• LOGIN
  • No products in the cart.

Mada kuu 4.2: Amani na Usalam

Amani na usalama ni masuala muhimu yanayopachana. Haya pia ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Hata hivyo, usalama ni suala pana linaloangazia utulivu wa watu, asasi au mashirika mbalimbali na nchi nzima kwa ujumla. Usalama pia unaweza kuzingatia kuwepo kwa chakula, fedha na ulinzi kwa raia.

Maneno muhimu

amani

dhima

maendeleo

mapatano

maridhiano

ugomvi,

ukiukaji wa sheria

usalama vurugu,

Matarajio ya mafunzo

Mada hii itakuwezesha:

(a) kutambua msamiati wa amani na usalama.

(b) kufafanua mashirika yanayoendeleza amani na usalama.

(c) kutathmini dhima ya mashirika yanayoendeleza usalama.

(d) kujadili vitendo vinavyoashiria ukuaji wa amani na usalama.

(e) kusoma makala kuhusu jinsi ya kudumisha amani na usalama.

(f) kutumia vimilikishi na viunganishi katika sentensi.

(g na h) kutambua nomino za makundi na kuzitumia kutunga sentensi.

(i) kubainisha na kutumia alama zote za uakifishaji katika sentensi.

(j) kueleza maudhui ya usalama katika novela.

(k na l) kutambua hatua muhimu za uandishi wa insha ya tahariri na kuiandika.

Utangulizi

Amani na usalama ni masuala muhimu yanayopachana. Haya pia ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Hata hivyo, usalama ni suala pana linaloangazia utulivu wa watu, asasi au mashirika mbalimbali na nchi nzima kwa ujumla. Usalama pia unaweza kuzingatia kuwepo kwa chakula, fedha na ulinzi kwa raia.

Kwa hivyo, hali ya amani na usalama, inafaa kuwaleta watu pamoja katika kufanya kazi za kimaendeleo bila ugomvi, usumbufu na vurugu au vita. Je, kwa nini unafikiri amani na usalama ni mambo muhimu katika maisha ya binadamu? Mada hii itakuwezesha kutambua vitendo vinavyokubalika katika jamii ambavyo ni muhimu katika uendelezaji wa amani na usalama.

Funzo a: Msamiati wa amani na usalama

Stadi: Kusikiliza na kuzungumza

Shughuli 2.1: Kutambua msamiati wa amani na usalama.

Katika vikundi,

1. Tazameni picha ifuatayo kisha mjadiliane kuhusu mnachoona.

2. Kwa kurejelea picha mliyotazama katika (1) hapo juu,

i) Shirikiana katika kujadiliana na kutaja mambo mbalimbali yanayoweza kutokea au kutendeka katika jamii au nchi yoyote iliyo na amani na usalama.

ii) Jadiliana pia kuhusu mambo mbalimbali yanayoweza kutendeka katika nchi ambayo haina amani na usalama.

Funzo b na c: Dhima za mashirika yanayoendeleza amani na usalama

Stadi: Kusikiliza na kuzungumza

Shughuli 2.2: Kufafanua mashirika yanayoendeleza amani na usalama na kutathmini dhima za mashirika hayo.

Katika vikundi,

Kwa kutumia maktaba au mtandao wa intaneti, tafuteni na kuelezea mashirika mbalimbali ambayo dhima yake ni kuendeleza amani na usalama nchini Uganda.

Funzo d: Vitendo vinavyoashiria ukuaji wa amani na usalama

Shairi: Kusikiliza, kuzungumza na kuandika

Shughuli 2.3: Kujadili vitendo vinavyoashiria ukuaji wa amani na usalama.

Katika vikundi,

1. Shirikiana katika kufanya utafiti na kujadili vitendo mbalimbali ambavyo vinaweza kusababisha hali ya utulivu katika jamii yako.

2. Ungekuwa kiongozi katika jamii yako, ungewashauri wanajamii kufanya nini au ungefanya nini ili kila mtu aishi kwa amani?

Funzo e: Ufahamu: Jinsi ya kudumisha amani na usalama

Stadi: Kusoma na kuandika

Shughuli 2.4: Kusoma makala kuhusu jinsi ya kudumisha amani na usalama.

Katika vikundi,

1. Shirikiana katika kusoma taarifa ifuatayo na kujibu maswali yatakayofuata.

Siku hiyo ndipo wanafunzi wengi tulitambua kwamba kuna mengi yaliyokuwa yametokea kabla ya kuzaliwa kwetu. Huku tukiendelea kuchora picha akilini, kila mtu alikuwa amenyamaza na kutulia tuli kama maji mtungini! Osiru Umar ambaye ni mhamasishaji mtendaji wa haki za binadamu, aliendelea kutusimulia hali ya amani na usalama ilivyokuwa nchini wakati alipokuwa kijana.

“Wakati huo, tulikuwa hatuwezi kutembea wakati wa usiku. Waliotembea usiku, wangechapwa viboko na kuporwa kila kitu. Aliyenusurika kuuawa, wakati mwingine wangemwachia mavazi ya ndani tu ili aweze kuziba utupu wake! Ujambazi ulikuwa umekithiri, mauaji ya kila siku yaliwaacha mayatima wengi bila mbele wala nyuma. Wafanyabiashara wengi waliamua kujiuzulu kazini kwa kuchoka na hali ya ukosefu wa usalama. Hata hivyo, hakukuwa na ukarabati wala ujenzi wowote wa miundombinu kwa sababu hali ilikuwa tete kiusalama wakati huo. Umiliki haramu wa bunduki ulikuwa umekithiri. Suala hili lilisababisha vurugu kubwa kila siku katika nchi yetu.

Kwanza kabisa, hakukuwa na kazi kwa vijana. Wale wachache waliopata kazi, wangekuwa ama ndugu au marafiki wa waliokuwa madarakani. Kwa sababu hiyo, vijana wengi wangeanzisha migomo na maandamano ambayo pia wakati mwingine hali ingeishia katika ghasia kwa kuharibu mali za watu. Walioshikwa na maafisa wa vyombo vya ulinzi vya serikali ya wakati huo katika maandamano hayo, wakati mwingi wangepigwa, wengine wangelemazwa na hata wengine hawakupata kuonekana tena.

Ni wakati huo pia ambapo vitendo vya waasi na magaidi vilipoanza kusikika sehemu mbalimbali za nchi. Ungesikia kwamba mabomu yalilipuka usiku na kuua watu huku au kule. Kuna wakati ungesikia redioni kwamba waasi wamevamia kijiji au shule fulani, wamebaka wanawake au wasichana, wamewateka nyara vijana na kuwafanya kurutu, wengine wangeonekana wakilia kuwa mifugo yao yote ilikuwa imeporwa. Hata hivyo, kuna watu waliouliwa na wengine nyumba zao kuchomwa bila sababu. Kwa kweli hali ilikuwa ngumu!”

Baada ya kuzungumzia mengi yaliyotendeka wakati wa ujana wao, Bwana Osiru alianza kusimulia tena juu ya mafanikio ya serikali ya wakati huu. Alianza kwa kuturai kuombea nchi yetu ili iendelee kuwa na amani na usalama.

“Siku hizi, ninafurahi sana ninapoona wanafunzi wakisoma shuleni bila hofu yoyote ya mchafuko wa kisiasa. Kwa sasa demokrasia ndiyo inayotawala. Hakuna unyakuzi tena wa madaraka kwa mtutu wa bunduki, ila raia ndio wanaojichagulia viongozi wao wanaowataka. Hata hivyo, kumewekwa taasisi mbalimbali za kuchunguza mafisadi, wanyakuzi wa ardhi, unyanyasaji kwa misingi ya kijinsia, unyanyasaji wa watoto na kadhalika.

Hata ingawa bado kuna changamoto za ukosefu wa kazi, serikali siku hizi inawapa vijana stadi, ufundi na mtaji wa kuwawezesha kujiajiri. Suala hili kwa kiasi kikubwa limepunguza migomo na maandamano ya mitaani.

Wakati huu si kama ule ambao watu wangekumbwa na janga la njaa pamoja na umasikini. Siku hizi kila mtu anashughulika katika kazi mbalimbali. N bayana kwamba elimu bora, shughuli za biashara na ubunifu ni masuala muhimu ambayo yamechangia pakubwa maendeleo ya nchi yetu siku ya leo

2. Shirikiana na mwenzako katika kutafuta maneno mapya kutokana na hadithi, kisha elezeni maana ya maneno hayo kwa kutumia kamusi au mtandao

3. wa intaneti. Pendekezeni kichwa cha makala hii.

4. Shirikiana katika kujibu maswali yafuatayo;

i) Taja jina na kazi ya aliyewasimulia hadithi hii kwa wanafunzi.

ii) Ni mambo gani yaliyotendeka katika serikali za zamani yaliyosababisha ukosefu wa amani na usalama?

iii) Andika zaidi ya mambo matano ambayo ungeshauri serikali pamoja na wanajamii wenzako kufanya ili kudumisha amani na usalama.

Funzo f: (i) Viwakilishi vimilikishi

Stadi: Kusoma na kuandika

Shughuli 2.5: Kutumia viwakilishi vimilikishi katika kutunga sentensi.

Zingatia

Viwakilishi vimilikishi ni maneno yanayotumika katika sentensi kuonyesha uhusiano wa kitu kuwa mali ya mtu au kumilikiwa na kitu kingine. Viwakilishi vimilikishi hutumika kwa kuambatanishwa na vya ngeli kulingana na nomino zinazohusika.

1. Somea mwenzako na kujadiliana kuhusu matumizi ya viwakilishi vimilikishi katika sentensi zifuatazo.

3. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiunganishi mwafaka.

(a) Ningekuja mapema mvua imenyesha tangu asubuhi. nimesikia kwamba kuna mgomo. (b) Sitaenda mjini leo

(c) Mwalimu Galabuzi aliendelea kufundisha walikuwa wanaongea darasani. wanafunzi

(d) Kachaacha anatumia penseli kuandika

(e) kalamu ya wino. Ojere anatumia kugombana hadharani, ni vizuri kukaa na kusuluhisha matatizo yenu kwa amani.

Funzo g na h: Nomino za makundi

Shughuli 2.7: Kuandika Kutunga sentensi kwa kutumia nomino za makundi. Katika vikundi, 1. Somea mwenzako na kujadiliana kuhusu taarifa katika kifungu kifuatacho. Siku hiyo tuliamka majogoo mimi na mama yangu ili tusiachwe na feri iliyokuwa ikienda kisiwani Kalangala.

Tulifika pale Nakiwogo kwenye kituo cha kupandia na kushukia wakati wa saa mbili asubuhi hivi, tulikuta umati wa watu waliokuwa wamesubiri ile feri tangu alfajiri. Kulikuwa pia na mlolongo wa magari yaliyosubiri kusafirishwa. Ilikuwa ni siku ya kusherehekea uhuru. Sherehe za kitaifa zingefanyika kisiwani katika wilaya ya Kalangala. Baada ya muda mfupi, feri ilionekana kwa umbali kiasi ikikaribia.

Hata ingawa kulikuwa na ukungu mwingi ziwani, taa zake zilionekana kwa umbali huo kama thurea ya nyota katika mbingu. Iliwasili ikipiga honi mchanganyiko ili kuwasafirisha raia wazalendo kwenda kusherehekea siku kuu ya uhuru wa nchi yao. Wengi walikuwa wamevalia mavazi ya rangi mbalimbali hasa rangi zilizofanana na za bendera ya taifa. Wengine walikuwa wamejipaka rangi, wengine walikuwa wamejipodoa, hata mama yangu alikuwa amejifunga shada la maua shingoni. Baada ya muda mfupi, tulianza kuingia ndani ya feri polepole.

Tulikaa katika chumba kimoja kilichokuwa kwenye ghorofa la pili la feri hiyo. Sote tulikaa kwa utaratibu kama darasa la wanafunzi. Nilikuwa nimekaa karibu na mwanamke mmoja aliyekuwa amepakata kifurushi cha pesa.

Nilijifanya ninaangalia nje kupitia dirishani, nikamwona akitumia kitenge kufichia bunda la noti za shilingi elfu kumi. Sikusema lolote. Niliendelea kuangalia nje nikitazama maji yaliyoelea. Mle majini, niliona kitu kama mzoga ambao sikutambua vizuri.

Mzoga ule ulikuwa umegubikwa na bumba la nzi waliorukaruka juu yake. Sikutaka kuangalia huko mara nyingine. Kuna mambo mawili yaliyonishangaza pale katika feri. Kuna magari yaliyokuwa yamebebwa pale ambayo pia yalikuwa yamebeba vitu vingine. Kwa mfano, kuna gari aina ya tipa, lilikuwa limebeba matita ya kuni, kuna lingine lilikuwa limebeba mikungu ya ndizi na jingine robota za nguo. Baada ya muda mfupi, safari yetu ilifikia hatima.

Tulishuka na kwenda katika uwanja wa sherehe. Tulipofika katika uwanja wa sherehe, tulikuta jeshi la askari tayari kwenye gwaride likimsubiri mgeni rasmi. Kikosi cha bendi ya polisi pia kilikuwa kimeanza kuvumisha tarumbeta. Rais alipowasili, sherehe ilianza. Tulifurahia sherehe hiyo mpaka ilipoisha muda wa saa tisa hivi alasiri.

2. Pendekezeni kichwa kinachofaa makala hii.

3. Mweleze mwenzako maana ya nomino za makundi zilizokolezwa.

4. Tungeni sentensi sahihi kwa kutumia nomino zozote kumi za makundi.

Funzo i: Matumizi ya alama za uakifishaji katika sentensi

Stadi: Kusoma na kuandika

Shughuli 2.8: Kubainisha alama za uakifishaji na kuzitumia kutunga sentensi.

Katika vikundi,

1. Shirikiana katika kusoma na kujadili matumizi ya alama za uakifishaji zilizotumiwa. Fanya utafiti na kuandika majina ya alama hizo za uakifishaji na kueleza matumizi yake. katika sentensi zifuatazo;

(a) “Msichezee darasani”. Mwalimu aliwaambia wanafunzi.

(b) “Mmesoma somo gani asubuhi?” Kakeeto aliomba kujua.

(c) “Pole sana kwa kupoteza kalamu!” Abwoli alimwambia Wodero.

(d) Bi. Nambirige hudai vitu vitatu kutoka kwa kila mtu; amani, usalama na heshima.

(e) Wanyama wa nyumbani (mbuzi, kondoo, ng’ombe na nguruwe) wote wana faida kwa binadamu.

2. Shirikiana katika kutunga sentensi sahihi zisizopungua tano kwa kutumia alama mbalimbali za uakifishaji.

Funzo j: Uchambuzi wa Novela

Stadi: Kusoma na kuandika yenye

Zingatia Novela ni kazi ya sanaa iliyoandikwa kama hadithi ndefu sifa zifuatazo; usahili wa muundo, wahusika wachache, mandhari machache tena yanayodhihirika moja kwa moja, inakuwa na ploti sahili, pamoja na maudhui yasiyo mengi ikilinganishwa na riwaya.

Kazi mradi

Shughuli 2.9: Kusoma na kueleza maudhui kutokana na novela.

Katika vikundi, Kwa kurejelea novela au hadithi yoyote inayohusu amani na usalama, shirikiana katika kuisoma na kuijadili.

Funzo k na 1: Hatua za kuandika insha ya tahariri

Stadi: Kuandika

Shughuli 2.10: Kutambua hatua muhimu za kuandika insha ya tahariri na kuiandika.

Katika vikundi,

1. Tafitini katika magazeti na mtandaoni kuhusu tahariri.

2. Elekezana na mwenzako kuandika tahariri kuhusu amani na usalama.

Zingatia

Tahariri huandikwa na mhariri wa gazeti au jarida husika kama maoni yake kuhusu suala fulani. Hatua au mambo muhimu yanayofaa kuzingatiwa katika uandishi wa tahariri ni; Jina la gazeti/jarida, tarehe pamoja na juzuu au nambari ya toleo hilo, mada ya tahariri, ujumbe wenyewe na kisha jina la mwandishi.

Muhtasari wa matarajio ya mada

Katika mada hii, umejifunza:

msamiati wa amani na usalama. mashirika yanayoendeleza amani na usalama. dhima ya mashirika yanayoendeleza amani na usalama. vitendo vinavyoashiria ukuaji wa amani na usalama. kusoma makala na kujibu maswali. kutunga sentensi kwa kutumia viwakilishi vimilikishi na viunganishi. kutambua, kueleza nomino za makundi na kuzitumia katika sentensi. kubaini na kutumia alama za uakifishaji katika sentensi. kueleza maudhui ya usalama katika novela. kutambua hatua muhimu kuhusu insha ya tahariri. kuandika insha ya tahariri.

Assignment

Mfano wa Shughuli jumlishi: Amani na Usalam

ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli jumlishi: Amani na Usalam MARKS : 10  DURATION : 1 week, 3 days

 

Courses

Featured Downloads