• LOGIN
  • No products in the cart.

LSC: MADA KUU: 1.7 NYUMBA

LSC: MADA KUU: 1.7 NYUMBA

How To Prepare To Buy A House In 8 Steps | 2023 Guide

Utangulizi

Je, unaujua kwamba nyumba ni kitu muhimu katika maisha ya mtu? Ukweli ni kwamba kitu ambacho kila mtu anastahili kuwa nacho ili kuishi vizuri ni nyumba. Nyumba huwa ni za aina mbalimbali na katika nyumba huwa na vitu vingi ndani mwake. Je, ni aina ngapi za nyumba unazojua? Je, ni vitu gani tunavyopata katika nyumba? Je, kila kitu miongoni mwa vile ulivyotaja kina umuhimu gani? Mada hii itakuwezesha kutambua aina za nyumba, umuhimu
wa nyumba na vitu vinavyopatikana katika nyumba.

Funzo a: Kutambua sehemu za nyumba

Shughuli 1.7: Kusikiliza, kuzungumza na kuandika

Katika vikundi,

1. Jadiliana juu ya sehemu za nyumba na kisha mwakilishi wa kikundi asimame mbele ya darasa na kutaja sehemu za nyumba.
2. Andikeni majina ya vitu vinavyopatikana katika nyumba.
3. Choreni nyumba na kuonyesha sehemu za nyumba.

Funzo b: Kuimba wimbo kuhusu vitu vinavyopatikana katika nyumba

Shughuli 2.7: Kusikiliza na kuzungumza

Mkiwa katika vikundi,

1. Kila kikundi kibuni wimbo kuhusu vitu vinavyopatikana katika nyumba.
2. Kwa zamu, kila kikundi kiimbe wimbo kilichobuni.
3. Kila kikundi kieleze ujumbe uliomo katika wimbo wao.

Funzo c: Kutaja vitu vinavyopatikana katika sehemu mbalimbali za nyumba

Shughuli 3.7: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika

Katika vikundi,

1. Jadiliana na kuandika vitu vinavyopatikana katika sehemu mbalimbali za nyumba. Andikeni vitu mlivyotambua kwenye karatasi.
2. Kila kikundi kitaje vitu hivyo ili vikundi vingine vilinganishe na vile vya kikundi kilichowasilisha.

Funzo d: Kujadili umuhimu wa vitu vinavyopatikana katika nyumba

Shughuli 4.7: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika

Katika vikundi,

Jadiliana kuhusu vitu vinavyopatikana katika nyumba na kisha kila kikundi kieleze umuhimu wa vitu kilivyotambua.

Funzo e: Kusoma Makala

Shughuli 5.7: Kusoma

Katika vikundi,

1. Someni makala ifuatayo kwa makini mkiwa kimya na kutambua ujumbe uliomo.
2. Jadiliana kuhusu ujumbe uliomo katika Makala.
3. Someni Makala ifuatayo tena kwa sauti na kisha ujibu maswali yanayofuata.

Nyumba ni jengo ambalo huwa likitumiwa kama makaazi ya binadamu. Nyumbani ni muhimu sana kwa sababu humhifadhi mtu wakati wowote anapohitaji uhifadhi hasa wakati wa usiku ambapo nje huwa na hatari yake.

Hapo kale, mababu zetu waliishi katika nyumba zao zilizokuwa zikiitwa mapango ambayo yalikuwa na vijisehemu vingi sana. Hata hivyo, siku hizi mambo yamebadilika kwa sababu maisha ya kale ya kuishi mapangoni yamepitwa na wakati. Katika enzi za leo, nyumba za kisasa zimeenea katika sehemu mbalimbali humu nchini.

Nyumba hizi zinaweza kugawanywa katika makundi tofauti tofauti. Kuna zile za ghorofa na zisizo za ghorofa. Hali kadhalika, kuna nyumba zilizojengwa kwa kutumia udongo ambazo hufahamika kama nyumba za muda na zile zilizojengwa kwa kutumia saruji ambazo ni za kudumu. Watu wasio na uwezo wa kumiliki nyumba za ghorofa wala za saruji huamua kujenga nyumba za udongo.

Nyumba ya uwastani huwa na sehemu mbalimbali ndani yake. Kwanza kabisa tuna sebule. Hiki ni chumba cha kuwakaribisha wageni. Vile vile, ni mahali ambapo mikutano na mazungunzo yasiyo ya faragha hufanyikia ndani ya nyumba. Katika sebule vitu ambavyo hupatikana mle ni pamoja na viti vya kulalia, meza, mkeka, saa ya ukutani, redio, runinga, kabati, feni na kadhalika.

SCIENTIFIC VASTU | LIVING ROOM | An Architect Explains

Jikoni nayo ni sehemu nyingine muhimu ndani ya nyumba ambapo chakula hupikiwa. Sehemu hii imejengwa kiufundi sana kwa sababu huwa na dohani, ambayo ni tundu linalopitisha moshi. Hata hivyo, sio kila nyumba huwa na jikoni ndani yake. Kuna wale watu ambao jikoni zao huwa nje ya nyumba kuu kwa sababu wao hupika kwa kutumia kuni. Vitu kama vile visu, vijiko, uma, sufuria, sahani, bakuli, sinia na kadhalika hupatikana jikoni.

Choo ni sehemu nyingine muhimu katika nyumba. Kuna choo cha maji ambacho huwa kiko ndani ya nyumba na kile kisicho cha maji ambacho huwa kiko nje. Zaidi ya haya, choo kisichotumia maji, ambacho ni cha kitamadun, kinafaa kiwe ni cha urefu wa mita thelathini kutoka kwa nyumba kuu ili kuepukaa na maradhi yanayoweza kujitokeza kutokana na vimelea vinavyosambazwa na nzi wachafu.

Chumba cha kulala pia hupatikana ndani ya nyumba. Hapa ni mahali ambapo watu hupumzikia baada ya shughuli zao za mchaka kutwa. Katika chumba cha kulala, vitu vinavyopatikana mle ndani ni pamoja na kitanda, shuka, godoro, mto, blanketi na kadhalika.

 

Maswali

(a) Jikoni la kisasa na la kitamaduni, ni lipi unalopenda? Toa sababu.
(b) Tazama kwa makini mchoro wa sehemu ya sebule na utaje vitu unavyoona.
(c) Tumia kamusi kueleza maana ya maneno yaliyokolezwa.

Sarufi

Funzo f: Kutunga sentensi sahihi kwa kuzingatia vipatanishi vya kisarufi vya ngeli ya U-Zi

Shughuli 6.7: Kusoma na kuandika

Katika kikundi,

1. Jadiliana kuhusu nomino za ngeli ya u-zi na kuzitaja kwa umoja na wingi.

2. Shirikiana kutunga sentensi sahihi kwa kuzingatia nomino za ngeli ya u-zi.

3. Tungeni sentensi ishirini zenye vivumishi viashiria; kumi zikiwa kwa umoja na kumi zikiwa kwa wingi.

4. Someni sentensi zifuatazo kwa sauti.

Taz: Ngeli hii hujumuisha nomino zinazowakilishwa na U- katika umoja na ZI- katika wingi, kwa mfano,

Funzo g: Kutoa na kutekeleza amri

Shughuli 7.7: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika

Katika jozi,

1. Igizeni vitendo vya kutoa na kuitikia amri kwa umoja na wingi.
2. Mbadilishane nafasi ili aliyetoa amri kwanza, sasa aitikie amri.

Funzo h: Kutambua na kutekeleza hatua mwafaka za kuandika insha

Shughuli 8.7: Kusoma na kuandika

Katika vikundi,

Jadiliana kuhusu hatua mwafaka za kuandika insha nzuri na kisha kila kikundi kifafanue hatua kilizojadili.

Funzo i: Kuandika insha

Shughuli 9.7: Kuandika

Katika vikundi,

Jadiliana juu ya sehemu za nyumba. Baada ya majadiliano, kila kikundi kiandike insha juu ya sehemu za nyumba kikiongozwa na mwalimu. Insha iwe kati ya maneno 150-200

Shughuli Jumlishi

Umemaliza masomo yako na umehitimu na shahada ya kwanza, na sasa umepata kazi. Kwa sababu hiyo, umepata pesa kutoka kwa kazi ambayo unafanya na sasa unataka kujenga nyumba.

(i) Tambulisha aina ya nyumba ambayo utajenga

(ii) Eleza sehemu za nyumba ambazo nyumba yako itakuwa nazo.

(iii) Taja vitu ambavyo utaweka katika nyumba yako

(iv) Igiza jinsi utakavyokuwa unaamrisha wafanyakazi wako ambao watakujengea nyumba.

(v) Eleza sababu angalau tano kwa nini nyumba ya kisasa ni bora kuliko ya kitamaduni.

Muhtasari wa Mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu:

a. Sehemu za nyumba na umuhimu wake.
b. Kuimba wimbo na kueleza ujumbe uliomo.
c. Vitu vinavyopatika katika sehemu mbalimbali za nyumba.
d. Kujadili umuhimu wa vitu katika nyumba.
e. Kusoma na kujibu maswali kutokana na makala.
f. Upatanishi wa kisarufi wa ngeli ya U–Zi katika sentensi.
g. Kubainisha matumizi ya vivumishi viashiria/vionyeshi katika sentensi.
h. Kuamrisha na kutekeleza amri na ukanushi wake.
i. Viambishi vya wakati katika sentensi.
j. Hatua mwafaka za uandishi wa insha.
k. Kuandika insha ya mwongozo.

 

Courses

Featured Downloads