• LOGIN
  • No products in the cart.

LSC: MADA KUU 1.8 SHULENI

LSC: MADA KUU 1.8 SHULENI

Utangulizi
Elimu kama haki ya msingi, ni muhimu kwa kila binadamu. Ni jambo la maana sana katika maisha ya binadamu kupata elimu. Maarifa kadhaa hupatikana shuleni. Mada hii itakuwezesha kutambua na kutumia misamiati inayohusiana na shuleni pamoja na vipengele vya lugha vilivyoteuliwa katika mawasiliano.

Summary - Wote Shuleni - Fundraiso

Funzo a. Kutambua Watu shuleni

Shughuli 1.8 Kusikiliza na kuzungumza

Katika makundi, Jadiliana na kutaja watu mbalimbali wanaopatikana shuleni kwako.

Funzo b. Kueleza kazi za watu wa shuleni

Shughuli 2.8 Kusoma na kuandika

1. Shirikiana na wenzako kujadilina kuhusu kazi mbalimbali za watu wa shuleni
2. Ambatanisha watu wa shuleni wafuatao na wajibu wake.

Funzo c. Kutambua sehemu watu wanakofanyia kazi shuleni

Shughuli 3.8 Kusikiliza na kuzungumza

Katika makundi,

1. Taja na kujadili sehemu mbalimbali ambako watu wa shuleni hufanyia kazi zao.
2. Kwa kutumia mifano, jadiliana kuhusu tabia zinakubalika katika sehemu ambako watu hufanyia kazi.
3. Jadiliana kuhusu mnachojua juu ya sehemu mbalimbali zifuatazo.

Funzo e. Kubainisha umuhimu wa vitu vya shuleni

Shughuli 4.8 Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Jadiliana na wenzako kuhusu umuhimu mbalimbali wa vitu vya shuleni.
2. Someni na kujadiliana kuhusu umuhimu wa vitu vya vinavyopatikana shuleni.

Vitu ambavyo hupatikana shuleni huwa na umuhimu mkubwa sana kwa walimu, wanafunzi pamoja na wafanyikazi wote waliomo. Kwa mfano;

Darasa – huwa likitumiwa kuwafunzia wanafunzi.

Ofisi ya Mwalimu mkuu – huwa ikiwakaribisha na kuwashughulikia wageni.

Kengele – Huwa inawafahamisha wanafunzi na walimu kuhusu mwisho wa vipindi inapopigwa.

Chaki – kifaa kinachotumiwa kuandikia ubaoni.

Ubao – mwalimu hukitumia kwa kuandika juu yake ili wanafunzi watazame.

Chati – hutumiwa kuonyesha maandishi au michoro kwa maelezo ya ziada.

Kalamu – ni kifaa cha wanafunzi na walimu cha kuandikia vitabuni.

Kitabu – hutumiwa katika kubeba matini inayoandikwa kwa kalamu.

3. Katika makundi, taja na kujadiliana kuhusu vitu vinavyotumika sana shuleni kwenu.

KISWAHILI FOR BEGINNERS: SWAHILI AUXILIARY VERBS - Daily News

Funzo f. Kusoma makala

Shughuli 5.8 Kusoma na kuandika

Katika makundi madogo,

1. Shirikiana kuandika na kusoma makala fupi kuhusu watu wa shuleni
2. Someni na kujadiliana kuhusu makala ifuatayo na kisha kujibu maswali.

Kufanya maamuzi ya busara

Maamuzi ya busara huwa yana faida kubwa sana katika maisha ya mhusika. Wanafunzi wanafaa kuwa na mwelekeo mwema katika maisha yao ambayo itaongozwa na aina ya maamuzi wanayoyafanya.

Hata hivyo, imekuwa ni vigumu kwa wanafunzi na watu wengine kufanya maamuzi ya busara kutokana na vizuizi vifuatavyo:

3. Tabia za kujiunga na makundi mabaya ya wanafunzi.
4. Tamaa ya pesa ambapo mwanafunzi anajikuta mtegoni.
5. Maisha ya kuzini.
6. Ushauri mbaya kutoka kwa marafiki wa karibu.
7. Ubabe dume katika jamii unaomdhalilisha mtoto wa kike.
8. Wazazi wasiojali maisha ya wanao.

Umuhimu wa maamuzi ya busara
Habari sahihi kuhusu maamuzi ya busara ni muhimu kwa sababu;

• Inamfanya mwanafunzi ajiheshimu na kutofanya maamuzi mabaya maishani.
• Mwanafunzi anaweza kutulia darasani na kufanya vyema katika mitihani yake.
• Inamwepusha mwanafunzi dhidi ya maovu yanayoweza kumletea madhara.

Athari za maamuzi mabaya shuleni na nyumbani
Athari za maamuzi mabaya shuleni na nyumbani ni pamoja na;

• Vifo vya mapema kwa waathiriwa.
• Kuanguka mitihani shuleni.
• Kuambukizwa maradhi ya zinaa.
• Kufukuzwa shuleni kwa mwanafunzi.
• Kunajisiwa.

SHUGHULI ZA SHULENI
Katika makundi, shirikiana kusoma na kujadili taarifa ifuatayo

Shule huwa na shughuli mbalimbali. Kando na masomo ambapo wanafunzi hutarajiwa kufundishwa na walimu wao, kuna mambo mengine ambayo hufanyika pia. Shughuli hizi ni kama zifuatazo:

Michezo – Katika nyanja hii wanafunzi huhusika katika mashindano mbalimbali ikiwemo kandanda, riadha, kuogelea, mpira wa vikapu, mpira wa mikono na mengineyo.

Vilabu na vyama – Kuna pia vilabu mbalimbali ambavyo huwashirikisha wanafunzi tofauti tofauti. Hata hivyo, mwanafunzi hujiunga katika vilabu na vyama hivi kwa hiari yake mwenyewe bila kushinikizwa. Vilabu na vyama hivi ni pamoja na vile vya; Maskauti, Msalaba mwekundu, Drama na Uigizaji, Midahalo, Utunzaji misitu, uandishi wa habari na vingine vingi.

1. Shirikiana na wenzako katika kikundi kujibu maswali yafuatayo;

(a) Taja shughuli za shuleni zilizozungumziwa katika taarifa hii.
(b) Unadhani vyama vya Maskauti na Msalaba Mwekundu vina umuhimu gani shuleni?
(c) Ni shughuli zipi ambazo hazijazungumziwa katika taarifa hii lakini ungependa ziwemo katika shule yako?

Tanbihi; Msamiati wa ziada shuleni
1. Shirikiana na wenzako katika kikundi kujadiliana kuhusu msamiati zaidi wa shuleni ufuatao

Mada, kidato/darasa, mtihani, maabara, maktaba, kalamu, daftari, bweni, ubao, ratiba, chaki, kamusi, karatasi, ukumbi wa shule, shamba la shule, shule ya bweni, shule ya kutwa, kanisa la shule, msikiti wa shule, ua la shule, jiko la shule, chumba cha walimu, cheti cha stashahada, shahada, muhula, likizo, michezo, stakabadhi, n.k.

2. Kwa kujadiliana na wenzako, Jibu maswali yafuatayo

a. Toa manufaa mawili ya:
i. Maabara
ii. Maktaba
iii. Bweni
iv. Ukumbi wa shule

b. Tunga sentensi tano ukitumia haya maneno:
a) Kidato
b) Mtihani
c) Ubao
d) Mwanafunzi
e) Mchezo

Sarufi:

Funzo g. Kutunga sentensi kwa kutumia nomino za Ngeli ya ‘‘U-YA’’

Shughuli 6.8. Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Jadiliana na wenzako kuhusu matumizi ya nomino za ngeli ya U-Ya kama inavyofuata.

Baadhi ya nomino katika ngeli hii huanza kwa kiambishi ‘‘U-’’ kwa umoja na ‘‘Ma-’’ kwa wingi

Mifano,

2. Katika makundi madogo, Someni na kujadiliana kuhusu maana ya sentensi zifuatazo na kisha uziandike katika wingi.
i. Ugonjwa huu ni hatari
ii. Uovu wao ni mbaya
iii. Ugomvi wetu umeisha
iv. Upishi wake si mbaya
v. Ulaji wako ni wa kimaskini.

3. Sentensi hizo zimeandikwa katika wingi, shirikiana na wenzako kusoma sentensi hiz na kisha kuandika upya katika umoja.
(i) Wacha maovu yako.
(ii) Watu maskini wana malaji mabaya.
(iii) Maamuzi yetu ni sahihi.
(iv) Tumechoka magomvi yenu ya kila siku.
(v) Magonjwa haya yameenea kila mahali.

Funzo h. Kutumia kauli mbalimbali za Mnyambuliko wa vitenzi

Shughuli 7.8 Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Someni na kujadiliana kuhusu kauli mbalimbali za vitenzi zifuatazo.

(Kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa)

Mnyambuliko wa vitenzi ni jinsi vitenzi vinavyobadilika kulingana na kauli/hali mbalimbali.

Kauli ya Kutenda – Kitendo katika hali yake ya kawaida (bila kunyambuliwa)

Kauli ya Kutendea – Kufanya kitendo kwa niaba (au kwa ajili) ya mtu mwengine

Kauli ya Kutendwa – Kuathirika moja kwa moja na kitendo.

3. Tazameni na kujadiliana kuhusu mabadiliko ya vitenzi katika jedwali lifuatalo.

4. Shirikian na wenzako katika kikundi, kunyambua vitenzi hivi katika kauli uliyopewa mabanoni:

i. Anguka (kauli ya kutendea)
ii. Fundisha (kauli ya kutendwa)
iii. Kimbia (kauli ya kutendwa)
iv. Okoa (kauli ya kutendea)
v. Somwa (Kauli ya kutenda)

5. Tunga sentensi zako mwenyewe angalau tano na ubadilishe kila sentensi katika kauli ulizopewa.

Funzo i. Kutambua na kutumia kiambishi cha wakati uliopita – li –

Shughuli 8.8 Kusoma na kuandika

Katika makundi,

1. Someni na kujadiliana kuhusu mnachotazama katika jedwali.

2. Mmegundua nini? Tunga sentensi zako mwenyewe kwa kuongozwa na mifano hiyo katika jedwali lililojuu.

3. Someni tena mifano ifuatayo na kisha uzitunge katika njeo nyingine yoyote unayojua.

1. Mwalimu alifundisha juzi.

2. Baba alinunua gari mwaka jana.

3. Niliandika barua asubuhi.

4. Alisoma Kiswahili

5.Tulicheza kandanda vizuri

Zingatia: Wakati uliopita huonesha kitendo ambacho kilifanyika katika majira yaliyopita/ muda mrefu uliopita.

i. Mtindo wa kukubali

Tazama jedwali lifuatalo;

3. Shirikiana kusoma kwa sauti sentensi zifuatazo.

Soma sentensi hizi kwa sauti.

1. Nilisoma kitabu.
2. Alicheza kandanda.
3. Ulileta maji.
4. Mliandika barua.
5. Tulifanya mtihani.
6. Walienda shuleni.

ii. Mtindo wa kukanusha

Katika hali ya kukanusha, viwakilishi vinageuzwa hadi mtindo wa kukanusha, alama ya wakati ambayo ni –li- inageuka –ku-. Kwa mfano,

a) Nilisoma barua. – Sikusoma barua.

4. Katika jozi, shirikiana kusoma kwa sauti na kujadiliana kuhusu sentensi zifuatazo zilizokanushwa.

(a) Hakucheza kandanda.
(b) Hukuleta maji.
(c) Hamkuandika barua.
(d) Hatukufanya mtihani.
(e) Hawakuenda shuleni.

Zingatia: Vitenzi vya silabi moja katika hali ya kukanusha hupoteza ku-.

Kwa mfano;

1. Sikula chakula jana.
2. Hakuja nyumbani.
3. Hatukunywa maji.
4. Wagonjwa hawakufa.
5. Musa hakuwa rais wetu.
6. Shirikiana na jirani yako darasani kukanusha sentensi hizi zifuatazo.

Vitenzi vya silabi zaidi ya moja.

1. Mama alisahau kupika chakula.
2. Tulizungumza Kiswahili.
3. Waliezeka nyumba.
4. Baguma alitandika kitanda chake.
5. Kanzira alicheza muziki na Mutesi.
6. Kato alikuja shuleni jana.

Funzo j. Kuandika Insha

Shughuli 9.8 Kuandika

Katika makundi, saidiana kuandika insha inayoanza; “Siku yangu ya kwanza katika shule ya upili ilikuwa ya kusisimua…”

Shughuli ya jumla
Tangu ujiunge na shule yako hii, umepata marafiki ambao mshazoeana. Mnashirikiana katika kufanya kazi mbalimbali shuleni, Shuleni pia, kuna watu mbalimbali ambao hushughulikia kazi mbalimbali shuleni.

a. Kwa maelezo, simulia jina lako, shule yako, inapatikana wapi? ni kitu gani unapenda kuhusu shule yako? Ni watu
wanaopatikana shuneni kwako? Watu hao wanasaidia katika kufanya zipi? Ni sehemu zipi za shuleni unazojua na ni shughuli zipi zinazotendeka huko?
b. Yaandike masimulizi yako uliyoyatoa hapo juu.

Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu,

a. Watu wa shuleni.
b. Kzi za watu wa shuleni.
c. Watu wanaofanya kazi shuleni.
d. Vitu vya shuleni.
e. Matumizi ya vitu vya shuleni.
f. kusoma na kujibu maswali kutokana na makala.
g. Upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya U–YAkatika sentensi.
h. Kauli za mnyambuliko wa vitenzi pamoja na matumizi yake katika sentensi.
i. Kiambishi cha wakati uliopita pamoja na matumizi yake katika sentensi.
j. Ukanushaji wa kiambishi kanushi cha wakati uliopita na akanushe sentensi.
k. Uandishi wa insha

 

Courses

Featured Downloads