To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Maneno muhimu
dhima
jinsia
kubaguliwa
kurithi
dhalilisha
ubaguzi
kunajisiwa
Matarajio ya mafunzo Mada hii itakuwezesha:
(a) kutambua msamiati unaohusiana na jinsia
(b) kueleza haki za kijinsia.
(c) kujadili dhima ya mwanamke katika maendeleo ya nchi
(d) kusoma shairi linalohusu haki za kijinsia na kujibu maswali
(e) kuainisha viwakilishi vya a-unganifu
(f) kutambua vivumishi vya ki- ya mfanano
(g) kuhakiki usawa wa kijinsia katika jamii.
(h) kufafanua maana kamili ya methali na matumizi yake.
(i) kueleza utaratibu wa kuandika insha ya onyo na ilani.
(j) kueleza utaratibu wa kuandika insha ya onyo na ilani. kuandika insha ya onyo.
Utangulizi Jinsia ni hali ya wanadamu kuwa wa kiume au wa kike kwa kuzingatia tofauti za kijamii na kitamaduni badala ya zile za kibiolojia. Je, wewe ni wa jinsia gani? Je, ni majukumu yapi yanayofaa kushughulikiwa na jinsia fulani? Mada hii itamwezesha kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na jinsia pamoja na vipengele vya lugha mbalimbali.
Funzo a: Msamiati wa Kijinsia
Shughuli 4.1: Kutambua msamiati unaohusiana na jinsia.
Stadi: Kusikiliza na kuzungumza
Katika vikundi,
1. Shirikiana katika kutazama picha zifuatazo na kisha mtaje watu mnaowaona.
2. Mkiwa wawili wawili, pangeni msamiati wa jinsia ufuatao katika upande unaofaa. Upande mmoja uwe wa jinsia ya kike na mwingine uwe wa jinsia ya kiume.
Mke, mvulana, binti, dada, mjomba, mwanamume, babu, mwanamke, bikizee, mume, mlamu, baba, shangazi, bin, baba wa kambo, msichana, kaka, nyanya, mjane, mama, ami
3. Elezeni maana ya msamiati wa jinsia mliopanga katika (2) hapo juu kwa kutumia kamusi au mtandao wa intaneti.
Funzo b: Haki za Kijinsia
Stadi: Kusikiliza, kuzungumza na kuandika.
Shughuli 4.2: Kueleza haki za kijinsia. Jadilini haki za kijinsia ambazo mtoto wa kike na wa kiume wanastahili kupewa.
Funzo c: Dhima ya mwanamke katika maendeleo ya nchi
Zingatia
Wanawake wamechangia pakubwa maendeleo ya jamii kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, wengi; hutoa elimu hasa kuanzia nyumbani wanapofundisha watoto wadogo na shuleni ambapo wengine wanaoelimisha vilevile ni walimu wa kike.
Hufanya biashara na kuchangia mapato ya familia, ni viongozi wa kijamii na kitaifa, hufanya kazi hasa za kujitolea kwa mfano; shuleni, katika vituo vya kulelea watoto yatima, makanisani, mashambani. Wengi pia ni wanaharakati wa haki za binadamu na kadhalika.
Shughuli 4.3: Kujadili dhima ya mwanamke katika maendeleo ya nchi.
Stadi: Kusikiliza na kuzungumza
Katika vikundi,
1. Tazameni picha zifuatazo na mtajiane shughuli zinazoendeshwa na wanawake.
2. Jadilini kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanawake ambazo ni muhimu katika maendeleo ya nchi.
3. Someni hadithi ifuatayo kisha mjibu maswali yatakayofuata.
Zamani, katika kijiji cha Kabonera, kuliishi familia mbili jirani. Familia moja ilikuwa ya Mzee Kakuba na nyingine ilikuwa ya Mzee Byekwaso. Mzee Kakuba na mkewe walikuwa na watoto wa kike wawili. Mzee Byekwaso na mkewe walikuwa na watoto wawili pia, binti mmoja na bin mmoja.
Mzee Kakuba na mkewe, walitia bidii sana katika kutafuta karo za shule ili kuwapeleka mabinti zao wawili shuleni. Mzee Byekwaso yeye, alitia bidii katika kumfundisha mtoto wa kiume na kumwacha binti yake nyumbani.
Siku moja, Mzee Kakuba aliguswa na suala la Mzee Byekwaso kutompeleka mtoto wa kike shuleni. Aliamua kumtembelea Mzee Byekwaso ili walizungumzie.
Mzee Kakuba: Ndugu yangu, mbona umeamua kumwachisha shule mtoto wako wa kike?
Mzee Byekwaso: Mimi ninaona hakuna faida yoyote kumfundisha mtoto wa kike. Kwa sababu, akifikisha miaka kumi na minane, atakuwa huru kuolewa. Akitoka hapa, hatanisaidia sana. Afadhali nimsomeshe mtoto wa kiume. Huyo atabaki hapa na huenda atanisaidia.
Mzee Kakuba: Ndugu yangu, hiyo ni fikra potovu kwamba mtoto wa kike hafai kupata elimu eti kwa sababu ataolewa na kutoka hapa nyumbani. Mimi nina mabinti wangu wawili. Lazima nifanye lolote liwezekanalo ili wapate elimu mpaka wafike chuo kikuu.
Mazungumzo yaliendelea, lakini Mzee Byekwaso hakushawishika kumlipia binti yake karo za shule. Mwishoni walikubaliana kwamba Mzee Kakuba angemlipia msichana huyo karo za shule. Kwa hivyo, Mzee Kakuba alianza kulipa karo za watoto watatu; alilipia binti zake wawili na yule binti ya Mzee Byekwaso.
Wasichana hawa wote watatu walisoma vizuri mpaka wakajiunga na chuo kikuu. Yule bin ya Mzee Byekwaso, alipofika kidato cha tatu, alianza kushirikiana na vijana wa tabia mbaya. Mwishowe walijifunza kutumia dawa za kulevya na kutoroka shuleni. Tulisikia baadhi ya vijana hao walianza kuzurura na kuishi mitaani.
Wasichana wale watatu wote walifuzu masomo yao vizuri sana na kila mmoja Bakapata digrii. Binti zake wawili Mzee Kakuba, mmoja alifuzu ualimu na mwingine uwakili. Binti yake Mzee Byekwaso, alifuzu udaktari. Huyu alipata kazi moja kwa moja katika hospitali kuu ya rufaa ya Mulago jijini Kampala. Baada ya mwaka mmoja, wale binti za Mzee Kakuba pia kila mmoja alipata kazi nzuri. Kila mmoja alilipwa zaidi ya milioni tano.
(a) Tajiana maneno mapya kutokana na hadithi na kuelezana maana yake.
(b) Mmejifunza nini kutokana na hadithi hii.
Nchini Uganda, katiba inawapa wanawake na wanaume nafasi sawa ili kuwawezesha kushiriki katika maendeleo ya nchi.
Tangu zamani kumekuwa na tamaduni fulani ambazo zimebagua watu wa jinsia ya kike na kupendelea wa kiume bila kuzingatia usawa wa kibinadamu ambao Mungu alidhamiria uwepo alipoumba binadamu.
Wanawake wengi wameteseka chini ya baadhi ya tamaduni. Wasichana ni miongoni mwa wale ambao wameozwa wakiwa na umri mdogo kwa lazima na wazazi walafi. Wengine wameozwa kwa waume wasiowapenda kwa sababu ya utamaduni mbaya. Baadhi ya wanawake wametengwa na kubaguliwa katika uongozi wa jamii hata wakazuiliwa kurithi mashamba. Hali hii inawanyima heshima na kuwafanya wadharauliwe.
Si wanawake waliokomaa pekee ambao wamedhalilishwa bali hata kuna baadhi ya watoto wa kiume ambao wameathirika kwa kulawitiwa na wale wa kike kunajisiwa. Visa hivi vimewasilishwa mahakamani ili kushughulikiwa. Kupitia katiba ya Uganda, hali ya ubaguzi imejaribu kusawazishwa kwa kulinda haki ya kila jinsia. Kufikia sasa, baadhi ya wanawake wameshirikishwa katika sekta mbalimbali kama vile za uongozi wa nchi, elimu, biashara na kadhalika.
Juhudi zinazidi kufanywa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na wanawake kuhakikisha usawa wa kijinsia unadumishwa.
5. Shirikiana na wenzako kujibu maswali yafuatayo;
(a)Fafanueni maana ya msamiati uliokolezwa kutokana na taarifa.
(b) Elezeni hoja zisizopungua tano kuhusu jinsi haki za mtoto wa kike zimekandamizwa kulingana na taarifa.
6. Kwa kurejelea zingatio katika utangulizi wa funzo hili, (funzo c), elezeni shughuli mbalimbali ambazo hufanywa na wanawake zinazochangia maendeleo ya jamii.
Funzo d: Ufahamu: Shairi linalohusu haki za jinsia
Stadi: Kusoma na kuandika
Shughuli 4.4: Kusoma shairi linalohusu haki za kijinsia na kujibu maswali.
1. Msomee mwenzako shairi lifuatalo kisha mshirikiane kujibu maswali chini
yake.
Mie binti wa nyumbani, kama ndege nitunzie,
Kanilishe mdomoni, maji pia niyanywie,
Univishe kwa makini, afya niifurahie,
Nifungue mbawa zangu, nipae kama kipungu.
Kama mbawa mgongoni, vitabu nikafungue,
Nifike hadi chuoni, masomo nimalizie Nihitimu vya shuleni, ndugu kazi tuwanie, Nifungue mbawa zangu, nipae kama kipungu
Sawa na undu kichwani, uongozi nipatie, Nafasi serikalini, hata bungeni nikae,
Niko sawa akilini, vikao tuje tukae,
Nifungue mbawa zangu, nipae kama kipungu
Kama nyoya za mwilini, kote dunia nipae, Usinifungie ndani, ujinga na unijae, Ukanitoe gizani, jua liniangazie
Nifungue mbawa zangu, nipae kama kipungu
Nipe kidona cha nyuni, ujumbe nikautue, Nijaze wangu uneni, walimwengu wasikie,
Nikae mikutanoni, kote nijumuikie,
Nifungue mbawa zangu, nipae kama kipungu
Nishiriki michezoni, mti mwema nikatue
Sinitupe kwa fulani, mzee uniozee,
Acha hizi tamaduni, mwisho wacha nichague
Nifungue mbawa zangu, nipae kama kipungu
(a) Lipeni shairi hili anwani ifaayo.
(b) Mwelezee mwenzako maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika
katika shairi.
i) nihitimu
ii) undu
iii) uneni
iv) tuwanie
v) kidona
(c) Msemaji katika shairi hili ni wa jinsia gani?
d)
Kwa kutumia lugha ya kawaida, elezeni haki zisizopungua tatu ambazo msemaji katika shairi hili anataka zitimizwe.
(e) Jadiliana na kujibu maswali haya.
(i) Hili ni shairi la aina gani?
(ii) Lina mishororo mingapi katika kila ubeti?
(iii) Taja vina vilivyotumika katika shairi hili.
(iv) Kila mshororo wa shairi hili una vipande vingapi?
(v) Kila mshororo una jumla ya mizani ngapi?
(vi) Andika kibwagizo kilichotumika katika shairi hili.
Funzo e: Viwakilishi vya a-unganifu
Stadi: Kusoma na kuandika
Shughuli 4.5: Kutunga sentensi kwa kutumia viwakilishi vya a-unganifu.
Katika vikundi,
na wingi.
Funzo f: Vivumishi vya ki- ya mfanano
Stadi: Kusoma na kuandika
Shughuli 4.6: Kutunga sentensi kwa kutumia vivumishi vya ki- ya mfanano.
Katika vikundi,
Ubaguzi wa wasichana kijinsia ni suala linalopingwa wakati wa sasa. Suala hili linafaa kuangaliwa kimakini na kitaratibu ili kuwasaidia wasichana na wanawake katika jamii kujiendeleza kimaisha na kimaadili. Usawazishaji wa binadamu si jambo la kijinga bali ni la kibusara. Hali hiyo ndiyo itafanya watu wote kuishi kitulivu.
Kwa mfano;
Awisi amevaa kiofisa leo.
Funzo g: Tamthilia
Stadi: Kusoma na kuandika
Zingatia
Tamthilia ni utanzu wa fasihi ambao hutegemea mazungumzo na uigizaji ili kuwasilisha ujumbe wake kwa wasomaji au hadhira. Mara nyingi, utanzu huu huandikwa kwa mtindo wa mazungumzo ya wahusika.
Shughuli 4.7: Kuhakiki usawa wa kijinsia
Kwa kurejelea tamthilia yoyote iliyo na maudhui ya kijinsia, elezeni jinsi usawa
wa kijinsia unavyoendelezwa.
Funzo h: Fasihi Simulizi: Methali
Stadi: Kusoma na kuandika
Shughuli 4.8: Kufafanua maana kamili ya methali tofauti na matumizi yake.
Katika vikundi;
1. Someni kifungu kifuatacho kisha mjibu maswali yatakayofuata.
Maji yakimwagika hayazoleki.
Kwa kawaida maji yakimwagika sakafuni kiajali, hata kama yalitarajiwa kutumiwa hayawezi kuchotwa tena yakatumiwa.
Methali hii inamaanisha kwamba jambo likishaharibika huwa vigumu kulirekebisha. Inatueleza kwamba hakuna haja kuendelea kulilia na kujutia jambo lililopitwa na wakati na badala yake tushughulikie jambo jipya litakaloleta faida.
Methali hii ina maana sawa na cha kuzama hakina usukani, cha kuvunja hakina rubani na la kuvunda halina ubani.
Katika kijiji cha Namagoma wilayani Wakiso, kulikuwa na mzee Mate aliyejaliwa kupata watoto watano wa jinsia ya kike pekee. Mkewe Asio alitarajia binti zake wapelekwe shule wasome kama binti wengine lakini hali ilikuwa tofauti.
Bintize mzee Mate walipokamilisha shule za msingi, alidai walikuwa wamesoma vya kutosha. Aliona hamadi kibindoni fimbo iliyo mkononi. Mkewe Asio alishikilia kuwa mvumilivu hula mbivu ambapo alionelea lazima watoto hawa wasome wamalize shule za upili.
Mzee Mate na mkewe Asio walizidi kuvutana kuhusu suala hili. Mzee Mate bila kujua tamaa ilimuua fisi, alienda kisiri akazungumza na mzee mwingine kutaka kumwoza bintiye. Asubuhi moja, mzee wa kuozwa binti zake wawili alifika nyumbani kwa mzee Mate kuleta posa. Baada ya siku chache, bintize mzee Mate walijikuta kwa mume mmoja. Walianza kuitana mke mwenza bila hiari yao. Walikatishwa tamaa katika masomo wakiwa kidato cha tatu.
Asio alilalamika kuhusu hatua ya binti zake kuozwa mapema lakini dua la kuku halimpati mwewe. Alitishwa na kunyamazishwa kwa vile mzee Mate
alikuwa amejaziwa mifugo katika zizi lake. Asio aliamini papo kwa papo kwamba kamba hukata jiwe. Alienda kisiri akashtaki mumewe katika afisi ya haki za kijinsia. Kwa kweli dawa ya dhambi ni mauti. Mzee Mate na mume wa bintize walishikwa na kupelekwa mahakamani ambapo walifungwa.
Bintize Mate walirudishwa kwa wazazi wao wakiwa wajawazito tayari. Binti za jirani waliopelekwa shuleni waliendelea kusoma wakafika chuo kikuu na kuajiriwa kazi nzuri baada ya masomo yao.
Mzee Mate alipokamilisha kifungo chake alimkataa mke wake akidai kwamba alimshtaki. Naye mume wa bintize alijuta sana akadai kurejeshewa mahari ambayo alikuwa amelipa, lakini wakati huo Mzee Mate hakuwa nayo. Mzee Mate alimjibu “Chendacho kwa mganga hakirudi.” Alikuwa ametumia mahari hayo kuponda raha kabla ya kufungwa.
Mzee Mate alijuta sana kwa kushindwa kurejesha hali yake aliyokuwa nayo hapo awali.
2. Someni na kujibu maswali yafuatayo.
(a) Elezeni maana ya juu na ndani ya methali kuhusu kisa hiki.
(b) Tajeni methali yoyote nyingine yenye maana sawa na methali iliyotumika kama anwani ya kisa hiki.
(c)Kwa kutumia kamusi ya methali au mtandao wa intaneti, elezeni maana bayana na maana batini ya methali zozote zisizopungua kumi.
Funzo i: Utaratibu wa kuandika insha ya onyo na ilani
Stadi: Kusoma na Kuandika
i. Onyo
Shughuli 4.9: Kueleza utaratibu wa kuandika insha ya onyo na ilani.
Zingatia
Hii ni taarifa inayomtahadharisha mtu kwa ajili ya kumwepusha na jambo baya.
Katika vikundi,
1. Someni mfano ufuatao wa insha ya onyo kisha mjadiliane kuhusu sehemu
za muundo wake.
ONYO!
HATARI YA KUPITIA BARABARA YA KISENYI BAADA YA SAA MOJA JIONI
Baraza la Jiji la Kampala liko katika harakati ya kuboresha jiji kwa kukarabati eneo la Kisenyi kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo tarehe 14.07.2024 Baraza la jiji linajulisha umma kuwa eneo hili halitatumika kwa vyombo vya usafiri katika muda huu. Raia wanashauriwa kupitia maeneo mengine hasa baada ya saa moja jioni kwa sababu zifuatazo:
(i)Umeme haupo katika sehemu hii kutokana na machimbo yanayoendeshwa na baraza hili.
(ii) Mashimo na mitaro mikubwa inayotokana na machimbo haya ya kuweka vifaa vipya vya barabarani ni hatari na yanaweza kusababisha ajali.
Baraza la Jiji la Kampala,
Sanduku la posta 20011, Kampala.
Funzo j: Uandishi wa onyo
Stadi: Kuandika
Jinsia
Shughuli 4.10: Kuandika onyo dhidi ya ubaguzi wa kijinsia katika jamii.
Katika vikundi,
Shirikiana katika kuandika onyo kuhusu ubaguzi wa kijinsia.
Assignment
ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli jumlishi: Jinsia MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days