• LOGIN
  • No products in the cart.

Sherehe za Kitaifa

Sherehe za Kitaifa

Utangulizi
Kila taifa ulimwenguni huwa na sherehe za kitaifa ambazo linasherehekea kila mwaka. Sherehe hizi huwa ukumbusho wa mambo muhimu yaliyotendeka katika taifa hilo. Sherehe hizi ni tofauti sana na sherehe za kimataifa. Je, unajua Sherehe yoyote ambayo taifa lako husherehekea? Ni sherehe ngapi ambazo nchi yako husherehekea? Katika sura hii, unatarajiwa kutambua msamiati unaohusiana na sherehe mbalimbali za kitaifa pamoja na vipengele vya lugha husika ambavyo vitakusaidia katika kukuza na kuendeleza mawasiliano yako ya kila siku. Baada ya somo hili, utakuza uzalendo, kuheshimu na kushiriki katika sherehe za kitaifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi yako.

Stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua sherehe mbalimbali za kitaifa
Utangulizi

Kila nchi huwa na sherehe ambazo zinathaminiwa sana. Siku za sherehe hizi zinapokuwepo, shughuli nyingine rasmi huwa zinasimamishwa kwa ajili ya kusherehekea siku hizi. Je, unaweza kutambua baadhi ya sherehe ambazo husherehekewa? Je, unaweza kutaja sababu za kuwapo kwa sherehe hizo? Mada ndogo hii itakuwezesha kuthamini sherehe mbalimbali za kitaifa na kueleza sababu za kuwepo kwa sherehe hizo.
jadiliana na mwezako ili kutambua sherehe za kitaifa, Uganda.

‘ Kutambua sherehe mbalimbali za kitaifa
Katika vikundi, tambueni sherehe ya kitaifa katika picha hii.

Baada ya kutambua siku hizi, tambueni siku ya maadhimisho ya sherehe ya kitaifa husika.

Taz: Katika sehemu hii umetambua siku mbalimbali za kitaifa na siku ambazo sherehe hizo husherehekewa. Ni muhimu sana kukumbuka tarehe hizi na kuziweka katika kalenda yako kwa sababu ni kinyume na sheria kufanya kazi hasa siku hizo wakati watu wengine wanasherehekea. Zamani, watu
walitozwa faini kwa sababu ya kudharau siku hizo na kutoonyesha uzalendo. Kwa hiyo ni muhimu kuonyesha uzalendo na kuheshimu siku za kitaifa.

Stadi za Lugha: Kusikiliza Na Kuzungumza
Funzo b: Kusimulia hadithi Juu ya Sherehe za Kitaifa
Utangulizi

Watu husimuliana hadithi kutokana na matendo ambayo wamewahi kusikia, kutazama, kushuhudia au hata kushiriki moja kwa moja. Je, umewahi kusimuliwa, kutazama, kusikiliza au kushiriki katika sherehe za kitaifa katika nchi yako? Ikiwa umewahi kuhudhuria sherehe ya kitaifa, je, unaweza kusimulia hadithi juu
ya siku kuu mbalimbali za kitaifa ambazo uliwahi kuhudhuria? Mada ndogo hii itakuwezesha kusimulia hadithi za kusisimua kuhusu sherehe za kitaifa.

Kusimulia hadithi juu ya sherehe ya kitaifa

  1. Katika vikundi, simuliana hadithi au visa mlivyowahi kutazama katika runinga,
    kushuhudia au kusikia kuhusu sherehe ya kitaifa mliyowahi kushuhudia.
  2. Kila kikundi kichague mtu mmoja asimulie hadithi mbele ya wanafunzidarasani.

Taz: Umejifunza mengi kutokana na masimulizi ya hadithi kuhusu sherehe za kitaifa nchini mwako. Umetambua siku ambapo sherehe hizo hufanyika na shughuli ambazo hutendeka katika hafla hizi. Pia umetambua kuwa katika sherehe hizi, kuna mambo ya kuvutia na ujumbe ambao hupokelewa kutoka kwa viongozi wetu wa kitaifa. Hivyo unastahili kukuza uzalendo kwa kusherehekea na wazalendo wengine kuhusu sherehe hizi muhimu ili kuendeleza uzalendo, umoja na ushirikiano wa watu katika taifa lako.
Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo c: Kueleza Umuhimu wa sherehe za kitaifa
Utangulizi

Nchi yoyote tukufu, haiwezi kuacha shughuli rasmi za kuendeleza uchumi na wananchi wake na kuweka siku ya kupumzika na kusherehekea sherehe bila sababu. Sijui kama umewahi kujiuliza kwa nini nchi huchagua siku ya kitaifa kusherehekewa. Je, umewahi kutambua umuhimu wa sherehe ambayo umewahi

kuhudhuria? Kama hujawahi kutambua, je, umewahi kusikiliza hotuba ambazo hutolewa katika siku za kitaifa? Mada ndogo hii itakuwezesha kutambua na kueleza umuhimu wa sherehe za kitaifa.

1.Kueleza umuhimu wa sherehe za kitaifa
Shughuli 3.3
Katika vikundi, jadiliana kuhusu umuhimu wa kila sherehe ya taifa.
2.Baada ya kujadiliana, elezeni umuhimu wa sherehe za siku kuu za kitaifa.
3.Baada ya kutambua siku hizi, tambueni siku ya maadhimisho ya sherehe ya kitaifa husika
Kuigiza sherehe za Kitaifa
Katika vikundi, igizeni sherehe kuu ya uhuru mbele ya wanafunzi wadarasa lenu.

Raisi
Msemaji
(Akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni waa/ikwa, kujenga nchi uza/endo, umoja na ushirikiano, kupinga ukabi/a na kuwa na /ugha moja. Anazungumzia kupinga uha/ifu na wizi wa ma/i ya umma na
kuwashukuru wageni na wananchi kufika) (baada ya hotuba ya Raisi anawae/ekeza watu kwenda ku/a na
kurudi kwa matumbuizo)

Stadi za Lugha: Kusoma
Funzo d: Kusoma makala kuhusu uzalendo na kujibu
maswali
Utangulizi
Uhuru wa nchi haupatikani tu kwa maneno bali kwa kujitolea kwa baadhi ya wazalendo wanaojitolea kwa ajili ya kupigania haki na ukombozi wa nchi yao. Je, unaweza kutambua baadhi ya wazalendo hao katika nchi yako na kuelezea michango yao katika uhuru wa taifa la Uganda? Mada hii itakuwezesha kukuza
ustadi wa kusoma makala kwa ufasaha.

1.Kusoma makala kuhusu wazalendo waliopigania uhuru
wa taifa
Tambueni wazalendo katika picha zifuatazo hapa chini.
2.Soma kwa makini makala yafuatayo kuhusu wazalendo waliopigania uhuru wa taifa la Uganda.

Uganda ni nchi iliyoongozwa na wazungu kutoka Uingereza kuanzia wa mwaka 1894 hadi mwaka 1962. Wazungu walipofika Afrika Mashariki, walitambua kuwa haingekuwa rahisi kuitawala nchi ya Uganda wao wenyewe. Kwa sababu hiyo, waliafikiana kuitwala kwa kuwatumia wanauganda wenyewe. Katika mpango
huu, Ufalme wa Buganda, Bunyoro, Tooro na Ankole ulishirikishwa sana kuona kuwa Uganda inawekwa mikononi mwa wakoloni.

Hata ingawa ufalme wa Buganda ulichukua nafasi kuu katika utawala wa kikoloni, mnamo mwaka wa 1897, mzalendo wa kwanza kupinga utawala wa kikoloni alikuwa Mfalme Mwanga. Mwanga alipinga utawala wa wakoloni na kupigania haki na uhuru wa watu wake, hali iliyosababisha kuondolewa kwake
madarakani na wakoloni. Badala yake akachaguliwa mfalme aliyekuwa mtoto
sana kwa jina la Mfalme Daudi Chwa.
Wakoloni walipochukua Uganda na kuifanya koloni yao, walikimbia kuangamiza jamii ya Bunyoro kuanzia mwaka 1894. Mfalme wa Bunyoro kwa jina la Kabalega, alipigana na wakoloni kwa sababu kadhaa. Sababu moja wapo ilikuwa kwamba wakoloni walitumia viongozi wa Buganda kukusanya ushuru kwa kiburi na madharau; kutumia watu wake kufanya kazi bila malipo na kuwanyanganya ardhi yao ya Buyaga na Bugangaizi. Ukinzani wake ulionyesha uzalendo wa
kutetea haki na uhuru wa nchi ya Uganda.
Mfalme huyu alifanikiwa kuwashinda wakoloni kwa msaada wa Chifu wa jamii ya Acholi- Payira Awich Abok kutoka kaskazini mwa Uganda. Umoja waliouonyesha uzalendo wa kupinga utawala wa wakoloni bila kujali ukabila. Mfalme Kabalega alikuwa na jeshi lililowezeshwa vyema kwa jina la ‘Abarusura.’Mfalme alihusika moja kwa moja katika vita hivi kwa kuliongoza jeshi lake lililomshinda mkoloni. Hata hivyo, baada ya upinzani wa miaka mitano, Mfalme alikuja kushikwa na wakoloni Tarehe 9 /4 /1899. Alishikwa na kufungwa katika kisiwa cha Seychelles kwa kupinga utawala wa Kikoloni.

Kufikia mwaka wa 1919, jamii za Acholi na Langi nazo zilipinga utawala wa’ Union, mwaka wa 1947. Chama hiki kilipokelewa na watu pamoja na makundi Kikoloni walitaka Wahindi kuondolewa katika mchakato wa biashara ya Kutokana na masharti yaliyowekwa na wakoloni, Ignatius K. Musazi alianzisha chama cha Muungano wa wakulima nchini Uganda cha ‘Uganda African Farmers Kaskazini mwa Uganda. Mnamo mwaka wa 1945 kulitokea mpinzani mwingine Ignatius K. Musazi aliyechochea mgomo wa wakulima. Mgomo huu ulishirikisha baadhi ya wafanyabiashara na wakulima kuhusu bei ya pamba na kahawa. Pia mengi
ya wakulima na wazalendo kutoka maeneo ya Bugisu, Teso, Lango, na Busoga. Aliungana na wananchi wengi kutoka katika kila eneo la Uganda kupinga utawala wa kikoloni kama vile Otema Alimadi kutoka Gulu, Cuthbert Obwangor kutoka Teso, George Magezi kutoka Bunyoro na wengine wengi kutoka Mashariki mwa Uganda. Lengo lao lilikuwa kujiuzia pamba na kahawa bila kuwepo kwa mawakala. Msukumo wake alichochea mgomo wa kupinga utawala wa Kikoloni ambao ulitokea mwaka
wa 1949. Nyumba za machifu wa Kikoloni ziliteketezwa katika mgomo huu. Mgomo wao ulitokana na sababu kuu za bei ya pamba, kuondolewa kwa Wahindi katika biashara ya pamba na haki ya kuwakilishwa na mwakilishi wao kuliko machifu
walioteuliwa na wakoloni na Mfalme ambaye hakuwa anawasaidia katika kupata haki na masilahi yao. Aliamua kuacha kazi yake ya ualimu katika Chuo Kikuu cha

wakulima na makundi ya mashirika pamoja na kuung’oa unyonyaji wa wakoloni. Baada ya chama chake kutupiliwa mbali na wakoloni, aliunda chama kingine Cha Federation of Partnerships of Uganda African Farmers Union (FPUAFU). Lengo la chama hiki lilikuwa ni kuwashirikisha watu wote bila kujali ukoloni. Musazi alikataa kushindwa na vikwazo vya wakoloni na kuendelea kupigania haki za wakulima.
Kupitia kwa chama hiki, aliweza kuwapata vijana wenye nguvu kumsaidia katika kuendeleza upinzani dhidi ya wakoloni. Miongoni mwa vijana hao ni Abubaker K. Mayanja na Henry Lwanga. Baadaye, Musazi alitumia chama
chake cha wakulima cha FPAUFU kukomboa nchi ya Uganda kutoka kwa wakoloni. Kwa ushirikiano na Abubaker K. Mayanja pamoja na Kironde Lule, walianzisha chama cha kisiasa. Chama hiki kinatambulika vikamilifu katika upataji wa uhuru. Hali hii ndiyo inawafanya wazalendo hawa kuitwa mashujaa
aliopigania uhuru wa nchi yetu Uganda.

Hatuwezi kumalizi uzalendo wetu bila kuwataja Benedicto Kagimu Mugumba Kiwanuka, waziri wa kwanza aliyepigania uhuru wa nchi yetu kwa kuunda chama cha Kidemokrasia cha Uganda (DP). Alichangia pakubwa kwa kuwapa Wanauganda motisha ya kuchagua kiongozi wa Uganda. Mzalendo mwingine
alikuwa Mfalme Kabaka Freddie wa chama cha Kabaka Yekka. Aliunda chama hiki kupigania masilahi ya Buganda. Alipokataa uongozi wa wakoloni alipelekwa kizuizini kule London. Baadaye alirudishwa madarakani baada ya kutambua kuwa hawakuwa na mtu mwingine aliyeweza kuwasaidia kufaulu kwa sera zao. Milton Obote naye aliunda chama cha wananchi cha Uganda Peoples Congresss
kupinga utawala wa kikoloni wa kuiweka jamii ya Buganda mbele na kusahau nchi nzima ya Uganda. Kwa sababu watu walikuwa wamechoka na uongozi wa Mfalme Frederick Walugembe Mutesa II, na Chama cha DP kilichoundwa kwa ajili ya kupinga wakoloni kuwaamulia juu ya Uongozi wao. Hali hizi zilisababisha wazalendo wa Kabaka Freddie na Obote kuungana katika uchaguzi wa kidemokrasia ulioiweka nchi ya Uganda kuwa nchi huru. Kwa kweli wazalendo Milton Obote, Kabaka Freddie, Mayanja, Kiwanuka na
Lule wataheshimiwa kwa mchango wao kwani bila wao kusimama kidede na kuunda vyama, Uganda ingalikuwa katika mikono ya wakoloni mpaka sasa. Maswali kutokana na makala
Katika vikundi, jibu maswali yafuatao katika vikundi na kuwasilsiha mbele ya wanafunzi wa darasa lenu.

Shughuli 3.6
Kujibu maswali kutokana na makala
Katika jozi, jibu msawali haya:
I.Je, umepata kutambua wazalendo waliopigania uhuru wa Uganda?
2.Kwa kutaja kila mzalendo, onyesha kero yake ya kupinga ukoloni waWazungu.
3.Miongoni mwa wazalendo waliopigania uhuru, ni wazalendo wepi ambao
kweli bila mchango wao nchi ya Uganda haingeweza kupata uhuru wake?
4.Kwa makundi shirikiana na kuonyesha kwa ufupi sababu za wazalendo kupigania uhuru wa Uganda.
5.Toeni maoni ya jumla kuhusiana na wazalendo waliopigania uhuru wa Uganda.

Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo e: Sarufi – Kutambua na Kutumia vivumishi vya
Idadi katika sentensi
Utangulizi

Kila mara umekuwa ukitumia nomino katika sentensi, kutaka kumiliki nomino au kueleza takwimu ya nomino. Mzazi anaweza kukutuma sokoni kununua sukari au mayai. Kile ambacho unaweza kumuuliza mama ni idadi ya kilo za sukari au mayai. Aidha, unakwenda jikoni kupata chakula na mpishi anakupa chakula lakini unaona kuwa chakula’ hakitoshi na ungependa kuongezewa. Je, unatambua maneno
unayotumia katika kutaja idadi ya nomino au kiasi cha nomino? Mada ndogo hii itakuwezesha kutumia viwakilishi vya idadi katika mawasiliano yako ya kila siku.

Kutambua na kutumia vivumishi vya idadi na matumizi
Shughuli 3.7
1.Tambueni vivumishi vya idadi katika sentensi hizi.yake katika sentensi
a) Mwanafunzi mmoja amepata alama nzuri.
b) Wachezaji kumi na mmoja wamepunguzwa kwa kadi nyekundu.
c) Kikombe kimoja cha chai kitatosha.
d) Tunda moja limeiva.
e) Matunda matano yameiva.
f) Mgeni wako amekutafuta mara nyingi ila hupatikani.
g) Watu wengi walihudhuria sherehe ya uhuru.
Tungeni sentensi kwa kutumia vivumishi vya idadi vifuatavyo:
c) Ingi
b) Chache
a) Kidogo
d) Elfu moja e) Mara nyingi f) Kadha wa kadha

Ukanushaji wa ki- masharti
Kila ukanushaji huwa na kanuni zake. Katika vipindi vya awali, ulijifunza juu ya kanuni za ukanushaji wa -nge- na -ngali-. Katika sehemu hii utajifunza namna ya kukanusha sentensi zenye -ki- ya masharti. Kwa mfano, mtu akisema, “ukifaulu kupata umilisi wa kukariri mashairi, utakuwa mwimbaji hodari” na kwa
mtazamo wako unaona kuwa sio lazima ukariri mashairi kuwa mwimbaji hodari. Utasemaje moja kwa moja kuonyesha ukanushaji wa sentensi hii? Funzo hili Iitakuwezesha kukanusha sentensi zenye -ki- ya masharti.

1.Shughuli 3.9
Kukanusha sentensi za -ki- ya •masharti
Kwa ushirikiano na jirani yako, tunga sentensi tano zinazoonyesha -ki- ya masharti.
Kanusha sentensi zifuatazo ambazo zimetumia -ki- ya masharti.
a) Mwalimu akiwaona atawaita.
b) Mkitufikia mapema tutaweza kuwasaidia.
c) Mkikimbia sana mtachoka.
d) Mkiimba vyema mtawashinda wote.
e) Mtoto akilala nitakuja kukuona.
Kwa mtazamo wako, ni mabadiliko gani ambayo yamejitokeza katika hali yako ya kukanusha sentensi zinazotumia -ki- ya masharti?

Katika funzo hili umetambua kuwa Kukanusha ni kukataa jambo. Vilevile lazima utambue kuwa katika Ukanushaji wa ki-ya masharti, kiambishi -Sipo- huwekwa baada ya kiwakilishi cha nomino na kabla ya kitendo kuonyesha kukataa au kukanusha. Hali hii inastahili kuzingatiwa bila kuvunjwa ili kukuza mawasiliano bora ya matumzi ya KI ya masharti.

Fasihi simulizi (shairi)
Stadi za Lugha: Kusikiliza na kuzungumza
Funzo g: Kukariri Shairi
Utangulizi

Shairi lina uhondo wa aina yake unapolikariri. Je, unaweza kukariri shairi ukipewa? Unaweza kubadilisha sauti yako na kukariri shairi na kumfanya msikilizaji kutaka kusikia shairi lako kila mara bila kuchoka? Unafikiri watu hufanyaje kukariri mashairi? Mada ndogo hii itakuwezesha kukariri shairi kwa ufasaha.

1.
Kukariri shairi juu ya sherehe
Kariri shairi lifuatalo
Sote tumefurahia, madaraka kuingia,
Ni miaka kadhaia, uhuru twajivunia,
Kabaka alililia, uhuru kujipatia,
Mashujaa wakachangia, Vitani wakaingia,
Siasa wakajitia, Uhuru kujipatia.
Kabalega kakimbia, Acholi akaingia,
Umoja wakachangia, beberu akajutia,
Awich twakuvulia, kofia ya umojia,
Beberu kaangamia, Uhuru tukajipatia.
Musazi kaingia, umoja kapalilia,
Mayanya kakubalia, kujenga demokrasia,
Wakulima kuchangia, moto akaukimbia,
amri wakasalimia, Uhuru tukajipatia.

Uchaguzi ulingia, kura tukajipigia,
Obote akaingia, hatamu katushikia,
Bendera ikapepia, Shangwe heko kusikia,
Koloni kuiachia, Uhuru tukajipatia.
Obote kajivunia, siasa kuharibia,
Raia kupigania, Amini Kashangilia,
Ujenzi twajivunia, Ukatili ukaingia,
Koloni Kuitetea, Uhuru tulijipatia.
NRM ikajengeka, maendeleo twajivunia,
Mengi tumeyafikia, katiba kuzingatia,
Vyuo vikuu kungia, elimu bure sawia,
Nani asiyefahamu , Uhuru tulijipatia,

Usalama kufikia, Somalia kuingia,
Dunia kutusifia, Uganda Lulu ndo nia,
Mengi tunatarajia, fisadi kufukuzia,
Nani asopenda amani, Uhuru tulijipatia.

Mkiwa katika vikundi, tafuteni maneno ambayo mnafikiria kuwa magumu kutoka shairi hili. Jadiliana juu ya maneno hayo na kueleza maana kutokana na muktadha wa kila neno.

Stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo h: Kufafanua istiari mbalimbali
Utangulizi
Umekuwa ukisikiliza taarifa ya habari na hasa katika michezo. Watu utawasikia wakisema ngome ya Uganda Crane ni imara. Simba wa Afrika Mashariki. Aidha umekuwa ukipata wachezaji hodari wakijiita majina ambayo sio yao bali majina ya watu wengine. Unampata mchezaji hodari akijiita Drogba, Messi, n.k
huku watangazaji nao wakijiita makocha hodari ulimwenguni. Nje ya michezo,unamsikia mume akisifia mke wake kuwa amepata malaika. Je, unajua sababu za kutumia istiari? Unaweza kutaja baadhi ya istiara katika lugha yako? Mada ndogo hii itakusaidia kujifunza maana ya istiari na matumizi yake katika lugha.

1.Shughuli 3.11
2.Kufafanua Istiari mbalimbali
Katika vikundi, jadiliana kuhusu maana ya istiari na baadaye, kila mmoja
katika kikundi awatolee wenzake istiari nne kutoka kwa lugha yake.
2.Someni sentensi hizi na kutambua istiari zilizomo na kisha mfafanuemaana ya kila sitiari.
a) Hakimu huyo ni simba hachezi na wahalifu.
b) Dadangu ni Chui, akikasirika haneni na mtu.
c) Jirani yangu ni shetani/ibilisi.
d) Bwana huyo ni mchwa hufanya kazi nyingi kila siku.
e) Mzee huyo ni mbwakoko hatulii sehemu moja.
Katika vikundi, fafanua maana ya istiari zifuatazo
a) Bolt ni duma hashindiki.
b) Mitihani ya mwaka huu yamekuwa mawe.
c) Mvulana yule ni kinyonga.
d) Mwalimu wangu ni tausi.
e) Mama yako ni chiriku wa ajabu.
f) Juma ni mbilikimo.
Katika vikundi tungeni sentensi tatu kwa kutumia maneno hayakujenga istiari.
a) Theluji b) Wembe c) Bahari d) Mfuba
e) Simba

Taz: Katika funzo hili, umetambua kuwa Istiari au istiara ni tamathali ya usemi ya kulinganisha kitu kimoja na kingine moja kwa moja bila kuhusisha vilinganishi. Katika kulinganisha huku, sifa za vitu vinavyozungumziwa huwa zinafanana au karibu kufanana.

Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo i: Kutambua mbinu za kuandika insha ya Wasifu
Utangulizi

Mashujaa ni watu waliohatarisha maisha yao kwa ajili ya kuokoa jamii. Katika muktadha huu, mashujaa ni wale watu waliopinga utawala wa kikoloni na kusaidia nchi yetu ya Uganda kupata uhuru. Je, umewahi kutambua baadhi ya mashujaa katika jamii yako waliopigania uhuru wa nchi yetu? Ni mambo gani
ambayo unafahamu kuhusiana na ushujaa wao. Je, ukiulizwa kusimulia juu ya shujaa wako unaweza kusimulia na kuonyesha jinsi alivyopigania nchi yako?
Mada ndogo hii itakuwezesha kukuza ustadi wa kuandika insha kwa urahisi.

Shughuli 3.12
kutambua mbinu za kuandika insha ya wasifu

  1. Katika vikundi, jadiliana na kueleza maana ya insha ya wasifu.
  2. Jadiliana juu ya mbinu za kuandika insha ya wasifu.
  3. Kila kikundi kiwasilishe matokeo yake mbele ya wanafunzi Taz: Umejifunza kuwa insha ya wasifu ni insha inayozungumzia sifa za mtu au shujaa yeyote. Katika funzo hili umetambua kuwa insha hii huwa ina muundo wake ambao huwa unafuatwa. Kuna mkondo wa usimulizi au wa kueleza moja kwa moja kutumia nafsi ya tatu (a-). Aidha umetambua kuwa ni lazima kutumia wakati uliopita.Muundo wake huanza kwa utangulizi wa jina la muhusika na familia yake.

Stadi za Lugha: Kuandika
Funzo j: Kuandika insha ya wasifu

Kuandika insha ya wasifuKatika vikundi, andikeni insha juu ya mashujaa waliopigania uhuru
wa nchi yao. Kila kikundi kitundike insha yake ukutani ili zikosolewewanafunzi wote wakitazama.
Taz: Uandishi wa insha ni njia mojawapo ya kuwasiliana. Kwa kuandika insha hii,umeweza kutambua shujaa wako, kueleza historia ya maisha yake na kuonyeshajinsi alivyopigania uhuru wa nchi yake. Aidha kupitia kwa insha yako, umewezakutambua wazalendo ambao bado wanaishi na kuwapongeza pamoja na
kuwaheshimu kwa uwezo waliokuwa nao wa kupigania uhuru na haki yetu. Hawandio watu wanaotufanya kujivunia kuwa wazalendo wa nchi yetu.

Katika mada hii, umejifunza juu ya:
Sherehe mbalimbali za kitaifa
Hadithi juu ya sherehe uliyowahi kuhudhuria
Umuhimu wa sherehe za kitaifa
Kusoma makala kuhusu wazalendo waliopigania uhuru
Matumizi ya viwakilishi vya idadi katika sentensi
Utunzi wa sentensi kwa kutumia -ki- ya masharti na kuzikanusha
Shairi kuhusu sherehe na kufafanua istiari mbalimbali
Mbinu za kuandika insha ya wasifu
Insha ya wasifu

Assignment

Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Sherehe za Kitaifa

ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Sherehe za Kitaifa MARKS : 10  DURATION : 1 week, 3 days

 

Courses

Featured Downloads