To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Mavazi na Mapambo
Utangulizi
Mada hii inahusu mavazi na mapambo ya binadamu. Je, haya mavazi ambayo unaona watu wamevaa, unayajua majina yake? Je, mapambo ambayo Watu hujipamba yana manufaa yoyote? Kwa nini jamii fulani huwa na mavazi na mapambo yanayotofautiana na ya jamii nyingine? Katika mada hii, utajifunza
juu ya mavazi na mapambo ambayo huvaliwa na jamii mbalimbali na kutambua umuhimu wa mavazi na mapambo haya. Mada hii vile vile itakuwezesha kujua majina ya mavazi na mapambo mbalimbali ya jamii tofauti. Mafunzo utakayopata yatakupa uwezo wa kutumia msamiati unaohusiana na mavazi na mapambo katika mawasiliano yako ya kila siku. Mwishowe, utaweza kuthamini mavazi,
kulinda mila zetu pamoja na kuheshimu tamaduni zetu.
Stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua msamiati ya mavazi mbalimbali
Shughuli 8.1
Kutambua msamiati wa mavazi mbalimbali
Taz: Mavazi tunayovaa katika maisha yetu ni mengi sana. Mavazi haya hutegemea sana utamaduni, hadhi na jinsia ya wanaoyavaa mavazi. Je, unaweza kutambua kila vazi ambalo umevaa sasa hivi kuanzia chini hadi juu? Mtazame jirani yako na kutambua mavazi na mapambo ambayo amevaa? Hayo yote mliyotaja ndio tunaiita mavazi na mapambo.
Shughuli 8.2
Kutambua msamiati wa mavazi mbalimbali
Katika vikundi, tambueni mavazi mbalimbali katika jamii yako.
Tazameni picha zifuatazo na kutambua aina za mavazi.
Taz: Msamiati wa mavazi ni mwingi. Huwezi kumaliza kutaja mavazi mbalimbali. Hii inatokana na hali kwamba, kila jamii ina mavazi yake. Inafaa ukumbuke kuwa kuna mavazi ambayo yanabakiza majina yake kutokana na asili yake.
Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo b: Kufafanua mavazi yanayovaliwa na tamaduni mbalimbali
Ukweli ni kwamba mavazi ya kitamaduni ni mavazi ambayo huvaliwa na jamii mbalimbali ulimwenguni. Kila jamii inayo mavazi yanayoitambulisha. Je, umewahi kuhudhuria sherehe yoyote ya kitamaduni? Unaweza kutambua aina za mavazi yanayovaliwa katika tamaduni mbalimbali? Tazama picha hii kisha
ueleze kwa ufupi kuhusu vazi na utamaduni.
1.
Kufafanua mavazi yanayovaliwa na tamaduni mbalimbali Katika vikundi, tazameni picha zifuatazo na kutambua mavazi yaliyovaliwa katika picha zifuatazo.
Tambueni picha na kueleza juu ya mavazi yaliyovaliwa.
Taz: Katika funzo hili, umetambua kuwa kila jamii ina vazi lake la kitamaduni ambalo huvaliwa na kuitambulisha. Baadhi ya mavazi haya huvaliwa wakati wa sherehe. Aidha utatambua kuwa baadhi ya mavazi ni mavazi yalikopwa kutoka kwa tamaduni nyingine. Ukitaka kutambua mavazi mengi ya kitamaduni, unafaa kushikiriki katika sherehe za kitamaduni za jamii mbalimbali bila
kubagua wala kuchukia bali kwa ushirikiano na upendo. Aidha, umetambua kuwa mavazi ni vitu vinavyovaliwa mwilini kwa madhumuni ya kufunika au kuficha uchi na kuna mavazi tofauti ya wanaume na wanawake, watoto na wazee pamoja na shughuli maalum.
Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo c: Kutambua na kutaja mamiati wa mapambo
Utangulizi
Mapambo ni vitu vinavyovaliwa na watu ili kuongezea uzuri wa kuonekana kwao au kujirembesha. Kuna aina za mapambo ambazo watu huvaa ili kuwafanya wavutie macho yao na ya watu wengine kulingana na umri na jinsia. Je, unaweza kutambua mapambo ambayo hutumiwa mara nyingi ili upendeze
mbele ya watu? Katika sehemu hiii, utambua aina mbalimbali za mapambo.
Kutambua aina mbalimbali za mapambo
Katika vikundi, tambueni majina ya mapambo haya:
Tungeni sentensi sahihi kwa kutumia majina ya mavazi ya nambarl
(3) hapo juu.
Tazama picha na kutambua aina za mapambo yaliyovaliwa.
Taz:
Katika mada hii umetambua aina mbalimbali za mapambo. Kuna mapambo ambayo huvaliwa nje ya mwili na mengine ndani. Hata hivyo unafaa kutambua kuwa baadhi ya mapambo huvaliwa tu wakati wa
sherehe za kitamaduni na mengine ni mila na tamaduni za jamii. Baadhi ya mapambo ni yale yaliyokopwa. Aidha, ni muhimu utambue kuwa baadhi ya mapambo ni ya kurashia au kujiwekea mwilini na mengine ni
ya kuvaliwa. Umefahamu kuwa mapambo huvaliwa kulingana na jinsia na mengine kutumika na jinsia zote.
stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo d: Kueleza aina tofauti za watu wanaotumia mapambo mbalimbali
Kueleza aina mbali mbali za mapambo na watu
41, Shughuli 8.5
wanaozitumia
Je, unatambua kuwa mavazi na mapambo huvaliwa au kutumiwa na watu tofauti? Unaweza kutambua watu na mapambo wanayotumia?
a) Watoto wa kike
d) Wanawake
b) Wavulana c) Kina baba
e) Wazee
Umejifunza kuwa baadhi ya mapambo huvaliwa wakati wowote na mengine, wakati wa sherehe maalumu. Baadhi ya mapambo huvaliwa kulinga na utamaduni au lengo la aliyeyavaa. Hata hivyo, mapambo haya si ya lazima kwa kila mtu. Wengine hawayatumii hata kidogo.
Stadi za Lugha: Kusoma
Funzo e: Kusoma makala na kujibu maswali
Je, umewahi kutambua mavazi na mapambo ya wanawake? Ili kelewa zaidi kuhusu mavazi na mapambo ya wanawake, soma Makala haya kwa makini.
Shughuli 8.6
Kusoma makala kuhusu mavazi na mapambo ya wanawake
Someni makala haya kwa makini na kujibu maswali yanayofuata.
Mavazi ni nguo ambazo huvaliwa na watu ili kufunika miili yao. Mavazi huvaliwa kwa ajili ya kusitiri mwili wa binadamu dhidi ya baridi au jua pamoja na madhara mengine ya mazingira. Aidha, mavazi huvaliwa
kuonyesha hadhi ya binadamu pamoja na utamaduni wa jamii. Mavazi ya wanawake ni mavazi ya kipekee ambayo kwayo wanapovaa hupendeza kupindukia. Wanawake wengi huvaa mavazi ya mitindo mbalimbali
kutegemea shughuli au sherehe.
Historia inaonyesha kuwa tangu kale, tamaduni mbalimbai zimepokea mitindo mipya ya mavazi mbalimbali ya wanawake kwa sababu ya usasa. Utandawazi umeingiza mavazi ya kila aina na hivyo utampata mwanamke akiwa amevalia vazi la kitamaduni pamoja na vazi la kigeni. Kuna mavazi ya aina nyingi kama vile kitambaa, nguo, suti, ngozi au plastiki Mavazi ya wanawake hutofautiana. Kuna mavazi ya
wasichana na mavazi ya mabibi au kina mama. Kuna mavazi ya kikazi, nyumbani au sherehe. Mavazi haya huweza kuwa ya kuvaliwa mwili mzima, nusu juu na chini na kadhalika. Mavazi haya yote huvaliwa
kulingana na hali ya hewa na mazingira. Wanawake wanaweza kuvaa
mavazi mepesi wakati wa joto na mazito wakati wa baridi nyingi. wahenga hawakukosea waliposema, “mwanamke ni nguo, mgomba ni kupalilia.” Usemi huu ulionyesha kuwa mwanamke yeyote anayejipenda,
kujiheshimu kuvaa mavazi na kujisitiri, anapendeza sana. Mwanamke anayekwenda uchi hapendezi hata kidogo. Kujisitiri ni kuvaa nguo kukinga uchi usionekane. Mavazi humfanya mwanamke kuwa maalumu
na kumfanya kuwa adimu na wa kuheshimika mbele ya jamii. Mwanamke anayekwenda ofisini huvaa suti ya sketi na koti au bilausi ya rangi kutegemea mtindo na umri wake. Kama ni mama wa umri wa
wastani, yeye huweza kuvaa rinda na kilemba kichwani na kujiwekea pete au bangili, na herini. Rinda hili linaweza kuwa la kanga, au kitenge. Vilevile anaweza kuvaa rinda na koti pamoja na skafu au mtandio shingoni kwa ajili ya kuzuia baridi. Mwanamke wa Kiislamu huweza kuvaa hijabu ambayo ni ya kaniki ya rangi mbalimbali au rinda na kujiwekea kilemba pamoja na kishaufu kutegemea mazingira ya kikazi. Kama sivyo, wao hl hl lihl li kwa il Imla na kl Ifi mika kitamhaa kir.hwani.
Aidha, mwanamke anaweza kuvaa suruali ndefu na fulana, au bilausi au kimono na kujirashia kanga
au kikoi anapokuwa anafanya kazi au kusafiri. Hali hii huwasaidia kuepukana na hali isiyo ya kawaida.
Mwanamke akiwa hana lesu au kikoi, anaweza kujifunga saruni kiunoni. Mwanamke akiwa kazini
jikoni anaweza kujifunga kikoi, saruni au kanga pamoja na kuvaa, kaniki. Vilevile anaweza kuvaa
joho, kilemba, na surupwenye kutegemea kazi anayofanya. Usiku, wanawake huweza kuvaa
gauni, gaguro, shumizi, suruali fupi na kujifunika na lesu au kanga au kikoi. Wakati wa kuoga,
wanawake wanaweza kuvaa koti la kuogea. Mavazi mengine wanaoyavalia ni mavazi ya ndani
kama vile kamisi na kocho kusitiri mwili au sidiria kusitiri matiti. Wanawake huvaa kanda mbili wakiwa
nyumbani na wakati wa kuoga, buti wakati wa kazi na makubadhi ya aina mbalimbali au viatu na
Mtandao wa intaneti
stokingi. Mwanamke huweza pia kijirashia mapambo ya aina mbalimbali kama vile marashi, podo, wanja, rangi ya midomo na nywele bandia na kuongeza uzuri zaidi. Aidha, mwanamke anaweza kuweka Vito puani au sikioni, bangili, herini, vikufu, hina usoni, kago au utanda au ushanga wa kiunoni,kanta kwa wenye mvi, kigesi au kikuku mguuni, kipini puani, mkufu shingoni,nti akiwa hana uwezo wa kununua mapambo ya sikio, nywele bandia, pete ya mapambo au pete ya harusi.
Mapambo mengine yanayozidisha urembo wa kina mama na mabinti ni kupaka rangi za kucha, ukaya wa kufunika pua na uso kwa baridi na vumbi, usinga, taji kwa malkia, saa mkononi, nyerere ambao ni uzi wa thamani, mafuta na kadhalika. Ama kweli, mavazi na mapambo ya wanawakeyamekuwa na mitindo inayobadilika kwa kasi kama mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Leo hii kumetokea mavazi ya mitindo mbalimbali na kwa kuangalia tu, utaona mengi kama yana lengo la kupeleka ujumbe mahali
fulani. Mfano mzuri ni wa vimini, nguo fupi zenye mipasuo mikubwa kiasi cha kuweza hata kuona mahala miguu inapounganikia na kiuno.
Kuna vazi la mgongo wazi ambalo huonyesha umbile la mgongo wote kiasi cha kuweza kuona hata nguo za ndani kupitia mgongoni. Kuna mavazi mengine yanayoonesha vitovu. Mengine kama viguo hivi
vinavyokuwa kama suruali vinavyoshika mwili ama suruali zinazobana n.k. Mavazi kama haya mara nyingi huvaliwa wakati wa starehe za jioni ama usiku. Hata hivyo, wanaoendelea kustaarabika wanafikiri kuwa
haya mavazi yavaliwa popote. Je, ni vyema kuuficha uchi kwa heshima au kuharibu heshimu kuonyesha uchi?
Kuna mavazi ya kitamaduni yanayoonyesha tamaduni mbalimbali za Uganda kama vile Gomesi ambalo ni vazi la heshima linalovaliwa wakati wa posa na harusi. Hili huvaliwa sana na wanawake wa Kiganda.
Kuna vazi la mushanana na kikoi ambalo huvaliwa na Wanyakitara wakati wa sherehe pamoja na kilemba na taji pamoja na ushanga unaovaliwa usoni. Mavazi mengine kama vile busuti huvaliwa na
wanawake wa Kinyankole wakati wa sherehe kama vile ya kuhingira, kufuga ndoa, n.k. Kusema kweli mavazi ya wanawake ni mavazi ambayo yakivaliwa kulingana na misimu yake hupendeza na hata
kuinua hadhi na heshima ya mwanamke wa Kiafrika.
Maswali
a) Tambueni baadhi ya mavazi na mapambo yanayovaliwa na wanawake.
b) Jadiliana kuhusu mavazi ya wanawake kama mnavyoyaona katika jamii mnamotoka.
c) Toeni maoni juuyamavazi na mapambo ya wanawake kulingana na taarifa.
d) Eleza maana ya methali iliyotumika katika habari kulingana na jinsi navyoielewa
e) Nini maana ya;
f) Tambueni maneno magumu katika taarifa halafu mtumie kamusi kutafuta na kueleza maana.
Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo f: Sarufi- Kutumia vivumishi Vya -ki- ya mfanano
kutunga sentensi
Unaelewa maana ya ki- ya mfanano? Ki- ni ile ambayo hutumika kulinganisha sifa ya nomino, hali au tabia ya vitu au nomino zingine katika mazingira. Unapokuwa njiani unatembea na mtu akueleze kuwa unatembea kilevi
unafikiria nini juu ya usemi wake? Je umewahi kutumia ki- ya aina hii ambayo huvumisha matendo ya watu kwa kulinganisha tabia au hali? Katika kipengelehiki, unaenda kutambua zaidi juu ya ki- ya mfanano kwa kutumia msamiati unaohusiana na mavazi na mapambo.
Kutunga sentensi kwa kutumia ki- ya mfanano, Shughuli 8.7
a)Mubiru anavaa kiofisa.
b)Babangu anavaa kwa njia ya Kifalme.
c)Ainembabazi alijipodoa kitausi akaonekana kama malaika.
d)Huyu Masaaba anapenda kuvaa mavazi ya kike!
e)Daktari anauliza maswali ya kijinga juu ya mavazi yangu.
2.Tungeni sentensi zenu mkifuata mifano katika 1 hapo juu ukurasa.
3.Tungeni sentensi tano kuonyesha matumizi ya ki- ya mfanano ukitumia
hali zifuatazo;
c) ya kiubunifu
b) ya kifahari
a) ya kiajabu
d) ya kimaisha e) ya kihistoria
Taz: ki- ya mfanano inatumika kulinganisha vitu viwili vilivyo na sifa zinazofanana au karibu kufanana. Inaleta mfanano ambao ungeletwa na maneno; kama, mithili ya, n.k
Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo g: Kutambua wakati usiodhihirika, kuutumia katika sentensi na kukanusha
Wakati usiodhihirika ni wakati ambao haujulikani. Unaweza kupata mtu akitoa maagizo juu ya kutekelezwa kwa jambo lakini unashindwa kuelewa ni wakati gani kitendo kitafanyika. Kwa mfano ukisikia mtu anasema kuwa kalamu yaisha. Utajiuliza itaisha, inaisha au iliisha? Katika mada ndogo, hii utajifunza juu ya wakati usiodhihirika na kutunga sentensi kwa kutumia wakati huo.
Kutambua na kutunga sentensi kwa kutumia wakatiugh usio dhahiri.
a) Kutambua na kutunga sentensi kutumia wakati usiodhahiri
a) Mwalimu atusubiri darasani kusoma.
b) Chakula chako chaungua, punguza moto.
c) Gari letu laenda kwa kasi mno, punguza mwendo.
d) Suruari yako yararuka wacha kuivutia.
e) Vitabu vyote vyaloa kwa maji hebu virudishe darasani
usiodhihirika.
Taz: Katika funzo hili, umetambua kuwa wakati usiodhahiri hutumia kiambishi Cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo kurejelea kitendo kinachoendelea
kutendeka katika wakati usiodhihirika. Mifano zaidi ni hii ifuatayo:
1.Kalamu yachemka wino, ifunge vizuri isiharibu vazi lako.
2.Mfalme yuaja akivaa mapambo ya kifalme, kuweni tayari kumpokea.
3.Mchezo wafurahisha sana kwa sababu washabiki wote wa mchezo wamejibampa katika rangi za bendera ya Uganda.
4.Wasichana wa siku hizi wajipamba kitausi.
5.Gari la maarusi laoshwa na kaka yetu ili lisichafue mapambo yao.
Baada ya kutambua matumizi ya wakati usiodhihirika, mnaweza kuzungumzia Pia kukanusha sentensi ambazo mmetunga hapo juu. Kwa kushirikiana na wanakikundi wenzako jaribuni kukanusha sentensi ambazo mlitunga hapo juu.
b) Ukanushaji wa hali isiyodhihirika
Katika vipindi vya awali, mlijifunza juu ya kanuni za ukanushaji ambapo mlieleza kuwa ukanushaji huzingatia ngeli, nafsi, nyakati na hali. Je, unaweza kutambua kanuni ya kutumia katika kukanusha sentensi ambazo hutumia wakati usio dhahiri? Jadiliana na wenzako kutambua jinsi ya kukanusha sentensi zilizomo katika wakati usio dhahiri.
l.Katika vikundi, tambueni vikanushi katika sentensi zifuatazo:
a) Anita hampendi mtu mwenye amejipamba sana.
b) Chema hakijiuzi, kibaya hakijitembezi.
c) Mkulima havai mapambo wala kujirembesha.
d) Batamuriza hanunui mikufu wala bangili kwa sababu hapendi
mapambo.
e) Namazzi halii asiponunuliwa nguo nzuri bali asubiri wakati mwingine.
2.Kanusheni sentensi zifuatazo:
a) Mbabulime ashukuru kwa msaada wenu.
b) Baluku apenda kula ugali wa muhogo kila baada ya kuvaa kiofisa.
c) Ritah ajihisi mkamilifu akivaa vipuli, rinda la madoadoa na kujipaka
manukato.
d) Vazi lapendeza sana.
e) Mapambo haya yapendeza sana.
3.Elezea mambo uliyotambua kutokana na ukanushaji wa wakati usiodhahiri
Taz: Katika ujifunzaji wako, umetambua kuwa viambishi vya ngeli vinazingatiwa pamoja na nafsi. Ni muhimu kuelewa kuwa ukanushaji wa wakati usiyo dhahiri hukanushwa kwa kutumia utaratibu wa wakati uliopo.
Fasili Simulizi
Stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo h: Kuchanganua semi mbalimbali na kueleza maana zake
Kueleza maana ya semi mbalimbali
Shughuli 8.9
1.Katika makundi, tambueni semi angalau kumi zinazotumika katika mazingira yak0.
Elezeni maana ya semi mlizotambua juu
Tungeni sentensi angalau tano kuonyesha maana ya semi iliyotumiwa.
Tambua maana ya semi zifuatazo na kutunga sentensi
a) Mkono wa birika b) Piga darubini c) Kufa kiofisa
e) Salimu amri
d) Angua kichek0
Taz: Katika kidato cha kwanza na cha pili, tulieleza kuwa semi ni tungo au kauli tupi za kisanaa zenye maana au mafunzo muhimu ya kijamii. Umejifunza kuwa semi hutumika kulingana na mazingira na muktadha. Aidha. umeelewa kuwa unaweza kupamba lugha kwa kutumia semi ili
kukuza na kuvutia mawasdiano.
Stadi za Lugha: Kusikiliza Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo i: Kutambua hatua za kuandika insha ya mdokezo
Kudokeza ni kugusia jambo. Insha ya mdokezo ni insha ambayo hudokeza wazo, kisha anayesikiliza kulitambua na kuliendeleza kulingana na fikra zake. Je, umewahi kuelezwa juu ya jambo na ukalikamilisha kulingana na mawazo yako bila kwenda nie ya muktadha? Je, unatambua hatua za kuandika insha
ya mdokezo? Mada ndogo hii itakuwezesha kutambua hatua za kuandika insha ya mdokezo. Hata hivyo, ili kuweza kutambua hatua hizo vyema, ni muhimu kuzingatia shughuli ifuatayo;
Kutambua na kueleza hatua za kuandika insha ya
Shughuli 8.10
mdokezo
Taz: Umejifunza kuwa kuna hatua mbalimbali ambazo huzingatiwa katika uandishi wa insha ya mdokezo. Kwanza kabisa ni kusoma mdokezo wenyewe na kutambua kisa ambacho kinaendana na mdokezo. Pia umeelewa kuwa ni muhimu kuandaa vidokezo vya kisa unachofikiria
kama maandalizi ya kuandika insha husika. Baada ya hapo, unatafuta kichwa mwafaka ambacho huendana na mdokezo na kujenga muundo wa utangulizi, mwili na hitimisho. Fikiria jinsi utakavyomalizia kwa sababu kimalizio chako ndicho muhimu. Ni muhimu kutumia mapambo ya lughana kuifanya insha yako kuwa ya kuvutia na hati yako kuwa ya kupendeza
katika mcho ya wasomaji.
Stadi za Lugha: Kuandika
Funzo j: Kuandika insha ya mdokezo
Baada ya kuelewa hatua mlizojadili katika vikundi, ni wakati wa kujieleza kwa kufanya shughuli ya kuandika insha ya mdokezo. Je, unaweza kuandika insha ya mdokezo?
Kutambua na kueleza hatua za kuandika insha ya
Shughuli 8.11
mdokezo
Katika vikundi, andikeni insha ya mdokezo juu ya mavazi ya kitamaduni yenye maneno kati ya 200-250. Baada ya kuiandika insha kwenye chati, tundikeni Chati yenu kwenye ukuta ili vikundi vingine viihakiki na kutoa maoni.
Assignment
ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Mavazi na Mapambo MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days