• LOGIN
  • No products in the cart.

Mada kuu 4.6: Magonjwa

Ugonjwa ni hali ya kukosa afya nzuri na utendaji unaostahiki ndani ya mwili wa mwanadamu. Kuna magonjwa ya aina mbalimbali na kila ugonjwa una dalili zake. Je, ni magonjwa yapi unayoyajua? Je, unaweza kutambua dalili yoyote ugonjwa wowote?

Maneno muhimu:

  1. dalli
  2. UKIMWI
  3. kujikinga
  4. seli
  5. saratani
  6. tiba
  7. athririka
  8. onyo
  9. barakoa

Utangulizi

Ugonjwa ni hali ya kukosa afya nzuri na utendaji unaostahiki ndani ya mwili wa mwanadamu. Kuna magonjwa ya aina mbalimbali na kila ugonjwa una dalili zake. Je, ni magonjwa yapi unayoyajua? Je, unaweza kutambua dalili yoyote ugonjwa wowote?

Ni mazoea yapi yanayoweza kumsaidia binadamu kutokumbwa na magonjwa mbalimbali? Mada hii itakuwezesha kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na magonjwa pamoja na vipengele vya lugha mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano yako ya kila siku.

Funzo a: Msamiati wa magonjwa

Shughuli 6.1:

Stadi: Kusikiliza na kuzungumza Kutambua msamiati wa magonjwa mbalimbali.

Katika vikundi,

1. Tazameni na kutaja aina za magonjwa yanayoweza kuwa yanauma watu katika michoro ifuatayo;

Magonjwa

2. Mtajie mwenzako magonjwa mengine yasiyopungua matatu yanayoathiri binadamu.

Funzo b: Dalili za magonjwa mbalimbali

Stadi: Kusikiliza na kuzungumza

Shughuli 6.2: Kubainisha dalili za magonjwa mbalimbali.

Katika vikundi;

Kwa kurejelea michoro na msamiati wa magonjwa mbalimbali mliyojadili katika shughuli 6.1 hapo juu, mweleze mwenzako dalili za magonjwa hayo mliyojadili.

Funzo c: Kinga dhidi ya magonjwa

Shughuli 6.3: Stadi: Kusikiliza na kuzungumza Kueleza kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Katika vikundi;

Funzo d: Kinga dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI

Stadi: Kusikiliza, kuzungumza na kuandika

Shughuli 6.4: Kueleza kinga dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI

Katika vikundi; 1. Tazamaeni na kujadili njia za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI zinazotumiwa na wahusika katika picha zifuatazo.

Funzo e: Ufahamu

Stadi: Kusoma na kuandika

Shughuli 6.5:Kusoma makala yanayohusu ugonjwa wa saratani na kujibu maswali.

Katika vikundi, Shirikiana katika kusoma na kujadiliana juu ya taarifa katika ufahamu na kisha mjibu maswali yatakayofuata.

Maradhi ya Saratani

Maradhi ya saratani za aina mbalimbali yamekuwa tishio kubwa si kwa raia wa Uganda tu, bali kwa ulimwengu mzima. Saratani pia hujulikana kama kansa. Ugonjwa wa saratani hutokana na kukua kwa seli za mwili kwa njia isiyokuwa ya kawaida.

Wataalamu wamethibitisha kuwa matumizi ya sukari nyingi sana huwezesha seli za kansa kuongezeka zaidi na kuchangia mgonjwa kudhoofika sana. Wagonjwa wengi katika bara la Afrika wameathirika na saratani katika sehemu mbalimbali za miili yao kuanzia kwenye ngozi na hata katika viungo vya ndani ya mwili. Kansa ya akili imechangia wazimu katika baadhi ya watu. Wengine wameugua kansa za mapafu, wengine wakasumbuliwa na kansa ya njia ya kizazi, na kansa ya koo miongoni mwa kansa nyinginezo.

Huu ni ugonjwa hatari ambao unaweza kuvamia sehemu moja na kuiharibu kabisa au uhame kutoka sehemu moja ya mwili hadi sehemu nyinginezo. Si ugonjwa wa kufanyia mchezo hata kidogo. Raia wa Afrika wametumia pesa kutafuta tiba kutoka hospitali za ng’ambo kwa vile hospitali nyingi katika nchi za Afrika zimeshindwa kuukabili ugonjwa huu. Wengi wamelipia nauli za juu za ndege ili kusaka matibabu katika nchi kama vile: Uhindi, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na kwingineko. Licha ya kutafuta tiba na kupata hasara ya pesa katika nchi za ng’ambo, bado wagonjwa wa kansa wameishia kifo.

Washauri kuhusu ugonjwa wa kansa wamesisitiza haja ya kinga badala ya kutafuta tiba. Wamesema kuwa huu ugonjwa huhitaji binadamu kuchagua jinsi ya kuishi ili kujiepusha na maradhi haya. Aina ya vyakula na kushiriki katika mazoezi ya mwili ya mara kwa mara ni miongoni mwa njia za kujiepusha na maradhi ya kansa. Wataalamu wa afya wanastahili kujitokeza kimasomaso kupitia wizara ya Afya kuelezea serikali na kuelimisha raia kuhusu njia bora za kujiepusha na kansa. Pesa zinafaa zitolewe ili kusaidia wahusika kuhamasisha raia. Hawafai kunyamaza huku jamii ya ulimwengu ikiangamia.

Maswali

Kwa kutumia kamusi, elezeni maana ya msamiati uliokolezwa katika

Elezeni jambo linalosababisha kuimarika kwa ugonjwa wa saratani kulingana na habari hii.

Andikeni aina mbalimbali za kansa zilizotajwa katika ufahamu huu.

Bainisheni hasara zozote tatu zinazowakumba wagonjwa wa kansa kulingana na habari hii.

Jadilini ushauri ambao umetolewa na wanaafya kunusuru raia dhidi a maradhi ya kansa kulingana na taarifa. ya

Kulingana na mwandishi, ni hatua zipi zinazostahili kuchukuliwa na serikali kukabili janga la saratani.

Funzo f: Sarufi

Stadi: Kusoma na kuandika

i) Kiambishi “ka” cha mfululizo

Shughuli 6.6: Kutunga sentensi kwa kutumia kiambishi ‘ka’ cha mfululizo.

Katika vikundi,

1. Someni sentensi zifuatazo na kutambua jinsi ‘ka’ ya mfululizo ilivyotumika na kisha uipigie mstari. (a) Alienda nyumbani akapika chakula akala na akarudi sokoni. (b) Nimekaa naye tukaongea na tukaelewana. (c) Daktari alifika hospitalini saa mbili za asubuhi akakagua wagonjwa akawatibu kisha akaondoka.

2. Shirikiana katika kutunga angalau sentensi kumi kwa kutumia ka ya mfululizo.

ii) Kiambishi tamati ‘ni’

Shughuli 6.7: Kutunga sentensi kwa kutumia kiambishi tamati ‘ni’. Katika vikundi,

1. Someni kifungu kifuatacho kwa kujadili matumizi ya kiambishi tamati ni kisha mwandike maneno yaliyotumia kiambishi tamati ni hicho. Ugonjwa wa kushangaza umezuka duniani! Chukueni tahadhari dhidi ya maradhi ya korona. Yatawamaliza msipojichunga. Ikibidi jifungieni nyumbani bila kutoka. Ninakwambieni msifanye mchezo wowote.

Vaeni barakoa kila mnapotoka bomani na kukaa umbali wa mita moja na nusu au mbili kutoka kwa mwenzako kila mnapokutana na watu au mnapoenda mijini au sokoni. Naweni mikono yenu mara kwa mara mgusapo ukutani, mezani na vitini katika maeneo mageni. Kumbukeni, kutomakinika ni kama kuchezea afya zenu. Ugonjwa huu ni hatari.

2. Tungeni sentensi tano tano kwa kuonyesha matumizi ya kiambishi tamati ‘ni’ katika hali zifuatazo. i) ‘ni’ cha upahali. ii) ‘ni’ cha wingi.

Funzo g: Fasihi: Novela Stadi: Kusoma

Shughuli 6.8: Kusoma novela au hadithi inayohusu magonjwa na kutathmini chanzo cha magonjwa mbalimbali.

Katika vikundi; Someni novela au hadithi yoyote inayohusu magonjwa na kutathmini chanzo cha magonjwa hayo.

Funzo h: Fasihi Simulizi: Misemo

Stadi: Kusikiliza, kuzungumza na kuandika

Shughuli 6.9: Kueleza maana za misemo mbalimbali.

Katika vikundi;

1. Jadiliana juu ya maana ya neno misemo kisha mripotie mwalimu maana iliyotolewa na kikundi chenu.

2. Undeni misemo kutokana na picha zifuatazo na kueleza maana yake.

3. (a) Kwa kutumia kamusi ya misemo, jadili misemo isiyopungua kumi na kueleza maana yake.

(b) Elezeni maana ya misemo ifuatayo:

i) Paka shume.

ii) Jamvi la wageni.

iii) Shingo upande iv) Jicho la nje.

Funzo i: Insha ya onyo

Stadi: Kusoma na Kuadika

Shughuli 6.10: Kutambua hatua za kuandika insha ya onyo na kisha kuandika onyo.

Katika vikundi,

1. Msomee mwenzako mfano wa insha ya onyo ifuatayo kisha mweleze sehemu za muundo zilizotumika kuliandika.

ONYO!

TAHADHARI YA UGONJWA WA UVIKO -19

Kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huu usiokuwa wa kawaida duniani na kuathiri nchi yetu, ningependa kwa niaba ya Wizara ya Afya kuwatahadharisha umma kuchukua hatua zifuatazo ili kujiepusha vifo:

(i) Ikiwezekana, baki nyumbani.

(ii) Nawa mikono kwa maji na sabuni kila mara au tumia kitakasa cha kuua virusi.

(iii) Kaa umbali wa mita moja na nusu au mbili kila unapokuwa karibu na mwenzio.

(iv) Punguza na ikiwezekana epuka kutumia usafiri wa umma.

(v) Usile vyakula ovyo ila tu mpaka umehakikisha ni salama.

(vi) Vaa barakoa kila wakati.

Hakikisha unasaidia watu wa eneo lako kujilinda dhidi ya virusi vya korona ambavyo vinatishia maisha ya raia.

Katibu wa kudumu,

Wizara ya Afya,

Makao Makuu Kampala,

Sanduku La Posta 7272,

Kampala.

2. Andikeni insha ya onyo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Muhtasari wa matarajio ya mada

Katika mada hii, umejifunza kuhusu: kutambua msamiati wa magonjwa. kubainisha dalili za magonjwa mbalimbali. kueleza kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. kuigiza kinga dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. kusoma makala kuhusu ugonjwa wa saratani. kutunga sentensi kwa kutumia ‘ka’ ya mfululizo pamoja na kiambishi tamati -ni cha wingi na cha upahali. kusoma na kujadili novela au hadithi inayohusiana na magonjwa mbalimbali. kueleza maana ya misemo mbalimbali. kuandika onyo kuhusu jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Assignment

Mfano wa Shughuli jumlishi:Magonjwa

ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli jumlishi:Magonjwa MARKS : 10  DURATION : 1 week, 3 days

 

Courses

Featured Downloads