.
Muhindo: Mbona sikuelewi?
Chepkorir: Daktari aliniambia kuwa ninaugua kutokana na ukosefu wa lishe bora.
Muhindo: Kwani wewe huwa huli vizuri?
Chepkorir: Sijui, lakini yeye anadhani hivyo.
Muhindo: Basi alisema nini hasa?
Chepkorir: aliniambia eti mwili wangu una ukosefu wa madini na vitamini.
Muhindo: Alaa! Kwa hivyo wewe huwa huli matunda pamoja na mboga za majani.
Chepkorir: Ndio. Mimi huwa nikila nyama kwa wingi.
Muhindo: Basi hayo ndiyo matatizo. Hakikisha kuwa unapata lishe bora.
Chepkorir: Pia daktari ameniambia hivyo.
Muhindo: Amekuambia nini hasa kuhusu lishe hili bora?
Chepkorir: Ameniambia ninywe maji kwa wingi. Pia ameniambia nile matunda mbalimbali.
Muhindo: Basi fanya si ufanye hivyo?
Chepkoroir: La, mimi huwa sipendi kula kila matunda na mboga. Kwani nikila mengine huniletea kichefuchefu.
Muhindo: Ni yapi haya usiyoyapenda?
Chepkorir: Limau, Zabibu chungu, fenesi, tomoko, tikiti maji na pia parachichi.
Muhindo: Na yale uyapendayo ni yapi?
Chepkorir: Machungwa pekee.
Muhindo: Lo! Unafanya makosa makubwa sana rafiki yangu. Nataka uanze kula matunda ya aina mbalimbali ili uwe na afya bora. Mimi unavyoniona huwa nikila matunda na mboga ya aina mbalimbali kila siku ambayo yamenipa afya kama unavyoniona.
Chepkorir: Asante kwa ushauri wako mzuri rafiki. Nami nitaanza kula matunda na mboga bila ubaguzi ili niwe na afya nzuri kama yako.
2. Tafuteni maneno mapya kutokana na mazungumzo mliyogiza hapo juu.
Funzo d: Kusoma na kukaruri shairi
Shughuli 5.5 Kusikiliza na kuzungumza
Katika makundi,
1. Shirikiana kutunga, kusoma, kukariri na kuimba shairi kuhusu mimea
Sarufi:
Funzo e. Kutambua nomino za ngeli ya ki-vi
Shughuli 6.5 Kusoma na kuandika
Katika makundi madogo
Shirikiana kusoma na kujadiliana kuhusu matumizi ya nomino katika ngeli ya Ki – Vi.
Hii ni ngeli ya nomino ambayo inajumuisha nomino zinazoanza na kiambishi “Ki- “kwa umoja na” Vi- “kwa wingi. Aidha, kuna baadhi ya nomino katika ngeli hii ambazo huanzia na kiambishi “Ch- na Vy-” kwa umoja na wingi mfululizo. Kundi hili linajumuisha nomino zisizo na uhai.
UPATANISHO WA KISARUFI.
NOMINO VIONYESHI KUWA VIVUMISHI
Kiti hiki(this) ni(is) kidogo
kitanda kile (that) si(is not) kizito
chandalua kizuri
MIFANO
1,kiti hiki ni kizito. Viti hivi ni vizito.
2,kitabu hiki ni kizuri. Vitabu hivi ni vizuri.
3,kitanda kile si kichafu. Vitanda vile si vichafu.
4,chandulua kile si kizito. vyandalua vile si vizito.
NOMINO VIONYESHI KUWA VIVUMISHI
viti hivi(these) ni vidogo
vitanda vile (those) si vizito
vyandalua vizuri
majina vimilikishi(umoja) vimikilishi(wingi)
kiti changu(my /mine) vyangu
kitanda chako (your/s) vyako
kitambaa chake (his/her) vyake
kisu chetu (ours) vyetu
chenu(theirs) vyenu
chao(yours/p) vyao
mifano
1,kiti changu ni kizuri. Viti vyangu ni vizuri.
2,kitanda chako ni kizito Vitanda vyako ni vizito
3,kisu chenu ni kichafu. visu vyenu ni vichafu.
4,chandalua chao si kichafu. vyandalua vyao si vichafu.
majina viwakilishi(ki-) viwakilishi(vi-)
kiti kinatakwa vinatakwa
chakula kinapendwa vinapendwa
kioo kinakata vinakata
kitambaa kinasafisha vinasafisha
mifano
1 ,kiti kinatakwa. Viti vinatakwa.
2,chakula kinapendwa . Vyakula vinapendwa.
3,kioo kinakata. Vioo vinakata.
4,kitambaa kinasafisha . Vitambaa vinasafisha.
4. Shirikiana na wenzako wawili kutafuta na kuandika nomino nyingine za ngeli ya ki-vi katika umoja na wingi kutokana na kamusi.
5. Tunga sentensi angalau kumi kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya ki-vi katika umoja na wingi.
Funzo f: Kutambua vihusishi mbalimbali
Shughuli 7.5 Kusoma na kuandika
Katika makundi,
1. Shirikiana na wenzako kusoma na kutambua matumizi ya vihusishi mbalimbali.
Taz: Vihusishi ni maneno yanayotuarifu zaidi kuhusu uhusiano wa nomino na mazingira yake. Hutuonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jingine.
2. Shirikiana kusoma sentensi zifuatazo, kisha mjadiliane kuhusu maana ya sentensi hizo kwa kuongozwa na maneno yaliyopigiwa msitari.
A Nyuma ya
Kuna mpira nyuma ya mti huo.
Mbele ya
Anatembea mbele ya gari.
Chini ya
Baba alipumzikia chini ya mti.
Juu ya
Nimesimama juu ya daraja.
Kando ya
Watoto wanapenda kuogea kando ya
mto.
Karibu
Embe langu liko karibu na kikapu.
3. Shirikiana pia kusoma sentensi zifuatazo, kisha mjadiliane kuhusu maana ya sentensi hizo kwa kuongozwa na maneno yaliyopigiwa msitari.
B Kabla ya
i. Ni vizuri kuoga usiku kabla ya kulala.
Baada ya
ii. Mzee alikimbizwa hospitalini baada ya kula paipai lililooza na kugonjeka.
4. Kwa kuongozwa na vihusishi vilivyopigiwa mstari katika A na B, tambuua na kutofautisha vihusishi hivyo kati ya vihusishi vya mahali na vihusishi vya wakati
5. Shirikiana kutunga sentensi moja moja kwa kutumia vihusishi hivi.
(a) Kabla ya
(b) Kando ya
(c) Kwa
(d) Juu ya
(e) Baada ya
6. Someni na kujadiliana kuhusu mifano ifuatayo kisha utunge sentensi moja kwa kila
kihusishi.
a) nyuma ya
i). Mwizi alijificha nyuma ya nyumba yetu.
ii). Huyu mwanafunzi anapenda kukaa nyuma ya darasa.
b) hadi/ mpaka
i). Nimelala tokea jioni hadi asubuhi.
ii). Tulitembea kwa miguu kutoka Chuoni mpaka Kampala.
c) toka
i). Ninatoka mjini sasa.
ii). Baba alitoka kazini saa moja jioni.
d) bila
i). Mwanafunzi amekuja shuleni bila vitabu.
ii). Mtoto ametembea bila viatu.
e) katika
i). Mwalimu alitwambia kuweka madaftari yetu katika meza.
ii). Unalala katika bweni gani?
f) Kwa
i).Yusufu anakwenda kwa msikiti kusali.
ii). Nimesafiri kwa basi.
g) tangu/tokea
i). Nimekuwa Tanzania tokea mwaka wa 2010.
ii). Tumesoma vitabu tangu asubuhi.
h) na
i). Mwizi aliingia ndani na bunduki.
ii). SSali aliumwa na mbwa.
i) miongoni
i). Isabirye anapenda kuketi miongoni mwa wasichana.
ii). Miongoni mwa walimu mmoja ni kaka yangu.
j) baada ya
i). Mwalimu wa Kiswahili atakuja baada ya dakika kumi.
ii). Nitamaliza kazi hii baada ya siku tatu.
7. Shirikiana kutunga angalau sentensi kumi kwa kutumia vihusishi mbalimbali mlivyojadili hapo juu.
Funzo g: Kutunga sentensi sahihi kwa kutumia wakati uliopita na ukanushaji wake.
Shughuli 8.5 Kusoma na kuandika
Katika makundi,
1. Tamka sentensi angalau tano zenye vitendo vinavyofanya sasa hivi.
2. Kanusha sentensi zako mwenyewe kwa kukataa kuonyesha kitendo hicho hakitendeki.
Funzo h. Kuandika insha
Shughuli 9.5 Kuandika
Katika jozi, shirikiana kuandika insha fupi kuhusu matunda na mboga unayoyapenda na usiyoyapenda huku ukitoa sababu zako.
Shughuli ya jumla
Nyumbani kwenu, ninyi ni wakulima. Mna mashamba mbalimbali ambamo mnatoa mazao ya mimea mbalimbali. Mimea hii huzaa vyakula mbalimbali pamoja na matunda mbalimbali.
a. Elezea ni mimea ipi mnayolima nyumbani kwenu?
b. Kwa kutaja mazao mbalimbali, simulia jinsi mazao hayo yanavyowafaidi ninyi kama familia nzima.
c. Andika kifungu cha maneno kuhusu taarifa yoyote. Hakikisha kwamba kifungu hiki kina sentensi zenye matumiza ya sentensi za ngeli ya ki-vi pamoja na vihusishi.
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu,
a. Mimea mbalimbali na mazao yake.
b. Misamiati ya matunda na vyakula mbalimbali.
c. Uagizaji wa chakula hotelini.
d. Kukariri shairi fupi kuhusu mimea.
e. Mtumizi ya upatanishi wa kisarufi wa ngeli ya KI–VI.
f. Vihusishi na matumizi yake katika sentensi.
g. Uandishi wa insha.