To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
LSC: MADA KUU 1.6: BIASHARA
Utangulizi
Kila mtu, kwa njia moja au nyingine, ameshiriki katika biashara. Amefanya hivi kwa kuuza au kununua kitu kutoka mahali fulani. Je, wewe umewahi kuuza au kununua kitu? Ikiwa jibu lako ni ndiyo, ulikinunua kutoka wapi; dukani, sokoni au kutoka kwa mtu? Mada hii itakufunza msamiati unaotumia katika biashara na jinsi utakavyoutumia kujinufaisha wewe mwenyewe.
Funzo a: Kutambua msamiati wa bidhaa za dukani na sokoni
Shughuli 1.6: Kusikiliza na kuzungumza
Katika makundi,
1. Jadiliana kuhusu msamiati ufuatao na kisha;
i. Elezea maana ya kila msamiati
ii. Tumia msamiati huo kutunga sentensi kimapokezi
chumvi mtama mkate
kabichi mawele mteja
sukari bidhaa bei
mchele ngano nyanya
wimbi vibiriti nyama
2. (i) Tajeni bidhaa tano zinazopatikana katika duka lililokaribu na nyumbani kwenu.
(i) Je, soko lililokaribu na kwenu linauza nini? Toa mifano mitano.
Funzo b: Kutunga sentensi kwa kutumia msamiati unaohusiana na ununuzi na uuzaji wa bidhaa
Shughuli 2.6: Kusoma na kuandika
Katika vikundi,
i. Shirikiana na kujadili msamiati unaohusiana na ununuzi na uuzaji wa bidhaa na kisha, tumieni msamiati huo kutunga sentensi.
ii. Kila kikundi kisome kwa usahihi na kutunga sentensi sahihi kwa kutumia msamiati ufuatao:
pesa deni hasara mtaji nunua hisa bima
salio faida mteja bidhaa uza kipato bei fedha .
Funzo c: Kuigiza mazungumzo kati ya mnunuzi na muuzaji
Shughuli 3.6: Kusikiliza na kuzungumza
Katika jozi,
Igizeni mazungumzo kwa zamu kati ya muuzaji na mnunuzi. Kila mzungumzaji azungumze angalau mara sita.
Funzo d: Kusoma Makala kuhusu shughuli za kibiashara
Shughuli 4.6: Kusoma
Katika vikundi,
i. Someni kimya makala ifuatayo, na kisha mjadiliane ujumbe uliomo katika Makala.
ii. Someni kwa sauti makala ifuatayo na kuelezea ujumbe uliomo
iii. Kila kikundi kijibu maswali yanayopatikana mwishoni mwa makala.
Katika maisha ya binadamu soko ni sehemu nyeti sana kibinafsi, kijamii na kitaifa.
Mwanadamu ana mahitaji mengi sana katika kukimu maisha yake na miongoni mwa hayo kubwa ni chakula.
Hatua ya mwanzo imesimamia kilimo na hata wahenga walisema kuwa ‘Kilimo ni uti wa mgongo wa maisha’. Kwa maana hiyo bila ya kilimo, maisha ya binadamu yamo mashakani. Pia, bila ya harakati za kilimo, soko halitapatikana kwani bidhaa za sokoni tuzitumiazo zatokana na kilimo. Kwa mfano nguo ni pamba, mbao ni miti na vinginevyo.
Wakulima wengi na wasiokuwa wakulima tegemeo lao kubwa ni soko. Bali si hao tu. Taifa nalo linategemea soko. Mkulima hulima akachukua mazao ya mimea sokoni akauza ili apate fedha. Asiyekuwa mkulima pia shamba lake ni soko na ndio maana wajuzi wa kusema huamba eti soko ni shamba la wavivu. Kwa vile ulimwengu wa siku hizi jinsi ulivyoendelea umetenga maeneo maalum ya kuendesha shughuli kama hizo za uuzaji na ununuaji wa bidhaa za sokoni. Na hapo ndipo pia taifa hupata pato lake kwa kupitia serikali za mitaa kuwatoza ushuru wale washiriki wa biashara zinazofanywa sokoni.
Maswali:
1. Ipe makala hii kichwa mwafaka.
2. Kwa nini soko ni sehemu nyeti sana katika maisha ya binadamu?
3. Bidhaa nyingi za sokoni zinatokana na nini?
4. Taja bidhaa zinazotokana na ukilima/ kilimo.
5. Ni nini tegemeo kubwa la wakulima?
Sarufi
Funzo e: Kutambua nomino za ngeli ya i-zi na kuzitumia kutunga sentensi kwa kuzingatia vipatanishi vya ngeli ya i-zi
Shughuli 5.6: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na kuandika
Katika vikundi,
1. Shirikiana kutambua nomino za ngeli ya i-zi kwa umoja na wingi na kisha kila mwanafunzi aziandike katika daftari lake.
2. Shirikiana pia kutunga sentensi sahihi kwa kutumia nomino za ngeli ya i-zi kwa umoja na wingi.
NGELI YA “I-ZI”
Nomino katika ngeli hii huanza kwa kiambishi “ n” katika umoja na wingi. Hii ndiyo sababu ngeli hii imekuwa ikijulikana kuna ngeli ya “N” kwa sarufi ya kimapokeo.
UMOJA WINGI
Nyumba nyumba
nguzo nguzo
njugu njugu
ngazi ngazi
ndizi ndizi
ndoo ndoo
nyama
nyota
njia
nafasi
nyika
nta
ndoa
ndoto
njaa
njuga
Nomino zifuatazo pia zimo katika ngeli ya (i-zi) ingawa hazianzi kwa kiambishi N kwa vile herufi kutangulia herufi ambazo nomino hizo huanza nazo.
kamusi damu mvua chumvi tufani alama tauni
pombe firimbi siri sahani risasi meza pombe
sukari siri pamba bahari adabu adhabu
faida barabara chuki mbiu fedha biblia
Nyota
Mbegu
ile
Si
Ndogo
Ndefu
Ngumu
A,UMOJA
B,WINGI
Nyota
Mbegu
zile
si
Ndefu
Ndogo
Ngumu
C
Nyumba yangu
Nyota yako
Mbegu yake
Taa yetu
Amri yenu
Kazi yao
Nyumba zangu
Nyota zako
Mbegu zake
Taa zetu
Amri zenu
Kazi zao
Nyumba imeanguka
Suruali imeibwa
Nguo imeletwa
Sahani imepotea
Kazi imekwisha
Likizo imependeza
Meli imefika
Nyumba zimeanguka
Suruali zimeibwa
Nguo zimeletwa
Sahani zimekwisha
Kazi zimepotea
Likizo zimependeza
Funzo f: Kutunga sentensi kwa kutumia nyakati mahsusi
Shughuli 6.6: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Katika vikundi,
Kumbushana msamiati wa biashara ulioko katika ngeli ya i-zi na kuutumia kutunga sentensi sahihi. Sentensi zitungwe kwa umoja na wingi kwa kutumia njeo zifuatazo: na, ta, li, me.
Funzo g: Kuandika insha juu ya bajeti ya shilingi 10,000 utakazotumia
Shughuli 7.6: Kuandika
Katika vikundi,
Jadiliana kuhusu jinsi utakavyotumia shilingi elfu kumi. Baada ya majadiliano, tungeni insha juu bajeti ya shilingi elfu kumi au kiasi chochote cha pesa. Insha ya kila kikundi iwekwe kwenye chati na kutundikwa ukutani ili wanavikundi vingine waione.
Taz: Sarafu ni vipande vya fedha, karatasi au shaba vinavyothaminiwa na kutumiwa kama pesa za nchi husika.
Shughuli ya Jumla
Wazazi wako wamekupa shilingi 50,000 kwenda kununua vitu kutoka sokoni. Vitu utakavyonunua ni vya kutumia wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa dada yako ambako kutakuwako wiki ijayo.
a. Taja majina ya vitu ambavyo utanunua ili kuvitumia katika sherehe hiyo.
b. Kwa kila kitu ulichonunua, tumia jina la kitu hicho kutunga sentensi kwa umoja na wingi.
c. Simulia hadithi kuhusu jinsi ulivyotoka nyumbani kwenda sokoni, vitu ulivyonunua na namna ulivyorudi nyumbani.
d. Chagua Rafiki yako humo darasani na muigize mazungumzo; wewe ni mnunuzi na yeye ni muuzaji.
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu
a. kutambua misamiati ya sarafu mbalimbali.
b. kutambua misamiati ya bidhaa za dukani na sokoni.
c. kabaini misamiati ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa.
d. kuigiza mazungumzo ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa.
e. kusoma makala yanayohusu shughuli za kibiashara.
f. kutambua matumizi ya upatanishi wa kisarufi wa ngeli ya I–ZI.
g. kutambua vivumishi vya a-unganifu na matumizi yake katika sentensi.
h. kueleza matumizi ya vielezi husika katika sentensi.
i. kuandika insha ya mwongozo ya bajeti kuhusu vile utatumia shilingi 10,000/=.